Wabunge wa CCM wamezinduka au wanawasafishia watu njia?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kuungwa mkono wa wabunge wa upinzania kutokana na kutetea wananchi na kufichua uvujaji wa mali ya umma, kumewafanya baadhi ya wabunge wa CCM waunge mkono hoja kwa kusaidia kufichua viongozi wao wa juu wanaotumia madaraka vibaya na kuvuja mali ya umma.Hata hivyo baadhi ya wabunge wa CCM wanajulikana kuwa katika makundi katika chama.Mfano wanamtandao,CCM asilia na CCM masilahi.Je kuzinduka huku kwa wabunge wa CCM ni janja ya kuwasafishia njia viongozi wa makundi yao?
 
Kama hauna habari, battle lines have already been drawn. Wanamikakati wameshapanga kuwa 2015 is not very far, kwa hiyo shughuli imeshaanza. Kuna makundi mawili tayari yameshapima upepo na kufikia uamuzi kuwa kazi ianze sasa. Tunachokishuhudia Bungeni kutoka kwa wabunge wa CCM wala si uchungu wa kuwatetea wapiga kura au nchi yao, ni maandalizi ya 2015. KUna kundi moja kubwa which has been caught sort of unaware, wanajipanga, naamini wataanza kujibu nmapigo karibuni. Hata kama haitakuwa bungeni, lakini tutarajie minyukano zaidi within CCM, mabomu zaidi na kadhfa zaidi. But let them be warned, wasipokuwa waangalifu, huyu atakuwa anamwoga mboga na mwingine anamwaga ugali.
 
Back
Top Bottom