Wabunge wa hisani ya serikali hawezi kuisimamia serikali

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Namna katiba yetu ilivyo inahitaji bunge lenye nguvu na meno kuisimamia serikali. Lakini kwa bahati mbaya bunge letu karibu lote limejaa wabunge ambao wameingizwa bungeni kwa msaada wa tume na serikali kwa kuwapitisha bila kupingwa na njia nyingine ambazo bila hizo huenda wasingeshinda ubunge wao. Serikali imewekeza kwao.

Wabunge wa aina hiyo watalazimika warudishe hisani kwa serikali badala ya kuisimamia. Taifa linalopitia njia kama hizi linaelekea kubaya sana kwakuwa linakosa huduma ya checks and balance ambayo ni muhimu kwa ustawi wa taifa lolote makini.

Hakuna mbunge pale mwenye ubavu wa kushikilia shilingi pale mpaka dk ya mwisho kudai jamvo lenye maslahi mapana kwa taifa. Kila wakati kila mbunge anajikumbusha namna alivyofika bungeni na anaihitaji njia hiyo kurudi tena bungeni baada ya miaka 5. Atalazimika kushangilia kila kinachosemwa, kuwakilishwa na kutendwa na serikali hata kama hakipendi.

Mbaya zaidi hali hii ya wabunge inawakumba hata wale wenye elimu kubwa sana. Hata wao nao wanalazimika kukaa kimya au kushangilia tofauti na walivyokuwa kabla ya kuingizwa kwenye siasa. Bunge limejaa watu waoga walioficha hisia na weledi wao kutokana na hisani waliotendendewa na serikali kiasi kwamba ni vigumu kumtofautisha mbunge mwenye elimu ya darasa la saba na mwenye PhD, labda tofauti iko kwenye kuzungumza kiingereza linapotokea jambo linalohitaji kujua kiingereza.

Sijui tufanye kulinasua taifa na jiinamizi hili hatari kwa taifa. Mfano, mtu mmoja anaamua tuhamie Dodoma leoleo bila kujali itakuwaje kwenye maeneo mengine yatakayoathirika kwa kutekeleza jambo hilo.
 
Back
Top Bottom