Watanzania wenzangu hivi wooote tunaukumbuka huu wimbo????
Tanzania, Tanzania, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE (!!!!?????????)
nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana (!!!!!!?????)
NILALAPO NAKUOTA WEWE, NIAMKAPO NI HERI MAMA WE (!!!!!!!!??????)
Kweli uzalendo ni kitu adimu sasa katika hii mihimili miwili ya dola- serikali na bunge!. Baada ya kujihakikishia posho nono za kukaa 'bure' bungeni a.k.a kwa kuchumia matumbo yao na si kuwapigania wapigakura wao, hawana zaidi cha kufanya!! wagonjwa kufa mahospitalini si issue kwao, after all wana uhakika wa kupelekwa India hata wanapopatwa na ukurutu! ndio wabunge tuliowachagua wenyewe kwa hiari yetu wenyewe ama kwa kuvutiwa na kanga na t-shirt ama pilau walizotufadhili wakati wa kampeni. Wa kujilaumu ni sisi wenyewe na wala si wao!.
My take
- Baada ya kipindi cha maswali na majibu kwisha,Speaker aka step down na naibu spika akachukua nafasi.
- Kutokana na kanuni ya 47 ya bunge,ulikua wakati wasaa wa kuwasilisha mwongozo.
- Wakajitokeza wabunge wawili kuomba mwongozo; 1.Ndungulile na 2.Mnyika-wote waliomba kujadili ishu ya madaktari kwani ni urgent.
- Ndugai akakubaliana nao kwamba wametumia kanuni vizuri lakiniiiii hoja zao hazikuungwa mkono.
Baada ya wabunge hao wawili kutoa hoja wabunge hawakuulizwa kama wanaunga mkono hoja.Ndugai ameizima hoja kiubabe.
....Mheshimiwa Ndugulile na Mnyika walitoa hoja ya dharura kujadili mgomo wa madaktari maana watanzania wanakufa, kwa maana kuwa waahirishe kazi nyingine za Bunge ili wajadili jambo hili la muhimu. Bahati mbaya hoja zao hazikuungwa mkono wa wabunge kwa kusimama.
Ndipo Naibu Spika Ndugai akasema ni kweli hoja zao zina nguvu na wamefuata kanuni ya 47 ya taratibu za Bunge, ila tatizo hazijaungwa mkono, kwa hiyo tunaendelea na kazi za kawaida.
Ndipo wabunge wakachekelea kwa vicheko vya raha mustarehe utadhani ni jambo la kufurahia. Na nina shaka kuwa serikali inawachezea madaktari, nawaomba endeleeni kukaza uzi kama kawaida. Madam Spika anachelewesha kuruhusu tamko la serikali juu ya hili akiwa na uhakika kuwa madaktari watarudi kazini.
Naomba kazeni buti.
....Mheshimiwa Ndugulile na Mnyika walitoa hoja ya dharura kujadili mgomo wa madaktari maana watanzania wanakufa, kwa maana kuwa waahirishe kazi nyingine za Bunge ili wajadili jambo hili la muhimu. Bahati mbaya hoja zao hazikuungwa mkono wa wabunge kwa kusimama.
Ndipo Naibu Spika Ndugai akasema ni kweli hoja zao zina nguvu na wamefuata kanuni ya 47 ya taratibu za Bunge, Kanuni hii inasema hivi;
KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA 2007
47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.
(2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
(3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge
kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.
(4) Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusu hoja hiyo itolewe kwa
muda usiozidi dakika tano na mjadala juu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataona unafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa.
Ila tatizo hazijaungwa mkono, kwa hiyo tunaendelea na kazi za kawaida.Ndipo wabunge wakachekelea kwa vicheko vya raha mustarehe utadhani ni jambo la kufurahia. Na nina shaka kuwa serikali inawachezea madaktari, nawaomba endeleeni kukaza uzi kama kawaida. Madam Spika anachelewesha kuruhusu tamko la serikali juu ya hili akiwa na uhakika kuwa madaktari watarudi kazini.
Naomba kazeni buti.
Ukisikia nchi yenye laana usisahau tz tunahitaji ukombozi,kiroho,kimwili na kiakili na kadhalika,kila m2 kwa dini yake tufunge na kuomba,
Andika lugha sanifu ueleweke, vinginevyo ulichoandika ni uozo!