Wabunge wa CCM wanaoipinga bajeti watakiwa kurudisha kadi za chama

Hakuna mtu aliyeambiwa cha kufikiri bali wamepewa nafasi ya kuchagua.

Kupewa nafasi ya kuchagua ni zaidi ya kupewa nafasi ya kuchambua fikra zako na kufanya uamuzi kwa faida ya fikra zako.
Kwanini msiwape nafasi ya kuchagua either ndiyo au hapana juu ya hii bajeti hewa?
 
Mi naona ni kuminywa demokrasia ndani ya Chama. Mtoa mada hayo yalikuwa maamuzi ya Chama baada ya kaukasi ya Chama kukutana Ijumaa iliyopita 17.6.2016. Kwa kifupi hata kurekebisha kile alichopanga Mpango ni kosa..hivyo usisifie sio vyema kabisa mi mwanaCCM sijapenda kbisaa. Hii bajeti ni ngumu sana yataka wanna CCM kuijadili so tuwape kichwa upinzani
Mkuu soma mada ili uelewe vizuri au umesoma heading tu?

Mada imesema hivi;
''Uongozi wa juu wa CCM na serikali umesema mawazo ya wabunge kwenye mchango wa bajeti na michango mingine yatapokelewa na kufanyiwa kazi na serikali kwa maslahi ya taifa lakini wale wabunge watakaopinga kwa sababu ya maslahi yao binafsi hawawezi kuvumiliwa ndani ya CCM''
 
Magazeti ya leo yana habari inayosema wabunge wa tiketi ya CCM watakaoipinga bajeti ya mwaka huu wa fedha 2016/2017 wametakiwa na uongozi wa juu wa CCM na serikali kurudisha kadi za uanachama wa CCM ili wakaendeleze adhima yao kupitia tiketi za vyama vingine.

Uongozi wa juu wa CCM na serikali umesema mawazo ya wabunge kwenye mchango wa bajeti na michango mingine yatapokelewa na kufanyiwa kazi na serikali kwa maslahi ya taifa lakini wale wabunge watakaopinga kwa sababu ya maslahi yao binafsi hawawezi kuvumiliwa ndani ya CCM.

Uongozi wa juu wa CCM na serikali umebainisha kuwa hauwezi kuruhusu kuwepo bungeni na kundi lililojiandaa kukwamisha bajeti katika wakati huu ambao serikali imedhamiria kwa dhati kukuza uchumi na kufikisha huduma bora kwa wananchi hasa wa kipato cha chini kwa haraka zaidi.
Kazi ya Bunge ni kusimamia serikali.CCM ndio inaongoza serikali.Iwapo ccm imetoa tamko kuziba midomo ya wabunge hivyo hakuna sababu ya bunge kuwepo.
 
Toka lini wabunge wa ccm wakapinga bajeti ya Serikali yao, ni kwa sababu maslahi yao yameguswa, mzee wa majipu wakate tu kodi kwenye pensheni yao maana hakuna namna nyingine
 
Soma vizuri thread ili uelewe vizuri.

Kama ilivyo kawaida, nadhani umesoma heading tu na kutoa comment!

Ulichokiandika siyo kile kilichosemwa katika mantiki kwenye thread.
Hapo usilazimishe watu wafikiri/wakubaliane nawewe jinsi ulivyoelewa.Kinachoonekana ni kwamba ccm haitaki wabunge wake kuikosoa serikali/bajeti hata kama ina mapungufu.
 
Nadhani wanaosema ni Udikteta kuwaambia wabunge wanaotaka kukwambisha bajeti kwa maslahi yao binafsi hawajui wanalozungumza. Wabunge wanaruhusiwa kuhoji serikali na kuchangia bajeti ikiwemo kuipinga kwa ajili ya kuiboresha kwa maslahi mapana ya taifa, na sio kuikwamisha kwa maslahi binafsi kwa kutumika kulinda maslahi ya watu.
 
Kuna maneno yametumika hapa " Uongozi wa juu wa CCM na serikali " hii ndo inatupa shiida baadhi, kuna haja ya kutenganisha chama na serikali.
 
Hakuna kubembelezana, sababu wabunge wenyewe walikuwa wanapinga bajeti kinafiki tu.

Bora wameambiwa ukweli wachague kunyoa au kusuka.!
 
Yes of course that's one type of democracy known as "Dictatorship Democracy",

either you are with us or with them.
either you are with us or with them is the pinnacle of democracy.

Kwa nini ung'ang'anie kwenye kikundi au chama ambacho hukubaliani nacho?

Kung'ang'ania kwenye kikundi au chama usichokubaliana nacho ni unafiki.

Unafiki ni sumu katika maisha endelevu ya kikundi au chama.
 
Hii ni aibu na fedheha! Mtafanyaje kazi bila kutofautiama? Huu nao ni uonevu uliopitiliza.
 
Kwa nini bunge lifutwe wakati kuna demokrasia ya kambi mbili ndani ya bunge.

Kama mbunge anadhani hakubaliani na chama kilichompa tiketi ya kugombea, anaweza kuhamia chama kingine kama alivyofanya Ester Bulaya.
Usichanganye mambo, tatizo siyo kuhama chama bali kusikilizwa hoja yake, sio lazima kila anayekuwa na mawazo mbadala ndani ya chama ahamie chama kingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom