Wabunge wa CCM waitwa na kuonywa kuhusu saini 70

Yaani UDP (Bw. Mapesa) na TLP (Mzee wa Kiraracha) hawajamwaga wino pamoja na mbwembwe zao za jana? Au walikuwa wanajikomba?
 
Walioko dodoma ni wangapi.
Kwanini wasingeitwa wote warudi kwenye jambo hili ili zibaki saini 22 pekee.
OTIS

ndipo hapo suala hili litaonekana ni la chadema peke yao na ccm watajitoa. Ni heri kusaka saini za wanaccm na kulifanya suala hili ni la bunge kuliko chama fulani.
 
Tundu kesi yake imehairishwa hadi tar 24 au 27 (sina hakika ni ipi kati ya hizo 2) kwa ajili ya hukumu.
Huo ugonjwa wa shibuda unatia shaka
OTIS


hukumu ya tundu lissu ni tarehe 27 saa tatu kamili....
 
Kwa mujibu wa Zitto kabwe hadi sasa saini 30 zimepatikana kutoka CDM,CUF na NCCR.
Wabunge wa CCM waliodhamiria wameitwa na Mnadhimu wa serikali bwana Lukuvi

Source: Zitto on twitter

Kwani nini hata Mheshimiwa Deo wa Ludewa hajasaini au alikuwa anawafurahisha wananchi. Hawa Wabunge wanawakilisha wananchi au wanamwakilisha Lukuvi?
 
ndipo hapo suala hili litaonekana ni la chadema peke yao na ccm watajitoa. Ni heri kusaka saini za wanaccm na kulifanya suala hili ni la bunge kuliko chama fulani.

lukuvi kajifanya mjanja kuwaita wabunge wa ccm na kuwakaripia sana..hasa wale walioonyesha nia ya kusaini...
 
Wabunge wenye kesi mahakamani kwa upande wa CHADEMA kwa sasa wote wanasubiri hukumu zao.

Kama kuna mbunge ambaye ni mgonjwa anaweza kupelekewa huko aliko na akasaini.

Bwana Mkosamali wa NCCR ndiye Mbunge pekee wa Upinzani ambaye leo anasomewa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo yake.


Kwenye red hapo..........Mkosamali kanasa tunduni atatoka salama kweli?
 
Kuna swala moja la msingi tujiulize wana JF.
Huu msimamo wa saini 70 wa zitto ni msimamo wa CDM pia?
Kama ni msimamo wa chama kwanini haukutolewa na Mwenyekiti wake ambae ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani.
Inawezekana kuna mambo hatujui huku nje.
OTIS
 
Back
Top Bottom