Wabunge wa CCM wakataa Kuunga Mkono hoja ya Kujadili Mgomo wa Madaktari

  • Baada ya kipindi cha maswali na majibu kwisha,Speaker aka step down na naibu spika akachukua nafasi.
  • Kutokana na kanuni ya 47 ya bunge,ulikua wakati wasaa wa kuwasilisha mwongozo.
  • Wakajitokeza wabunge wawili kuomba mwongozo; 1.Ndungulile na 2.Mnyika-wote waliomba kujadili ishu ya madaktari kwani ni urgent.
  • Ndugai akakubaliana nao kwamba wametumia kanuni vizuri lakiniiiii hoja zao hazikuungwa mkono.
My take
Baada ya wabunge hao wawili kutoa hoja wabunge hawakuulizwa kama wanaunga mkono hoja.Ndugai ameizima hoja kiubabe.

Mkuu hoja kama hii huungwa mkono kwa wabune KUSIMAMA haraka mala baada ya mtoa hoja kumaliza kutoa hoja!Hilo halikufanyika,unadhani Ndugai angefanyaje pale?Upuuzi umefanywa na wabunge ambao kwa makusidi wamemsaliti Mnyika na Ndungulile kwa kugoma kusimama ili kuunga mkono hoja FULL STOP!
 
kimsingi wanao ua wanchi ni serikali na si madaktari, kitendo cha kuwaacha madaktari waendelee na mgomo na kushindwa kutatua matatizo yao kwa njia ya majadilliano ni dharau kwa wananchi tuliowapa dhamana ya nchi yetu.
 
Hakika tunasubiriwa sisi tu kuamua hatima ya nchi yetu..hakika naapa hawa(ccm) sio watanzania....hakika tusipoamua sisi wananchi nchi hii imekwisha....
 
Conflict of interest, Mgongano wa kimaslahi. Ukiongelea mgomo huu, unarudi kwenye uhalali wa posho ya 200,000x30+ = 6,000,000+. Kwa hiyo ukibanwa katika mazingira kama haya unafunika kombe mwaharamu apite.
 
....Mheshimiwa Ndugulile na Mnyika walitoa hoja ya dharura kujadili mgomo wa madaktari maana watanzania wanakufa, kwa maana kuwa waahirishe kazi nyingine za Bunge ili wajadili jambo hili la muhimu. Bahati mbaya hoja zao hazikuungwa mkono wa wabunge kwa kusimama.

Ndipo Naibu Spika Ndugai akasema ni kweli hoja zao zina nguvu na wamefuata kanuni ya 47 ya taratibu za Bunge, Kanuni hii inasema hivi;

KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA 2007

47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

(2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
(3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge
kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

(4) Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusu hoja hiyo itolewe kwa
muda usiozidi dakika tano na mjadala juu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataona unafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa.


Ila tatizo hazijaungwa mkono, kwa hiyo tunaendelea na kazi za kawaida.Ndipo wabunge wakachekelea kwa vicheko vya raha mustarehe utadhani ni jambo la kufurahia. Na nina shaka kuwa serikali inawachezea madaktari, nawaomba endeleeni kukaza uzi kama kawaida. Madam Spika anachelewesha kuruhusu tamko la serikali juu ya hili akiwa na uhakika kuwa madaktari watarudi kazini.

Naomba kazeni buti.


Hata wabunge wa CHADEMA nao wamechangia, mbona hawakusimama? Kwa wingi wao kama wangesimama lazima hoja ingejadiliwa.
 
Hii ni mechi kali sana.Tutajua nani mwenye Kombe.Ma dr Wakishinda tuu, Waalimu wanaanza kivyao.Baada ya hapo? wakulima wanakuja juu wanagoma kuuza mazao hadi bei ifike laki kwa gunia la mahindi...kulaladek
 
umenena vyema, tukubaliane hapo kuwa, wabunge wa CDM nao wamechemka kutomuunga mkono mwenzao.
Sijui kama tupo serious kuitoa madarakani CCM.wakati hali ikiwa tete nilitegemea CDM wawashe moto kwa style yao ili wananchi waamke zaidi lakini naona wamepoa kweli! Hakuna nafasi nyingine! Hatuwawezi kwa kura hawa!
 
Mnyika Mwenyewe anasema hivi:

"Asubuhi ya leo Naibu Spika Job Ndugai alitumia kanuni vibaya kuzuia hoja ya dharura bungeni kuhusu mgomo wa madaktari. Kimsingi, sikuwasilisha hoja ila niliomba muongozo wa Spika ili niweze kupatiwa nafasi ya kuwasilisha hoja ya dharura. Kwa kuwa hoja kama hiyo iliwasilishwa juzi na ikaungwa mkono lakini Spika akasema ameshakubaliana na serikali kuwa ingewasilisha kauli. Hata hivyo, jana hakukuwa na kauli ya serikali huku wananchi wakiendelea kupata madhara ya mgomo. Hivyo nikataka muongozo kwa kuwa Spika alitumia kanuni ya 49 (2) ambayo kimsingi inatoa mwanya kwa kauli ya serikali kuwasilishwa kwenye wakati atakaoona yeye kuwa na unafaa juu ya jambo linaihusu serikali na lisilozua mjadala. Nilitaka kanuni hiyo isitumike badala yake wabunge tutimize wajibu wa kuisimamia serikali kwa kutumia kanuni ya 47 kuhusu hoja ya dharura. Kwa kuwa ilikuwa muongozo hakukuwa na hitaji la kikanuni la wabunge wengine kuunga mkono lakini akaamua kuilinda serikali kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa. Lakini mwishoni ameahidi kuwa kauli ya serikali itatolewa kesho."

Naona yuko sawa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
CCM imekataliwa na Mungu. Mungu akikataa utawala, utawala huo hufanya maamuzi ambayo hata mtoto mdogo anajua si ya busara.
Kwa hili CCM wananithibitshia kwamba hawapo kwa ajili ya watu. Wapo kwa ajili yao!! Watanzania, ni lini tutauona ukweli huu?. Ni lini tutaisikia sauti hii inayotuambia waziwazi kwamba watawala wamesaliti malengo ya Uhuru wetu?????
 
The challenges that our country is now facing,require strong leadership, visionary policies and the spirit of cooperation from all of us that helped our parents and grand parents defeat colonialism!! unfortunately, all these essential requirements are neither provided by the ruling party nor the opposition parties. the populace has only one option at its disposal and that is to commit suicide!!
 
Nadhani haitakuwa vema, kwasababu watakufa sana watu wasio na hatia na wasio na uwezo, mimi na wewe twaweza kukomaa tukatibiwa hata Private Hosptals, na viongozi kama wabunge wao wanaweza kwenda kutibiwa nje ya nchi. Siungi mkono hoja kwasababu moja tuu kwamba inapelekea vifo kwa watu wasio na hatia. Note ninamchukia sana kikkwete kwa moyo wangu wote!!!

Then what.......?
 
CCM imekataliwa na Mungu. Mungu akikataa utawala, utawala huo hufanya maamuzi ambayo hata mtoto mdogo anajua si ya busara.
Kwa hili CCM wananithibitshia kwamba hawapo kwa ajili ya watu. Wapo kwa ajili yao!! Watanzania, ni lini tutauona ukweli huu?. Ni lini tutaisikia sauti hii inayotuambia waziwazi kwamba watawala wamesaliti malengo ya Uhuru wetu?????

Lakini wachungaji wako wanasema Kikwete ni chaguo la Mungu!
 
siombei mtu mabaya lkn hebu pata picha hao waliozima hoja kibabe akiugua gafla atatibiwa na wabunge au madaktari?
inakuwaje unaemdharau ndio awe mtu atakaeokoa maisha yako au ya ndugu zao?
ngoja aumwe spika au huyo bwana mkubwa afu tuone mziki utakuwaje.
 
kwa hali hii tutakufa tutaisha, hawaoni, hawasikii wala hawaambiliki sasa ni wakati watanzania tuitake serikali ilipe maisha ya ndugu zetu!
 
Watanzania msiwalaumu wabunge wa ccm! Mliwachagua ninyi wenyewe kwa kura zenu. Waacheni wafanye wanavyotaka! Hao ni wawakilishi wenu halali!!
 
Back
Top Bottom