Wabunge wa darasa la saba wataweza kuchangia hoja za kitaalam??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa darasa la saba wataweza kuchangia hoja za kitaalam???

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Aug 19, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimeona kwenye list ya wagombea wa CCM kuna wagombea kadhaa ambao elimu yao ni shule ya msingi, swali langu je hawa wakiwa kwenye kamati za bunge wataweza kutusaidia? Mfano mikataba karibu yote imeandikwa kwa kiingereza, na majarida mengi ya kitaalam pia yapo kwa kimombo je hawa watatoa michango gani kama hawataweza kuelewa kilichoandikwa??
  1. Jah People - Njombe Kaskazini
  2. Jamal Tamimu - Muhambwe
  3. Lameck Airo - Rorya
  4. Luckson Mwajale - Mbeya Vijijini
  5. Hussein Amar - Nyang'wale
  6. ........
  7. ........
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu huyu niliye bold ni mbunge?
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu huyu amepitishwa kugombea, kwenye mchakato kuna kushinda au kushindwa, akishinda atakuwa ndiye mbunge wa Njombe Kaskazini
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  6. Mtoto wa Abou Juma - Kibaha vijijini
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Lameck Airo ndiyo huyu jamaa mwenye LAKAIRO HOTELS - ZOO? Kama ndiye nasikia sasa kaweka mwalimu w kumfundisha kiingeleza
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  kuchangia wataweza tatizo watachangia nini?
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  John MAJOR alimaliza O-Level peke yake lakini aliweza kuongoza taifa kubwa kama Uingereza:John Major - Wikipedia, the free encyclopedia
  Waweza kukuta hao jamaa wa darasa la saba wanamapenzi makubwa na nchi kuliko wasomi waliobobea na wala rushwa wakubwa...kipi bora? Kuwa na msomi mwizi au kuwa na darasa la saba mwenye moyo na mapenzi ya maendeleo ya wanajimbo na nchi yake? what is your take?
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280


  Mkuu bado kuna Professor Maji Marefu Korogwe.Nakwambia mwaka huu tutakoma
   
 9. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Huyo jamaa ni darasa la nne jamani, hata akijifunza kingredha chenu hicho atachangia nini?? au wengine wanataka kutumia ubunge kama kivuli cha kuendeleza uharamia wao??:mad2::mad2::mad2:
   
 10. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  O level ya uingereza na la saba wa Tanzania...:sleepy::sleepy:.... sipati picha, hilo bunge litakuwa la ma mbumbumbu.... Majambazi..... wahuni..... :ballchain:
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Bunge la Tanzania linaundwa na watu kidogo wasioweza kiasi wasioweza kusoma technical documents, wengi kiasi wenye kuweza kuzisoma lakini wakashindwa kizielewa, wachache wenye uwezo wa kuzisoma, kizielewa na kutoa maamuzi sahihi na kidogo wenye uwezo wa kuzisoma, kizielewa na kutoa maamuzi ya upotoshaji

  Kwa ufupi ni kuwa bunge letu linaendeshwa na watu wachache tu wenye uwezo wa kuelewa technical papers....wengi wa walobaku wanafata maamuzi ya chama blindly
   
 12. M

  Mulugwanza Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15


  Mi naona hata darasa la saba sawa tu kwa hii nchi, kwani hata Maprofesa waliojaa huko bungeni hawana msaada wowote kwetu. Ingekuwa kusoma ndio kuna mfanya mtu awe na busara wasomi wote waliojaa mjengoni wasigekubali kodi zetu ziliwe na mafisadi wachache, kwa hiyo kwa upande wangu mimi naona hata Memkwa ni sawa tu kuwa wabunge/mawazili!
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rostam Azizi huwa anachangia nini?
   
 14. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... kama King Maker wa awamu ya dola hii, sintoshangaa akiwa kule Bungeni anafurahia matokeo ya mipango na hata jinsi alivyowafikisha jamaa wengi mle ndani MJENGONI... na kwa hiyo akichekelea BONGO INAVYOTAFUNWA naye. Hapa siweki sentensi ... jinsi Mitanzania ilivyo ya KUDANGANYWA..MIJUHA ...kwani ntakuwa najitukana mwenyewe. RA rules OK? For laughing out loudly!
   
 15. D

  Dick JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawawezi. Matarajio ya wananchi ni ndoto za mchana.
   
 16. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hilo bunge litakuwa kichekesho kama mwenyekiti wa kamati atakuwa la saba halafu mjumbe profesa realna mwingine prof maji marefu sasa sijui nanai atakubali kushindwa hapo.
   
 17. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Teheteheteheeeee!kama vipi hilo bunge wakijisahau tu nchi inapigwa mnada na hakuna wa kupinga.
   
 18. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Plato aliwakusema hivi:

  "Wale ambao ni weledi, mahiri na waadilifu lakini hawataki kuingia katika siasa, mwishowe hujikuta wakitawaliwa na watu hovyo na wajinga"

  Je haya maneno yanaanza kutimia?? Sipati picha kama hawa ndugu zangu (siyo dhamira yangu kuwadharau kwa sababu hawakupata fursa ya kupata elimu zaidi ya waliyonayo) wa std seven itakuwaje iwapo wakipewa nyadhifa za uwaziri, je wataweza kuwatendaje wasaidizi wao wanaowazidi elimu? Je pale ambapo hawa wasaidizi watataka ku-argue na mabosi wao hao maboss hawatapata inferiority complex na kuwanyanyasa??
  Haya ni mawazo yangu tu lakini nadhani elimu ni silaha muhimu katika kumuwezesha binadamu kupambana na mazingira yake. Na kwa ulimwengu wa leo wa technologia je watatufaa? Je lugha haitawakwamisha kutekeleza majukumu yao?????????
   
 19. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Suala la kujiuliza ni , je, huyu Mbungu wa darasa la saba anamwakilisha nani? Je hawa darasa la saba wanatengeneza asilimia ngapi ya wabunge? Kama elimu bila kuangalia talanta nyinginezo katika uongozi wa umma basi baraza la mawaziri 2005-2010 lingekuwa limepaisha hali ya maisha ya Mtanzania kwa sababu kuna 'madaktari' na maprofesa wa 'kufa mtu' lakini nini matokeo yake?
   
 20. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  goodluck to him. tz hakuna lisilowezekana. Hata ukimweka kichaa ikulu, the country will go on na watu wala hawatachinjana ila wataendelea kulalamika tu kwenye magazetu. TZ is the only country in the world where its people can live happily without a leader. Afterall tuna ma- dk (Phd) and some professors in the parliament, but they are just good for nothing.
   
Loading...