Wabunge wa CCM wakataa Kuunga Mkono hoja ya Kujadili Mgomo wa Madaktari

Naibu spika ametoa kauli kuwa kesho serikali itatoa tamko vinginevyo litajadiliwa bungeni
 
Hapa mimi naona serikali ingewasikiliza madaktari ili kupata muafaka. Wanaoteseka ni watanzania ambao waliwachagua wabunge wanaofurahia posho bungeni. Jamani Serikali iwasikilize madaktari
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, bunge limetupilia mbali hoja ya dharura iliyotaka kujadiliwa kwa swala la mgomo wa madaktari unaoendelea nchini kama hoja ya dharura. Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi, naibu spika alizuia kujadiliwa kwa hoja hiyo kwa madai kwamba haijaungwa mkono na wabunge.

Mtazamo wangu: Ikiwa bunge halijaona kama vifo vinavyoendelea kutokea kama ni jambo la dharura, nadhani umefika wakati watuambie ikiwa:
1. Pale bungeni wanamwakilisha nani?
2. Je, wanataka hadi watu wangapi wafe, ndiyo walione kama ni jambo la dharura?
 
Na wewe funguka na uelewe!, kwenye hizo kanuni za kuduma wapi kanuni inasema lazima mwongozo/hoja iungwe mkono na wabunge?.......

we unakurupuka kulaumu wakati we mwenyewe hujui kitu.acha wanaofahamu kanuni waongee waujuze ulimwengu
 
Mgomo huwagusi wao na familia zao.Maisha ya siasa ya Tanzania ni ya kinafki na ubinafsi hakuna uwakilishi wakweli ngoja nimeze panado kutuliza maumizu.Maisha ya binadamu hayana spear once gone never come back nadhani hawajui hilo.
 
Hivi kumbe kama hoja haijaungwa mkono na wabunge, hata kama ni ya msingi, spika kwa nafasi yake hawezi kuiruhusu kujadiliwa.
Au jamaa wanaweza kususa kuijadili! Oooh, my poor Tanzania, ni nani atakayetusitiri na aibu hii?!!
 
Hizi ni hoja za kujitafutia umaarufu tu. Watu tumeisha anza kumfahamu Mnyika ni mtu wa show off zaidi kuliko utekelezaji


Sasa katika hili ambapo Kanuni ziko wzi ulitaka utekelezaji gani zaidi, utekelezaji wa mbunge si ni kutaka ufafanuzi toka serikalini au kuna lingine tena?
 
Walio toa hoja ni mbuge wa ccm na chadema, kwa nini kina mdee na wengine hawakuunga mkono hoja? Kwani lazima iungwe na ccm tu ndio ijadiliwe?
Macinkus
 
Hivi kweli hili nalo linaonekana ni la kiitikadi. Wabunge liangalieni vizuri watu wanaumia. Ua kwa vile nie mna matibabu ya uhakika?
 
Kwakuwa serikali inatuchonganisha na madaktari wakati yenyewe wanajipendelea. NASHAURI: watanzania wote tuingie barabarani TUANDAMANE na tukaonyeshe hasira zetu, Waziri wa afya anafanya nini badala ya kuwajibika
 
Walio toa hoja ni mbuge wa ccm na chadema, kwa nini kina mdee na wengine hawakuunga mkono hoja? Kwani lazima iungwe na ccm tu ndio ijadiliwe?
Macinkus

Hata kama wangeunga mko zisingetosha kwani wazalendo ni wachache
 
Walio toa hoja ni mbuge wa ccm na chadema, kwa nini kina mdee na wengine hawakuunga mkono hoja? Kwani lazima iungwe na ccm tu ndio ijadiliwe?
Macinkus

Kwa staili ya kusema "NDIYOOOOOOOO!!!" au "HAPANAAAAAAA!!!!!!!" unatarajia sauti ya Mdee na wenzake ingesikikaje ilhal wagonga meza na wataalam wa mipasho (Ndugai na Makinda inclusive) wako pale kufuata uelekeo wa upepo kama ilivyo bendera pasi na maamuzi binafsi wala kufikiri.
 
Pinda kisha towa tamko, au hamjamsikia? waliokuwa hawajarudi kazini hawapo kazini. Na wanaotaka kuunga mkono na wao waunge wawe jobless. Serikali msiwachie msimamo wenu kwa hili, wafundisheni hawa madaktari uchwara ni nini nidhamu.

Unalipwa kiasi gani kwa kila post unayobandika hapa JF!
 
Hawa Wabunge wa CCM walisha kaa ktk kikao chao na kuambiwa ni marufuku kusupport hiyo hiyo ya kujadili mgomo wa madaktari... ndiyo maana hoja haiungwi mkono. Bunge ga ni ambalo linakaa wiki bila kujadili watu wanakufa kila siku. Hizi kanuni za Bunge ni lazima ziangaliwe upya. Kwa kweli wabunge mmetia kinyaa.
 
NI KWELI Naona Nape Nauye anachekelea walalahoi kufa mahospitalini,AFU YE JUZI TU KAUGUA TUMBO AMEKULA MAHINDI MABICHI HAPA PASIASI MWANZA AKAGOMEWA KUPELEKWA INDIA.aliponea kona ya bwiru medical research hivyo angewasihi wabunge kujadili hoja.Manesi jiungeni tuwakomoe mpaka mpewe masurufu mazito
 
Back
Top Bottom