Wabunge wa CHADEMA ndivyo tulivyo watuma mtuwakilishe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CHADEMA ndivyo tulivyo watuma mtuwakilishe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 17, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa CHADEMA wanahitaji kujua kwamba Katiba nzuri itapatikana kwa mchakato utakaofanyika Bungeni si kwenye jukwaa la Katiba kama wanavyofanya wanaharakati. Wananchi tuliowachagua tuna matarajio makubwa kutoka kwenu maana ndiyo mnaotuwakilisha katika masuala mbalimbali ikiwemo kupatikana Katiba inayokidhi mahitaji ya wananchi wa majimboni yenu na Taifa kwa ujumla. Igeni Mbunge MACHALI, MREMA, na wabunge wa CUF walioamua kupambana kwa hoja Bungeni kwa maslahi ya wananchi wa majimbo yao na Taifa kwa ujumla. Tambueni kuwa siyo tu mnategemewa na wananchi waliowapigia kura majimboni bali watanzania kwa ujumla wetu. Kama mnayo mazuri mnayodhani ni muhimu kwa taifa hili myasema Bungeni na siyo kutoka kama mnavyoendelea kufanya.

  Hivi mnaleta picha gani kwa wananchi tulio wachagua mnapotoka nje ya Bunge na kutuacha hatuna wawakilishi kwenye suala hili muhimu la Katiba na mengineyo. Au hizi ni dalili za woga kwa Wabunge wa CCM mnayoituhumu kuwa haijafanya lolote huku nyie mnawakimbia? Mnatupa wasi wasi na kutufanya tuamini kuwa mnatusaliti na kutupotezea nafasi ya uwakilishi tuliyowakabidhi ambayo ni dhamana ya maisha yetu. Mnashindwa nini kupambanisha hoja zenu mpaka mkimbie? Hii inatia mashaka na kutufanya tujiulize la kufanya mwaka 2015.

  Acheni fujo zenu, tutumikieni kama tulivyowatuma.
   
 2. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninawasiwasi kama wewe uliwapigia kura hao wabunge wa cdm.wanayoyafanya ni njia mojawapo ya kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uendeshwaji wa zoezi lenyewe.hao waliobaki bungeni wamechangia nini cha maana zaidi ya mipasho.je hiyo mipasho ndiyo waliyotumwa na wapiga kura wao?kuna wasiwasi hata mawazo ambayo wanayotoa ni yao binafsi na siyo ya wananchi.kukubali kukosolewa ndiyo ukomavu wa uelewa.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Wewe mbunge wako ulimtuma kwenda kupiga makofi,kuisifia na kuishukuru serikali kila anaposimama kuongea? Kutoka ni ku-make a statement. Kisiasa inaeleweka kabisa
   
 4. c

  cheseo Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  CUF wanapambana kwa hoja??????
  Au mkuu wewe unaangalia bunge la ANTACTICA???
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe hata uongee mpaka mapovu yakutoke lakini ikifikia kwenye wanaoafiki waseme ndiooooo na wasioafiki waseme siooooooo na spika akasema nadhani walisema ndiooo wameshinda! Hoja yako imetupwa kapuni.
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  Chadema wako sahihi ninawaunga mkono, na kwa misimamo yao ntawachagua zaidi!
   
 7. S

  Straight JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we mwehu nyamaza, hata kura yenyewe hukupiga....
   
 8. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  hujamtuma mbunge yeyote chadema wewe, uliowatuma wewe wako bungeni wanapiga makofi na kusifia mswada. Ni wafu wanaowazika wafu wenzao, ni kundi la manyumbu wanaofuata mkumbo. hakuna marefu yasiyokuwa ncha, this hypocrisy of ccm mps makes sick to core, I almost smashed my tv yesterday.
   
 9. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ninawaunga mkono Wabunge wa Chadema kwa njia waliyoitumia(walk out protest) kupinga uwakilishwaji wa muswaada "kimahepe" kwa sababu zifuatazo:
  Wako wachache ndani ya bunge kuzuia mswaada mbovu usipite,
  Kuhusiana na mchakato Kama ulivyoletwa haufai kwasababu hakuna kuaminiana Kati ya serikali na CDM kwani serikali anafanya kazi za CCM tena bila KIFICHO NA mwisho,
  Wananchi watambue kwamba kuwachagua wabunge wa CCM ni "mzigo" Kwao na wale wasiopiga kura waone athari zake(CCM haiheshimu wapigakura)
   
 10. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanachama,wapenzi na wafuasi wa chadema lazima ieleweke kwamba kitendo cha wabunge wa chadema kutoka bungeni na kugomea kushiriki kwenye mjadala wa muswada wa katiba hakina tija kwa taifa,mimi binafsi kuna mambo mengi ambayo nakubaliana na chadema lakini si kwa hili, sikubaliani nao kwa kuwa ilitakiwa washiriki mjadala ili tusikie maoni yao,waweze kuwashawishi wananchi kwa hoja zao, kama maoni yao ni dhidi ya muswada wangeyatoa bungeni yasikike ili wananchi waelewe na si lazima ccm au cuf waelewe kwa kuwa tayari wao wana malengo yao tofauti, kinachotakiwa ni wananchi waelewe, sasa watapata wapi tena hiyo nafasi ya kuwaeleza wananchi ikiwa sheria itapita ya kuzuia kutoa maoni au mawazo kwenye tume ya katiba tu na si popote pale, nawapongeza wabunge wa nccr, moses machali na agripina buyogera kwa kutumia nafasi na uhuru wao wa kikatiba kwa kutoa maoni yao bungeni, wamepinga muswada, wananchi wamewasikiliza na wapo baadhi waliokubaliana na maoni yao licha ya kuwa ccm na cuf hawakubali kwa sababu wana ajenda zao binafsi na hata kama muswada utapita lakini maoni yao wameyatoa na wananchi wamesikia sasa wale waliotoka nje maoni yao ni nini? na wamewakilishaje wapiga kura wao? basi japo watupe hoja na sababu za msingi za wao kutoka nje ya bunge na kususia kikao labda tutawaelewa.
   
 11. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Viva chadema...nimeipenda strategy yenu ya kwenda dodoma kusaini tu posho na kwenda kula starehe!
   
 12. u

  utantambua JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbunge wako ole sendeka anakuwakilisha vyema katika mchakato usihofu. Ya Chadema waachie chadema.
   
 13. A-town

  A-town JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  We tunakufahamu kula kwenda pimbi mkubwa hujitambui kibaraka wa magamba tu
   
 14. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  VGL
  Kabla ya kuwauliza wabunge wa Chadema, jiulize na wewe unamwakilisha nani. It is simple logic. Hao unaodhani hawakuwatuma wanayofanya wewe ulikutana mao kwenye forum gani na kama hamjakutana unapata wapi legitimacy ya kuwasemea?
   
 15. k

  kagosha Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Au jamani mwenzenu masikio yangu? huwa nasikia supika anasenma hivi : Wanafiki waseme Ndiyoooooo.. Na wasio Wanafiki waseme Siyooooo. Mara zote wanafiki huwa wanashinda kwa kuwa ni wengi bungeni, ha ha haaa!!!
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hope umeshapata majibu ya uzi wako
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Watanzania wa leo sio wale wa 1947. Hivyo hii mipasho yako mpelekee Steven Wasira, Ole Sendeka, Hamad Rashid na wenziwe. CHADEMA msirudi nyuma, tunataka katiba ya wananchi, iliyoundwa na wananchi, na kusimamiwa na wananchi kwa ajili ya wananchi. CCM waendelee kufanya kazi ya kuwalinda mafisadi that's what they are good at!
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Unajua tusiwe wajinga na watu wakujifanya tunatoa analysis kumbe tunaandika ujinga,upunguani na kujidhalilisha...Umetolea mfano wa Machali na Mrema...Hivi nani asiyejua kuwa Mrema ni mpinzani mfu? Uliona mchango wake? Hao CUF unaona wanachofanya? Haya Machali alijikakamua lakini Je,mawazo yake yatawekwa kwenye utendaji? Maana sio ishu ya kuongea tu tujiulize CCM ni wasikivu kiasi hiki? Ni bora kabla ujaleta wazo ujipambanue kuwa mie ni CCM nataka kuwasema CDM na sio kujifanya kuwa ni mwananchi mwelewa kumbe ni kibaraka wa magamba......
   
 19. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna aja ya maamuzi katiba mhimili muhimu kama bunge kuwa concesors na siyo majority kama ilivyo sasa.
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ukiacha maelezo mengi uliyoandika kwenye thread yako ambayo sikubaliani nayo, nataka nikujibu heading tu!

  Mbunge wangu, Mh. Lema anafanya exactly yale tuliyomtuma. Ananiwakilisha vema sana bungeni. Yaani anayafanya yale ambayo ningefanya mimi! Na kwakuwa tulimwagiza na akakubali kutokukubali upuuzi wowote wa ccm usio na manufaa kwetu, anachokifanya sasa ni kutekeleza makubaliano/ ahadi.

  God bless Lema!

  .
   
Loading...