Wabunge wa chadema kutoka bungeni mbele ya raisi ni ukomavu wa kidemokrasia


M

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Likes
0
Points
33
M

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 0 33
Kitendo cha wabunge wa chadema kutoka bungeni mbele ya raisi kimetafsiriwa kwa namna mbalimbali na jamii ya watanzania. Wapo wanaokiona kitendo hicho kuwa ni utomvu wa nidhamu kwa raisi, wapo wanaoona kama wabunge hao wamewasaliti wapiga kura wao kwa kitendo hicho. Lakini pia wapo wanaodhani kitendo hicho kinaweza kuhatarisha amani nchini. Hata baadhi ya watu wanaodhaniwa kuwa wasomi na wenye upeo mkubwa nao wameonesha mawazo kama hayo.

Kinachonishangaza na kwa kweli kunisikitisha ni jinsi bado watanzania tulivyo nyuma kwenye mwamko wa kisiasa na ukomavu wa kidemokrasia. Mwitikio huu wa aina hii na hasa ule wa wanaccm kutishia kutoa tamko dhidi ya wabunge wa chadema unaashiria uchanga wa hali ya juu kidemokrasia. Nachelea pia kuwa watanzania tuna hofu isiyo na msingi juu ya kitu uvunjifu wa amani, kiasi kwamba kila kitu tunafikira kitavunja amani. Tunakimbia hata kivuli chetu tukidhani kinavunja amani. Tumesahau amani ya kweli imejengwa juu ya misingi ya haki na ukweli, na siyo vinginevyo.

Ni muhimu kukumbuka kuwa chadema kama chama kilichokuwa kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa nchi katika uchaguzi uliopita kilikuwa kinatumia haki yake ya kidemokrasia. Na haki hiyo hiyo ndiyo sasa wanayoitumia kudai kuwa hakikutendewa haki kwa kutokusikilizwa kilipotoa malalamiko yake tume ya uchaguzi kuwa matokeo yanayotangazwa ya uraisi hayapatani na yale waliyonayo toka majimboni. Hivi jamani, mnadhani chadema ingekaa kimya tu na kuangalia matokeo yaliyo tofauti ya yale waliyonayo yakitangazwa? kuna chama chochote hata ccm kingekaa kimya katika hali hiyo?

Hata kama madai yao hayakuwa sahihi tume ilipaswa kuayasikiliza, iwaite iwape nafasi waoneshe matokeo yao hayo ya jimboni wanayosema hayapatani na yale yanayotangazwa. Kisha kama chadema hawakuwa right wangejulikana. Walichoogopa kuwasikiliza ni nini? Walikuwa na haki gani ya kudharau madai ya chama shiriki kwenye uchaguzi? Kama ccm wangekuwa ndio waathirika wangekaa kimya? Je tume ingedharau malalamiko yake? Kudharau huku kwa tume kumeonesha upendeleo wa dhahiri kwa ccm na kumewapa chadema haki ya kuyakataa matokeo. Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa kama vile ilivyokuwa haki ya kidemokrasia kwa chadema kugombea uongozi ndivyo ilivyo haki pia kuyakataa matokeo yanapokuwa yamegubikwa na utata na hasa kwa kuwa walitoa malalamiko wakanyimwa haki ya kusikilizwa.

Demokrasia ina gharama, watanzania tukue, tuache utoto wa kufikiri kuwa kila kitu ni uvunjifu wa amani. Ni lazima ijulikane kuwa mtu au chama hakiwezi tu kucheza rafu kwenye uchaguzi halafu kikakalia kiti cha utawala bila kusukwa sukwa na wapenda demokrasia. Wanopinga wabunge wa chadema kutoka bungeni wafikiri mara mbili.
 

Forum statistics

Threads 1,237,696
Members 475,675
Posts 29,297,784