Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
CHADEMA imeazimia kuyapuuzia maagizo ya Spika Job Ndugai, aliyewataka Wabunge wote wa chama hicho wasiohudhuria vikao vya Bunge kwa sasa kurudisha posho walizolipwa, ambapo kwa umoja wao wanadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 110
Chama hicho kimesema madai ya Spika kuwa Wabunge wake waliopewa fedha za kujikimu Dodoma ni wezi, ni ya uongo na kimetoa rai kwa Wabunge kutokutekeleza yale Spika aliyoelekeza
Akitoa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema pamoja na hayo Chama kimewataka Wabunge waliotii maagizo ya kujitenga kumalizia siku zilizobaki kisha kurejea Bungeni kama hali ya #COVID19 itakuwa inatia matumaini
Itakumbukwa kuwa Mei Mosi mwaka huu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitoa waraka ulionesha kuwa Wabunge wa CHADEMA waliamua kujiweka Karantini kwa siku 14