Wabunge wa CCM wakataa Kuunga Mkono hoja ya Kujadili Mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM wakataa Kuunga Mkono hoja ya Kujadili Mgomo wa Madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Feb 2, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Mheshimiwa Ndugulile na Mnyika walitoa hoja ya dharura kujadili mgomo wa madaktari maana watanzania wanakufa, kwa maana kuwa waahirishe kazi nyingine za Bunge ili wajadili jambo hili la muhimu. Bahati mbaya hoja zao hazikuungwa mkono wa wabunge kwa kusimama.

  Ndipo Naibu Spika Ndugai akasema ni kweli hoja zao zina nguvu na wamefuata kanuni ya 47 ya taratibu za Bunge, Kanuni hii inasema hivi;

  KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA 2007

  47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

  (2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
  (3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge
  kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

  (4) Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusu hoja hiyo itolewe kwa
  muda usiozidi dakika tano na mjadala juu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataona unafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa.


  Ila tatizo hazijaungwa mkono, kwa hiyo tunaendelea na kazi za kawaida.Ndipo wabunge wakachekelea kwa vicheko vya raha mustarehe utadhani ni jambo la kufurahia. Na nina shaka kuwa serikali inawachezea madaktari, nawaomba endeleeni kukaza uzi kama kawaida. Madam Spika anachelewesha kuruhusu tamko la serikali juu ya hili akiwa na uhakika kuwa madaktari watarudi kazini.

  Naomba kazeni buti.

   
 2. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  We have to do something now let go out kesho
   
 3. t

  taranda Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani bunge linaendelea na huyu naibu spika kaombwa mwongozo kuhusu mgomo wa madaktari kapotezea. Alieomba ni daktari mbunge wa kigamboni na mbunge wa ubungo. Jamani..mbona bunge linakwepa hii ishu?
   
 4. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hao hawana uchungu tumbo likivuruga wanakimbilia India
   
 5. t

  taranda Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wanavuta posho ya nguvu ndio maana wamechuna. Madaktari kazeni buti
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hujaeleza kwa uwazi kapotezeaje? Lete kitu kamili ili watu wakuelewe maana tunaoangalia TV tuko wengi na maelezo ya Naibu Speaker yameeleweka?
   
 7. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  mgomo wa madaktari kwake sio issue, issue kwake ni posho kwa hiyo usione cha ajabu kukaushia
   
 8. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyotarajiwa mh Ndugai amekataa kuruhu wabunge kujadili mgomo wa madaktari kwa hati ya dharura.Baada ya maswali na majibu wabunge Ndugulile na Mnyika waliomba mwongozo lakini naibu spika kagoma eti wabunge wengine hawajaunga mkono, halafu wabunge ccm wanashangalia wakati watanzania wenzetu wanaendelea kuumia na kufa. Is this Tanzania we want?
   
 9. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Andika lugha sanifu ueleweke, vinginevyo ulichoandika ni uozo!
   
 10. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya wabunge wa ccm ambao ndio wengi wapo bungeni kwa maslai ya chama na sio wananchi
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,390
  Trophy Points: 280
  Ni wakati wa wauguzi kuunga mkono mgomo
   
 12. t

  taranda Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magamba utawajua kwa maneno yao
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  kwenye posho yuko radhi hata kuomba air time kwenye vituo vya televisions.
   
 14. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nimeona tukio hili nimeudhunika sana.La kuomba usipate mgonjwa au kuuguliwa sasa.
   
 15. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  • Baada ya kipindi cha maswali na majibu kwisha,Speaker aka step down na naibu spika akachukua nafasi.
  • Kutokana na kanuni ya 47 ya bunge,ulikua wakati wasaa wa kuwasilisha mwongozo.
  • Wakajitokeza wabunge wawili kuomba mwongozo; 1.Ndungulile na 2.Mnyika-wote waliomba kujadili ishu ya madaktari kwani ni urgent.
  • Ndugai akakubaliana nao kwamba wametumia kanuni vizuri lakiniiiii hoja zao hazikuungwa mkono.
  My take
  Baada ya wabunge hao wawili kutoa hoja wabunge hawakuulizwa kama wanaunga mkono hoja.Ndugai ameizima hoja kiubabe.
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  kama aliwahonga wapiga kura wake,wakampigia kura ina maana alinunua ubunge kwa hiyo sasa mbunge wa aina hiyo ambao ni wengi wanahangaika kurudisha walicho honga,hawana habari na shida za wapiga kura wao.
   
 17. k

  kabuga Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anae jibu majibu yenye kinyaa ni nape hakika nimegundua
   
 18. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,451
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenzangu hivi wooote tunaukumbuka huu wimbo????

  Tanzania, Tanzania, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE (!!!!?????????)
  nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana (!!!!!!?????)
  NILALAPO NAKUOTA WEWE, NIAMKAPO NI HERI MAMA WE (!!!!!!!!??????)
   
 19. T

  Tanganyika2 Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The system failed to cater for Doctors,
  The Government failed to listen and talk to Doctors,
  The Parliament has failed to even discuss the issue........
  THERE WILL NO BE SOLUTION ON THE SAGA AND ITS SISI TUNAOKUFA!!
  LETS BE SERIUS........
  KESHO.
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  We ni kibaka wa maghambas au Ndugai,naona upo kazini kweli??????????

   
Loading...