Wabunge wa CCM waliounga Pinda kuwekwa kikaangoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM waliounga Pinda kuwekwa kikaangoni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 2, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]


  Wakati hayo yakiendelea, wabunge wengine watatu wa CCM ambao walisaini kusudio la kumng’oa madarakani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda nao huenda wakajadiliwa kutokana na hatua yao hiyo.

  Wabunge hao Deo Filikunjombe (Ludewa), Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) na Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara) walisaini hoja yenye kusudio la kutaka kumng’oa Waziri Mkuu, Pinda ambalo lilikuwa likitaka kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

  Habari zinasema suala hilo ni moja ya mambo ambayo yaliwagawa wajumbe wa kikao cha Halmshauri Kuu ya CCM (Nec) kilichofanyika mwezi uliopita mjini Dodoma, lakini hakuna mwafaka wowote uliopatikana. “Wapo ambao tulitaka hawa wabunge wachukuliwe hatua za kinidhamu, lakini pia wapo ambao walikuwa na msimamo kwamba wabunge hao walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba, mjadala ulikuwa mkali lakini hitimisho lilikuwa kwamba suala hilo lirejeshwe kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM,”alisema mmoja wa wajumbe wa NEC.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alithibitisha suala hilo kijadiliwa ndani ya kikao hicho na kwamba ni kweli limerejeshwa katika kamati ya wabunge wa chama hicho. “Kimsingi hoja zote zinaanzia pale bungeni, na hata hayo ambayo yanadaiwa kuwa ni makosa yalifanyika katika mazingira ya Bunge, sasa kama chama tuliona ni vyema tuiachie kamati ya wabunge wetu, nao wataangalia kwa kutumia kanuni zao kama wataona kuna kosa, basi watachukua hatua,”alisema Nape na kuongeza: “...wanatakiwa watumie kanuni zao sasa inategemea zinawaelekeza vipi, kama wanaweza kutoa adhabu sawa, kama wanalifoward (wanalileta) kwetu nasi tutalipangia utaratibu mwafaka, lakini lazima lianzie huko kwa wabunge wenyewe, sisi hatuwezi kuwaingilia”. Katibu wa Wabunge wa CCM, Janester Mhagama kwa upande wake, alisema alikuwa hajapata taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa NEC na kwamba baada ya kuarifiwa, angeweza kulizungumzia.

  “Kwa bahati mbaya katika NEC iliyopita sikuweza kuhudhuria nilikuwa na matatizo ya kifamilia, lakini niseme tu kwamba kama watatuletea kama walivyosema, basi kanuni zetu zipo na tutaangalia zinasemaje kuhusu hilo,”alisema Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho. Mhagama ambaye pia ni mmoja wa wenyeviti wa Bunge aliweka wazi kwamba anachofahamu yeye ni kwamba wabunge hao walikuwa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba lakini akakumbusha kuwa chama nacho kina nafasi yake.

  Aliongeza: “Ndiyo maana nimesema lazima twende kwenye kanuni zetu za Bunge halafu pia tuangalie kanuni zetu za wabunge wa CCM, tutapata mwafaka hakuna haja ya kuwa na haraka”. Akizungumzia suala hilo, Filikunjombe alisema kuwa aliyoyazungumza bungeni ikiwa ni pamoja na kusaini fomu ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni kwa maslahi ya Serikali na CCM.

  “Ukweli ni kwamba nilichokizungumza sikumsingizia mtu na nilifanya hivyo kwa maslahi ya Serikali yangu na chama change,” alisema Filikunjombe. Alifafanua kwamba wanaomuona adui na kutaka achukuliwe hatua na chama, wao ndio maadui namba moja wa Serikali na CCM.

  “Rais Jakaya Kikwete mwenyewe aliwahi kukiri wazi kuwa amefurahishwa na mawazo ya wabunge waliyoyatoa kuhusu suala zima la kuwajibishwa kwa mawaziri”. Aliongeza, “Unajua watu wanadhani kwamba wenye uchungu na nchi hii ni wapinzani pekee…,hilo jambo sio kweli nchi hii ni yetu wote”.

   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ili iweje kama sio kujiongezea usumbufu?
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ....teh,teh, kweli CCM inajimaliza kwa moto wake wenyewe,badala ya kuwachukulia hatua wakina Ngereja walio iba wanaenda kuwachukulia hatua waliotaka wezi wawajibike
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wawafukuze wabunge hao na kisha wahamie upinzani, na kwa jinsi wanavyokubalika majimboni mwao watakuwa wamewakomba wote kuhamia upinzani. Kitakuwa kilio na kusaga meno. Hata hivyo sidhani kama wanaweza kuchukua hatua hiyo kwani ni kitanzi kwa CCM yenyewe.
   
Loading...