Wabunge wa Singida, hivi Tundu Lissu sio ndugu yenu?!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,166
9,376
Damu ni nzito kuliko maji!

Nachukua fursa hii kuhoji ukimya wa Wabunge wa Mkoa wa Singida, kwa kukaa kimyaa baada ya mwenzao kuumizwa na magaidi!

Hivi mnatupa picha gani kukaa kimya pale mwenzenu anapopata shida? Hivi vyama venu ni muhimu kuliko undugu?

Hakika hili tutahoji, subirini muda ufike.
 
Mkuu kimoyo moyo wanaumia sana ila shida ni kwamba [HASHTAG]#Atubu[/HASHTAG] haeleweki hakawii kukupoteza.
 
Kwa hiyo ulitaka wafanyeje kwa mfano....waungane na Lissu kuilaani serikali ya chama chao.

Lini umewahi kuona wabunge wa Chadema wakilaani uovu wa chama chao hadharani.
Isitoshe, ni lazima pia tujue mahusiano ya Lissu na wabunge wenziye wana Singida yalikuwaje? Lissu ni mtu mgumu sana kuelewana naye, kila mtu kwake ni kibaraka wa CCM au ni mwizi. Ona jinsi anavyomkashifu Ndugai huku akimtaka aende kumsalimu Nairobi. Watasalimianaje? Wacha wabunge wa Singida, jiulize majirani zake Dodoma Area D au Tegeta Dar es Salaam: umeona wakifurika kwenda kumpa pole? Hamna, mtu ni kauli, Waafrika ndivyo tulivyo. Sasa kamgeukia Lowassa, mzee wa watu, hakumbuki kuwa naye ni binadamu ana mawazo yake na mapungufu yake na ni mzee sana kwa Lissu, ana mvi. Huwezi kumtukana hivyo.
 
Masikini mama yake!! Alizaa dude dude,lisilo na adabu.
 
Back
Top Bottom