Wabunge wa CCM waungana na wa Upinzani kupinga Ufisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM waungana na wa Upinzani kupinga Ufisadi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Jun 26, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siyo siri tena kuwa Wabunge wetu wameungana kupinga ufisadi.Wabunge wa CCM ambao wameonyesha njia katika mapambano juu ya ufisadi ni Selelii,Ole Sendeke,Kilango n.k.Jamani tuwaunge mkono ili tututokomeze mdudu huyu wa ufisadi nchini.Je sasa si ni wakati Serikali iwachukulie hatua wahusika/watuhumiwa wote wa ufisadi?
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii dalili njema kwa mapambano juu ya ufisadi unaolitafuna taifa letu.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Si vibaya kuungana sasa lakini wakumbuke kuwa wakati wao wanasuasua kuungana leo, adui zetu (Mafisadi) waliungana toka wanaanza kuweka mikakati ya kufisadi.
   
 4. F

  Fechee2001 Member

  #4
  Jun 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si vibaya kweli kuungana na wawe wakweli katika kuungana huko na isiwe maneno tu na vitendo vinatakiwa ili tupige hatua mbele katika maendeleo na macho ya wananchi waliowaweka madarakani/bungeni yako wazi yanawatazama. Wananchi wanahitaji watu wakujitolea kwa lilaahi katika kufanya kazi za umma na wenye uchungu mkubwa na nchi yao. Wote tufaidike na si wachache wenye kufikiri bila ya wao madarakani basi nchi haitawaliki. Watanzania ni waelewa sana wa mambo na huwa hawana papara ila subra tu. Na ikitokea watu wakianza kulalamika ni wazi kuwa kuna kitu kimezidi na kuvuka mpaka. Serikali sasa ifanyie kazi malalamiko ya wengi ili kurudisha imani ya wananchi wake dhidi yao.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  wabunge wengi wa CCM ni wanafiki tu. Kabla ya bajeti walitishia ikija kama ilivyo basi itaweka historia kwa kufanya bunge livunjwe kwa mara ya kwanza. Haya bajeti ikapelekwa kama ilivyo. Waka piga piga kelele na porojo nyingi. Siku ya bajeti kupigiwa kura ikapita bila matatizo. Sasa kweli tunaweza kusema wabunge wa CCM wanaweza kuungana na upinzani kupinga ufisadi? Mimi naona hawana lolote. Mbele ya kamera wanaongea vitu vingi sana ila behind the doors they can never chose the nation over their party. Siasa za bongo too much lip service.
   
 6. SOARES

  SOARES Member

  #6
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 6, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  The late, Mwenyeheri, JKN, alisema hivi " Mtu akisema kuwa anaichukia rushwa anatakiwa kweli aonekane kuwa anaichukia, siyo ukimtazama usoni mm... heh!" Hivi hao wanaoonekakana kupinga ni kweli ukiwatazama usoni wanasomeka hivyo? Wana JF tutafakari hilo. Pili kumesemwa kuwa kutenganisha siasa na biashara itakuwa 'solution' ya ufisadi, hivi unafikiri Fisadi akimnunua mlala hoi msemaji kweli kweli anayeaminika na wanajamii kuwa ni mlipuaji, mtajuaaa? Baada ya kuingia kwenye jumba la kutunga sheria ataanza kusema oooh "Ubaguzi wa Rangi" ooh "Gere" ooh, ni "Mzawa" aah "Huyu anawajua masikini tu sisi je, tukale wapi?" na kama hayo. Nadhani kuwepo kipengele cha wapiga kura kumpigia kura ya kutokuwa na imani mwakilishi wao kama ilivyo kwa Wabunge kwa Rais. Na fursa hii iwepo hata kama ni siku moja tu tangu kuchaguliwai kuzuia madhara zaidi.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunapaswa kuangalia kwa sasa ni kupambana na mafisadi wote,anayepambana nao ni nani tutajua baada ya kuwashughulikia mafisadi waliogundulika sasa,tuungane wote kuwatokomeza kabisa 2010.Hata wale walioanza kugawa fedha majimboni tuwafichue giliba zao.
   
Loading...