Wabunge wa Marekani kuisemea Tanzania ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa Marekani kuisemea Tanzania ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, May 17, 2012.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,100
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Posted by FJM

  Kwenye gazeti la Habari Leo (Jumapili 13/May), kuna habari inasema kuwa "Wabunge wa Marekani wataunda kamati ya bunge lao kuitetea na kuisemea Tanzania kwa kila jambo!"

  Hapa nakuwa na maswali mengi sana:
  1. Kuisemelea Tanzania kwa sababu gani? Tanzania ni taifa huru kwa nini wasemelewe?
  2. Kuisemea kwa kila jambo - maana yake nini? Mambo yote? yepi?
  3. Huu urafiki wa Tanzania na marekani unaliweka waki taifa la Tanzania?
  4. Na kwanini tunahitaji utetezi ndani ya bunge la Marekani? Ni kitu gani hasa tunakitaka ndani ya bunge la Marekani?
  5. Balozi wetu ameshindwa kuitetea na kuisemea Tanzania? Kama jibu ni ndio kwa nini tusifunge ubalozi wetu huko maana tayari bunge la Marekani linajiandaa kufanya hiyo kazi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. M

  Musia Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hizo ni sifa za nchi iliyouzwa au ambayo iko mbioni kuuzwa
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,523
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  Hujui kuwa kuna gesi huko ruvuma na ntwara? na baada ya gesi ni mafuta ..hawa jamaa wanajiweka tayari kudominate
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Rais yuko huko anakunwa chai, huku nyumbani Balozi wa Marekani anakwama kwenye lift 'eti' anaenda kumpongeza Prof Sospeter kwa kuteuliwa kuwa waziri wa Nishati na Madini. Mungu si Athumani, kama sio lift tungejuaje huu umangungo anaoufanya "black American" kwetu sisi waafrika wenziwe?

  Kuna haja ya kupitisha sheria kila baada ya miezi 6 viongozi wote wakuu (rais-mawaziri) pamoja na wabunge waweke hadharani orodha ya watu waliowatembelea.
   
 5. mtalae72

  mtalae72 Member

  #5
  May 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama wanawapa hela kila kukicha na nyie mnaunga foleni kwenda kuomba huko, basi inabidi waendelee kufanya biashara yao ambayo ni kuwasemea ili muweze kuongezewa lakini pia na wao wanafidi kwa nyie kuendelea kuwafanya miungu watu!!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,437
  Likes Received: 22,352
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 7. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani tufikiri kama ma-great thinkers. Hivi kuna ubaya gani kwa wabunge,wafanyabiashara aukundi la watu wawe wanatoka Marekani au nchi yoyote ile na waliokuja nchini na picha hasi kama vyombo vya huko vinavyopenda "kuipaka" Afrika kuahidi kwenda kuwasemea au kuitetea Tanzania na pengine Afrika na kuuweka ukweli hadharani ili kuwaumbua wasioitakia mema nchi yetu?
  Kuzungumza ukweli juu ya wanachokifahamu juu ya Tanzania kamwe hakuondoi umuhimu wa kuwa na balozi huko kwani balozi kazi yake si kuisemea nchi tu.
  Binafsi nawaunga mkono na natamani na wengine toka mataifa ya magharibi (Na hata mashariki) waliomezeshwa propaganda chafu dhidi ya Tanzania na Afrika waje wajionee wenyewe na wakaseme walichokiona ambacho kitakuwa tofauti kabisa na kinachotangazwa huko.
  Mfano rahisi ni mara nyingi tu tumekuwa tunalalamika matangazo ya ughaibuni kuwa mlima Kilimanjaro uko nchi jirani, je kuna ubaya gani hawa jamaa wakienda kwao na kusema "Hapana, tumeouona na tumehakikisha uko Tanzania, au wakafafanua vivutio vilivyopo nchini ambavyo hatujavitangaza kikamilifu?
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  uranium namtumbo na dodoma,ipo siku wajukuu au vitukuu vyetu watafukua maiti zetu kutaka kujua iq zetu kisha kuyapiga risasi mafuvu yetu
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu sijakuelwa unachounga mkono, na hunda siko peke yangu- labda utusaidie:
  Hii ni kwa Tanzania tu au ni nchi gani nyingine?
  Role ya Balozi Maajar ni nini katika hili?
  Kuna mijadal/agenda gani ktk bunge la Marekani zinayohus TZ?
  Nani kawaeleza kuhusu ya kusema au ni watakavyo kusema wao?
  Hivi wakitusemea vibaya(kwa kukosea) itakuaje?

  Napata maswali mengi lakini niishie tu hapa - tujuze mkuu walivyokueleza
   
Loading...