Wabunge wa CHADEMA wapewe semina elekezi jinsi ya kufanya kazi na viongozi wa serikali

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Ukifuatilia utendaji wa wabunge wa CHADEMA utagundua kuwa hawaelewi maana ya mbunge wa upinzani ni nini? Kwao mbunge wa upinzani ni mwakilishi wa CHADEMA bungeni sio mwakilishi wa wananchi bungeni.Muda mwingi husemea mambo ambayo CHADEMA inayataka bungeni badala ya kuongelea mambo ambayo wananchi wa majimbo yao wanayahitaji wakisahau kuwa waliowapigia kura ni wananchi ambao wengi si wana chadema

Muda mwingi hata katika hoja zao nyingi hazilengi kusemea majimbo yao hujikita katika mambo yasiyohusiana na majimbo muda mwingi.Huwa wakipoteza muda mwingi kuongelea bungeni ajenda zisizohusu majimbo yao.

Pia wabunge wa CHADEMA uhusiano wao na viongozi wa serikali si mzuri kwani huenda zaidi na UCHADEMA badala ya kushirikiana na serikali kutatua kero zilizopo.Wanapenda zaidi kujionyesha wao kama wapinzani kwa viongozi wa serikali badala ya kujionyesha kwa viongozi wa serikali kama wawakilishi wa wananchi ambao wako tayari kufanya kazi kwa moyo mmoja na ushirikiano na viongozi wa serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Viongozi wengi wa serikali hawapendi kukutana na Wabunge wa CHADEMA kwa kuwa hawako friendly wagomvi gomvi tu hata kwenye mambo ambayo mtu wa kawaida mwenye akili zake asingetarajia.

Kama kuna semina elekezi wabunge wa CHADEMA wanahitaji ni namna ya kufanya kazi na viongozi wa serikali kuanzia wa vijiji hadi taifa.

Ni wajibu wa CHADEMA Kutumia ruzuku zake kufunza wabunge wake waelewe namna ya kutoa hoja za kiungwana iwe bungeni,au mje ya bunge na namna ya Kuheshimu viongozi wa serikali na kuwa rafiki nao katika utendaji kazi na pia kuwa waungwana wawapo bungeni na nje ya bunge.Wasionekane kama wahuni fulani.

Mbunge Lema,Sugu,Mchungaji Msigwa,Mnyika na Tundu Lissu,Mdee na kubenea wanahitaji sana semina elekezi.

Bila kuwa mnafiki niseme wazi Mbowe na wabunge wa CUF wanajitahidi sana.Wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi na viongozi wa serikali na kuwapa ushirikiano wenye heshima .

Ila hao wengine niseme wazi wanaifanya hata CHADEMA kionekane kama chama cha vibaka na wavuta bangi.

Mbowe wape semina elekezi
 
Mheshimiwa Mtukufu sana RAis wetu kipenzi alishasema hakuna Semina elekezi, kama wanataka wafanye kwa pesa ya Chagadema na sio pesa ya sisi walipa kodi! msitafute sababu za semina elekzi! serikali hii ya awamu yatano haina pesa ya kuchea chezea ina pesa ya kuleta maendeleao kwa Taifa na wananchi wake wafaidi keki ya TAifa.

Tunapenda kuona Kodi tunayolipa inafanya kazi za Maana kama kununua dawa mahspitali kujengwa mabarabara mpaka zile ndogo na kuendeleza miji yetu ili iendane na pesa tunatotoa
 
Mkuu,

Mwambie Rais Magufuli, awape semina elekezi hao watumishi ambao hawaelewi wajibu na mipaka yao. Wafanye kazi na wabunge wa UKAWA vizuri.

Na siyo mbaya nawe ukiwemo
 
Mburula mtoa mada,hujafanya utafiti wowote bali umekurupuka tu,ingekua wabunge wa ccm ndio wazuri rais asingekosa mawaziri katika wizara nne,acha ushabiki wa kijinga.Hakuna aliyemkamilifu tambua hilo,kubwa zima linakurupuka tu na mada za kijinga.
 
Kabisa mkuu hata mie hua siwaelewi nahisi hili jina UPINZANI lingetolewa tutafute mbadala.....

Kitendo cha kuitwa mpinzani,, hapa nahisi pepo fulani huwatawala..... Vinywani hadi akilini mwao..... Mpendekeze nini jina sahihi...
 
Ukifduatilia utendaji wa wabunge wa CHADEMA utagundua kuwa hawaelewi maana ya mbunge wa upinzani ni nini? Kwao mbunge wa upinzani ni mwakilishi wa CHADEMA bungeni sio mwakilishi wa wananchi bungeni.Muda mwingi husemea mambo ambayo CHADEMA inayataka bungeni badala ya kuongelea mambo ambayo wananchi wa majimbo yao wanayahitaji wakisahau kuwa waliowapigia kura ni wananchi ambao wengi si wana chadema

Muda mwingi hata katika hoja zao nyingi hazilengi kusemea majimbo yao hujikita katika mambo yasiyohusiana na majimbo muda mwingi.Huwa wakipoteza muda mwingi kuongelea bungeni ajenda zisizohusu majimbo yao.

Pia wabunge wa CHADEMA uhusiano wao na viongozi wa serikali si mzuri kwani huenda zaidi na UCHADEMA badala ya kushirikiana na serikali kutatua kero zilizopo.Wanapenda zaidi kujionyesha wao kama wapinzani kwa viongozi wa serikali badala ya kujionyesha kwa viongozi wa serikali kama wawakilishi wa wananchi ambao wako tayari kufanya kazi kwa moyo mmoja na ushirikiano na viongozi wa serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Viongozi wengi wa serikali hawapendi kukutana na Wabunge wa CHADEMA kwa kuwa hawako friendly wagomvi gomvi tu hata kwenye mambo ambayo mtu wa kawaida mwenye akili zake asingetarajia.

Kama kuna semina elekezi wabunge wa CHADEMA wanahitaji na namna ya kufanya kazi na viongozi wa serikali kuanzia wa vijiji hadi taifa.Ni wajibu wa CHADEMA kufunza wabunge wake waelewe namna ya kutoa hoja za kiungwana iwe bungeni,Kuheshimu viongozi wa serikali na kuwa rafiki nao katika utendaji kazi na pia kuwa waungwana wawapo bungeni na nje ya bunge.Wasionekane kama wahuni fulani.

Mbunge Lema,Sugu,Mchungaji Msigwa,Mnyika na Tundu Lissu,Mdee na kubenea wanahitaji sana semina elekezi.

Bila kuwa mnafiki niseme wazi Mbowe na wabunge wa CUF wanajitahidi sana.Wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi na viongozi wa serikali na kuwapa ushirikiano wenye heshima .

Ila hao wengine niseme wazi wanaifanya hata CHADEMA kionekane kama chama cha vibaka na wavuta bangi.

Mbowe wape semina elekezi

Ingefaa kwanza wewe upewe semina Elekezi ili ujue namna ya kuandika jambo litasomwa na watu wazima wenye akili zao na uwezo wa kuchambua mambo. .....ukipewa semina Elekezi akili yako itaacha kuandika kama unaandika barua ya ccm kutoka kwa balozi nyumba kumi kwenda shina. ..Ukipewa semina Elekezi wewe utajifunza kuandika ukweli na uhalisia uliopo kwa kuzingatia political landscape.

Ukipewa semina Elekezi kwanza wewe utajifunza kuwaheshimu wapinzani, hasa Chadema ktk kipindi cha miaka ya karibuni kwa mchango wao mkubwa ktk kubadili siasa za nchi hii na utendaji wa serikali pamoja na wananchi kujua kudai haki zao.

Uombe kwanza semina Elekezi ili uache kushabikia vyama. ....hasa liccm na maccm kwa ujumla wake.
 
Kabisa mkuu hata mie hua siwaelewi nahisi hili jina UPINZANI lingetolewa tutafute mbadala.....

Kitendo cha kuitwa mpinzani,, hapa nahisi pepo fulani huwatawala..... Vinywani hadi akilini mwao..... Mpendekeze nini jina sahihi...

Uko sahihi Ili kutoa pepo la upinzani kwenye roho na vichwa vyao badala ya kuitwa vyama vya upinzani viitwe VYAMA VYENYE MAWAZO MBADALA.Hili la kuviita vyama vya upinzani nadhani inawafanya wasijielewe.Inawafanya wajielewe kuwa wao ni sawa na wapinzani wa serikali kama akina Jonas SAVIMBI nk inawapa kitambulisho kibaya na pepo mbaya wa upinzani anawaingia kupinga kila kitu hata kama kizuri

Kama kuna TIBA MBADALA basi na vyama hivi viitwe vyama vyenye mawazo mbadala tuachane na hilo neno la kishetani lA VYAMA vya upinzani au kwa jina la pepo wa kiingereza (opposition party)
 
Mbunge wetu ni ccm. Ana shamba kubwa haliendelezwi last week wananchi walienda kulivamia akawatimua na bastola. Je huyu naye yuko sawa?
 
Hajakosea kabisa ila alisahau ilibidi awatokee na panga pia.
Magufuli kwenye kampeni zake aliahidi kuwa serikali itachukua mashamba ambayo hayajeendelezwa na kuwapa wananchi.Sasa wananchi kwa nini wasisubiri serikali iyachukue kisheria kutoka kwa mtu anayemiliki kisheria na kuwagawia kisheria? Kwa nini wajichukulie sheria mkononi.

Alichofanya huyo mbunge ni kulinda hilo shamba na pistol yake ili lisichukuliwe kinyume cha sheria.Mpe hongera kwa kutumia pistol kuzuia uvunjaji sheria
 
Mburula mtoa mada,hujafanya utafiti wowote bali umekurupuka tu,ingekua wabunge wa ccm ndio wazuri rais asingekosa mawaziri katika wizara nne,acha ushabiki wa kijinga.Hakuna aliyemkamilifu tambua hilo,kubwa zima linakurupuka tu na mada za kijinga.

Well Said, Pia Mikataba Ya Zarura Iliptishwa Na Wabunge Wa Chama Gani?
 
Ni Dhambi Kuhani Kuwa Mwongo.Sijawahi Kuona Makada Wa Lumumba Wakiwataja Vizuri Lema ,Sugu,Rev.Msigwa, Lisu, Mnyika Na Mdee.SishangaiMaandishi Yako
 
Wewe Mtoa Mada Ni Mjinga,kama Ccm Ni Wazur Kiasi Hicho Kwa Nn Amekosa Mawazir Wa Nne. Ww Naona Una2mia Akili Za Bangi Mbichi
 
Jiulize upande wa CHADEMA

Mwenyekiti wa chama Mbowe anatoka Kaskazini
Mgombea uraisi Lowassa anatoka Kaskazini
mpiga debe mkuu wa Lowasa Sumaye anatoka kaskazini
Meneja wa kampeni wa Lowasa NI mrema ANATOKA KASKAZINI
Mweka hazina wa CHADEMA kitaifa mR.KOMU anatoka kaskazini
Mwenyekiti wa akina mama Taifa -Halima Mdee ANATOKA kaskazini

Hivi kanda zingine za nchi hamna watu wa kushika hizo nafasi? Wajuaji ni hao wa kaskazini tu CHADEMA?
 
Hajakosea kabisa ila alisahau ilibidi awatokee na panga pia.
Magufuli kwenye kampeni zake aliahidi kuwa serikali itachukua mashamba ambayo hayajeendelezwa na kuwapa wananchi.Sasa wananchi kwa nini wasisubiri serikali iyachukue kisheria kutoka kwa mtu anayemiliki kisheria na kuwagawia kisheria? Kwa nini wajichukulie sheria mkononi.

Alichofanya huyo mbunge ni kulinda hilo shamba na pistol yake ili lisichukuliwe kinyume cha sheria.Mpe hongera kwa kutumia pistol kuzuia uvunjaji sheria

Mbona Lukuvi ameshaanza kufatilia na wameshaanza kupokonywa kisheria, hao utakuta ni wafuasi wa UKAWA wengi ndo wanatabia hizo za ubabe na fujo au nyuma ya hizo fujo kuna kiongozi mbovu anachochea. hii ni serikali sikivu watu wafate sheria na sio kuchukua hatua mikononi.
 
Mnafiki si rahisi kujificha...Kwa hiyo halali kwa CCM haramu kwa CDM kutetea haki zao?
 
Mbona Lukuvi ameshaanza kufatilia na wameshaanza kupokonywa kisheria, hao utakuta ni wafuasi wa UKAWA wengi ndo wanatabia hizo za ubabe na fujo au nyuma ya hizo fujo kuna kiongozi mbovu anachochea. hii ni serikali sikivu watu wafate sheria na sio kuchukua hatua mikononi.

Hata Makonda ni CDM
 
Jiulize upande wa CHADEMA

Mwenyekiti wa chama Mbowe anatoka Kaskazini
Mgombea uraisi Lowassa anatoka Kaskazini
mpiga debe mkuu wa Lowasa Sumaye anatoka kaskazini
Meneja wa kampeni wa Lowasa NI mrema ANATOKA KASKAZINI
Mweka hazina wa CHADEMA kitaifa mR.KOMU anatoka kaskazini
Mwenyekiti wa akina mama Taifa -Halima Mdee ANATOKA kaskazini

Hivi kanda zingine za nchi hamna watu wa kushika hizo nafasi? Wajuaji ni hao wa kaskazini tu CHADEMA?

Na wewe unatoka wapi?Acha ubaguzi usio na maana.
 
mtoa mada wala usiwalimishe waache wakivunja sheria wanakutana na rungu kama hivi sasa kubenea

Kubenea wala hajakutana na RUNGU bali matumizi mabaya ya MADARAKA yanaenda kumuharibia maisha ya kisiasa ya MAKONDA.Kama hakutenda jinai kwanini apore kamera za waandishi wa habari na kufuta kilichopo?Alikuwa anaficha nini??Na mbaya zaidi walikuwepo watu wengi ambao hawakuipenda tabia ya Makonda...........Naona amezoea kubebwa na hajaelewa bosi wake anahitaji nini toka kwake.
 
Back
Top Bottom