Wabunge wa CCM washindwa kunenepa sababu ya kukosa nyongeza ya posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM washindwa kunenepa sababu ya kukosa nyongeza ya posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Feb 12, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wabunge wamwangukia JK

  12th February 2012

  [​IMG] Mmoja asema ameshindwa kunenepa
  [​IMG] Wasema ni muhimu kwa kazi za ubunge
  [​IMG] Mwenyewe asema liachwe kama lilivyo  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete

  Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukanusha kuwa hajabariki nyongeza posho za wabunge, wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamemwangukia na kusema jambo hilo haliepukiki ingawa baadhi ya wananchi hawataki.

  Hayo yalijitokeza juzi usiku katika kikao chao na Rais Kikwete ambacho kilifanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma.
  Hata hivyo, baada ya kusikiliza hoja zote, hili la posho, kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, aliwatamkia wabunge hao kwa kifupi kwamba waliache suala hilo kama lilivyo.

  Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba ndiye aliyeibuka na hoja ya posho katika kikao hicho ambacho kilianza saa 2.00 usiku baada ya Bunge kuahirishwa. Nkumba alisema posho ni muhimu sana kwa kazi za ubunge, akasema yeye ni kipindi chake cha tatu cha ubunge, lakini ameshindwa kunenepa kwa sababu ya majukumu aliyonayo, kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba na kuongeza; Kwa hiyo, akasema umuhimu wa posho kwa ubunge hauepukiki ingawa baadhi ya wananchi hawataki wabunge waongezwe posho.

  Wabunge hao na Rais Kikwete, walikutana ili pamoja na mambo mengine, kujadili mwelekeo wa chama na kuangalia njia za kujiimarisha zaidi dhidi ya vyama vya upinzani. Chanzo cha habari hizi kilisema kuwa Rais Kikwete alipoingia ukumbini aliwaambia wabunge hao kuwa yeye si msemaji wa kikao hicho na kwamba amewaita ili awasikilize waliyonayo. Wabunge hao wanataka posho ya vikao iongozwe kutoka sh 70,000 kwa siku hadi kufikia sh 200000 kwa siku.

  Hata hivyo, wabunge wawili wa chama hicho wamejitokeza hadharani wakipinga kulipwa kwa kiasi hicho kipya cha posho.
  Wabunge hao ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba na Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalah.

  Chanzo hicho pia kimemkariri Nkumba aligusia suala la wabunge wa CCM kuzuiwa kugombea nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia wilayani na akataka ukweli wa jambo hili uko wapi maana kila mmoja anasema yake.

  Aidha habari zaidi zinasema kuwa, ingawa kikao kilikwenda vizuri, wabunge waliochangia walionyesha hisia zao kwa njia tofauti ili mradi wahakikishe ujumbe waliotaka kuufikisha unafika.

  Mbunge mwingine aliyesimama na kutoa hoja yake alikuwa ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy Mohamed ambaye pamoja na mambo mengine alimtaka Rais kupunguza ukimya.

  Mbunge mwingine ni wa Ludewa, Deo Filikunjombe, yeye aliwashukia zaidi mawaziri kwa kusema kuwa hawawajibiki ipasavyo.

  Alisema Filikunjombe aliwafananisha mawaziri na bidhaa ambayo ni vigumu kuandikika na kuongeza kuwa ukweli ni kwamba aliwashambulia sana mawaziri wa serikali yao. Filikunjombe aliwashambulia pia wabunge wa Viti Maalum, akasema wabunge hao wanakiharibu chama kwa sababu wanapokuwa majimboni, hawafanyi kazi za kuimarisha chama bali wanatafuta umaarufu majimboni, kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilisema Filikunjombe aligusia pia fedha za serikali zinavyotafunwa bila wahusika kuchukuliwa hatua na kutolea mfano fedha za zao la Pamba.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, wengine waliochangia ni Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugora ambaye alisisitiza umuhimu wa CCM kuwa imara kwa vile bila CCM madhubuti hakuna serikali madhubuti.

  Wengine walisimama na kuongea katika kikao hicho ni Mbunge wa Kilwa, Kaskazini, Murtaza Mangungu ambaye alimkumbusha Rais juu ya ahadi aliyowahi kuitoa mkoani Lindi ya kunununua mashine za X-ray mkoani humo.

  Kutokana na maelezo hayo na mengine, chanzo hicho kilisema Rais Kikwete aliwambia wabunge hao kuwa, amefurahi kukutana nao na pia akaahidi kuyafanyia kazi mawazo yao kwasababu yanalenga katika kuimarisha chama na Serikali.

  Kuhusu suala la wabunge wa CCM kutoruhusiwa kugombea nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kupitia wilayani, chanzo hicho kilisema Rais Kikwete alisema hawajazuiwa kama inavyosikika.

  Wakati huo huo, akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma jana, Rais Kikwete alisema kikao hicho kinalenga katika kuandaa kikao cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika leo. Alisema Nec itajadili marekebisho ya Katiba ya CCM.

  Awali Katibu Mkuu wa chama hicho, Willison Mkama, alisema kikao hicho kina wajumbe 39 na waliohudhuria ni 34 na kwamba ni halali kuendelea. Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakipingwa na wabunge wa CCM kuhusiana na marekebisho ya katiba ni suala la kura za maoni na kujilimbikizia madaraka.

  Pia suala la ubunge wa viti maalum kuwa na ukomo nalo ni jambo ambalo limekuwa likipingwa na baadhi ya wabunge wa chama hicho.

  Source: Nipashe Jumapili
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  wali[ize kisasi kama vipi
   
 3. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida ya baba Mwanaasha, hakuonekani chochote alichokisimamia wala kukitolea jibu dhahiri; kwa muonekano wa habari hii ni alikuwa tu kama mgeni aliyepita kusikia nini wanataka kusema.
  Hata hivyo, kimsingi kama mwenyekiti alifuata nini kikaoni ambacho ukisoma hapo unakiona?
   
 4. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona wafanyakazi wengine wakisema hawanenepi mnawakebehi?
   
 5. p

  pazzy Senior Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hivi mbunge anayezungumzia posho anajua mishahara wanayolipwa walimu,askari polisi na wanajeshi wetu?wabunge acheni ubinafsi baadhi ya mambo mnayoyafanya hayana tija kwajamii.... mfumuko wa bei na mazingira magumu yakazi nikero kwawatumishi wa kada za chini,msipotimiza wajibu wenu wakikatiba wakuisimamia serikali Iboreshe maslahi kwawatumishi wa UMA mtasababisha maafa kwataifa yaliyofanywa na madaktari ni mwanzo tu mengi yanakuja kwani watumishi wa uma wamekata tamaa" tanzania yenye neema niyetu sote"
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...