Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 136
Anza wewe kuonyesha uchungu wako. Usimbebeshe mtu mzigo usioweza kuubeba.kweli kabisa kama wanauchungu basi waamue kuhama na hii Nchi kabisa
Anza wewe kuonyesha uchungu wako. Usimbebeshe mtu mzigo usioweza kuubeba.kweli kabisa kama wanauchungu basi waamue kuhama na hii Nchi kabisa
Kama wao kweli wanajua kususa wasuse Posho bungeni tuwaone kama kweli wamepania.
And you are DEMOCRATICALLY IMMATURE
sasa hao wabunge wa chadema kama hawamtambui rais napia hata serikali yake hawaitambui,je wanaingie bungen kufanya nini?wangesusia kabisa bunge mpk malengoyao yatimie,ila kwa style hii ni sawa nakujambia mtoni,hakuna walifanyalo,unaingia bungen unampiga swali wazir alieteuliwa narais ambae humtambui huoni kama unatwanga maji kwenye kinu?unamtambua wazir ila aliemteua wazir humtambui,ama kweli hawa chadema wana akili kama zayule juha wakale abunuwas,wowote iwavyo PoSHO TAMU KAKA, ila nawewe sikulaum,UKIPENDA CHONGO UTASEMA NI KENGEZA
Akili na sura vinapoelekea kufanana huwaacha wenye macho mdomo wazi!kweli kabisa kama wanauchungu basi waamue kuhama na hii Nchi kabisa
kishongo nadhani umekurupuka kujuddge kuwa ni political immaturity, hiyo ni kuiamsha jamii ya kimataifa itake kujua kulikoni? lakini CUF ya leo ilipitia haya haya. hongera wewe ambaye ni politically matured!Political Immaturity.
Wewe unaishi sayari gani yaani Kikwete awasaidie wabunge wa Chadema kurudi bungeni mbona hakuwasaidia mwaka huu nafikiri unaota.
Mmh! lakini jambo lililofanyika pale bungeni ni utovu wa nidhamu kwa mamlaka iliyoko madarakani.
Mwenye political immaturity ni yule anayejisifia watanzania watakuja kwake kumlilia,jana alisema watanzania watamlilia huku akiwa na furaha,hivi rais wa nchi anaona fahari anapoliliwa?watanzania hali inapozidi kuwa mbaya JK anajawa furaha manake ataliliwa zaidi?JK aliingiza suala la udini kwenye kampeni leo anaomba asaidiwe kulifuta,hivi kama si JK+MKAPA kuhubiri udini watanzania wasingeutizama uchaguzi from religious angle.From now dini itakuwa central issues kwenye chaguzi JK ametupeleka wapi jamani?CCM +JK walishangilia kuondoka chadema bcs walijua wamepata mwanya wa kuiuza nchi KUMBE NO!Mnyukano kama kawaPolitical Immaturity.
Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah.. ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake.
Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.
Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge.
Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.
Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum nje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.
Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli.
Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza,
tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi,
Wabunge wa CHADEMA kwa pamoja wametoka nje kususia hotuba ya Rais sasa hivi.
JK itamchukua muda sana kuelewa kitendo cha Chadema kutoka nje ya ukumbi ndiyo maana badala ya kusikitika alianza kuponda mwishowe.Lakini he got touched ndiyo maana hata speech yake hakuimalizia maana nadhani aliwazia kila kitu in the eyes of wote alio waalika wakiwemo mabalozi nk .Hapo picha ime haribika and something need to be done haraka .
safari hii wakitoka tunafunga mlango mpaka bunge liishe na posho hakuna