Wabunge wa Republican wafungua kesi ya madai dhidi ya makamu wa rais Mike Pence ili kupindua matokeo ya uchaguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Wakiwa na lengo la kupindua matokeo ya uchaguzi wa Marekani, mbunge wa baraza la wawakilishi Louie Gohmert na wenzake wa Republican Jumatatu walifungua kesi ya madai dhidi ya makamu wa rais Mike Pence, ambaye ataongoza mkutano ujao wa Bunge ambao utakamilisha ushindi wa rais mteule kutoka chama cha Democratic Joe Biden.

Madai hayo, ambayo mwenyekiti wa chama cha Republican wa jimbo la Arizona Kelli Ward na wenzake pia wamejiunga nayo, yataangalia uwezo wa Pence kama makamu wa rais, ambapo sheria ya kuhesabu kura ya 1887 inasema anapaswa kuongoza mkutano mkubwa wa Januari 6 wa Bunge kuhesabu kura za uchaguzi na kuhitimisha ushindi wa Biden dhidi ya rais wa sasa Donald Trump.

Madai yanamtaka jaji wa mahakama ya Texas Jeremy Kernodle kumpa Pence mamlaka ya kipekee na uhuru pekee wa kuamua ni kura zipi za uchaguzi kutoka jimbo fulani zinapaswa kuhesabiwa.

Madai hayo yanasema sheria ya kuhesabu kura imekiuka marekebisho ya 12 ya katiba ya Marekani, ambayo yanasema Mwenyekiti wa Seneti mbele ya wabunge wa seneti na baraza la wawakilishi, atafungua vyeti vyote halafu kura ndio zitahesabiwa. Nchini Marekani makamu wa rais anatumukia kama mwenyekiti wa seneti.
 
Unaweza kuona mifumo ya wazungu inavyofanya kazi systematically and procedurally.

Hakuna ukanjanja wala janja janja za Kiswahili.

Whether you win or you lose, you are given legal avenues to pursue. Transparently and decently!

Huko Danganyika kila kitu kinaenda kwa janja janja. Kuna miungu watu wenye nguvu za giza zisizoonekana.

Nchi inaongozwa kama genge la machokoraa!

Jamaa mmoja anaweza KUAMRISHA na KUAGIZA lolote wakati wowote jinsi anavyotaka na hakuna wa kuleta fyoko. ALFA AND OMEGA.

Ukileta fyoko unagongwa rungu la utosi instantly!
 
Hivi wewe godzilla siye ndiye huyooooo mungumtu unayejisemea!??? "The are things happening in US that would have been literally unthinkable in countries like Tanzania!"~ Ruddy Giuliani
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwakweli sijui kwanini huwa simkubali kabisa Biden.
 
Wanahangaika tu. Muda wa Trump madarakani unaelekea ukingoni.
 
Back
Top Bottom