Wabunge wa CCM waendelea kuyatendea haki na wajibu Majimbo yao

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,099
630
Hakika wabunge wa CCM wameendelea kujipambanua vyema kwa wapiga kura wao kwa kutimiza kwa
vitendo ahadi walizoweka na pia kushirikiana na wapiga kura wao katika kuleta maendeleo katika majimbo
yao.
112.jpg

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo imejengwa na Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya shilingi milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo, Mbunge huyo pia ameahidi kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta ili wanafunzi wajengewe mzingira mazuri zaidi ya kujisomea lakini pia ameahidi kushughulikia tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru kwenda kidato cha ano na sita lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa.


Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizindua mradi wa maji kwa kunywa maji ya mto kwa majani ya mgomba maji ambayo wapiga kura wake wa kijiji cha Madindo Mlangali wamekuwa wakiyatumia mbunge huyo mbali ya kuzindua pia alitoa msaada wa matenki makubwa ya maji mawili na vifaa mbali mbali juzi
Filikunjombe2.JPG

k4.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
 
Baadhi ya Wabunge wanafanya kazi nzuri inayoonekana lakini wengine ni Mizigo isiyobebeka.
 
Ahadi ni deni. Hatuendi bungeni kulumbana bali kupanga mikakati ya maendeleo kwa nchi nzima sio kwa wabunge wa ccm tu!
 
Jimbo lako likiwa na Mbunge wa CCM....una uhakika wa maendeleo


Hahahahahahahahahahahahahahahahahahahah,du hahahahahahahahahah uwiiiiiiiiiiiiiiiiiii hahahahahahahah,du nimecheka hadi basi,hahahahahahah jamani mwenye zile picha za ziara za kinana na nape walipokwama jamani embu mrushie hizo clip tuone ilikuwa jimbo gani liko chini ya chama gani,maana haya maisha bora kwa kila mtanzania yanafanyika kweli kweli
 
Mbunge wangu wa Ubungo inampaswa aombe ushauri kwa wabunge wa CCM jinsi ya kuhudumia wananchi badala ya kuongoza maandamano yasiyo na TIJA
 
Ridhiwani anakata utepe wa kuzindua maktaba mpya!!! Mbona hilo jengo limeshachoka hata kabla ya kuanza? Angalia rangi imeanza kubanduka!!!

Yaani CCM kwa kuchapia ni kiboko. Nyumba yenyewe ni ya zamani, kwa haraka haraka wamepiga rangi ya bluu na bila shaka walishindwa hata kumlipa fundi rangi bora, matokeo yake ONA! Kudanganya wananchi tu. Na naamini hata hilo daraja la Kilombero itakuwa geresha tu! Mbona hakuna mwakilishi wa mkandarasi atakayejenga daraja hilo? Ni nani amejenga jiwe la msingi? Serikali? Magufuli? ACHENI KULAGHAI WANANCHI KWEUPE NAMNA HII!
 
Mkuu MSALANI ninazo picha za MAANDAMANO tuu za Mbunge wa Arusha!!


wewe arusha mjini sasa kuna taa za barabarani na barabara nyingi lami mpaka njiro kuna ring road...kuna mahali pale shoprite ilkuwa wakati wa mbunge wa ccm ikifika jioni jam inaanzua kisongo sasa mhhhh shwari heko mbunge ar mjini
 
kweli wapo wabunge kazi zao siyo za kubezwa wanafanya vitu vya kuonekana kabisa japo wapo wanafanya kwa mnato sana nao wanapaswa kuongeza bidii.
 
wewe arusha mjini sasa kuna taa za barabarani na barabara nyingi lami mpaka njiro kuna ring road...kuna mahali pale shoprite ilkuwa wakati wa mbunge wa ccm ikifika jioni jam inaanzua kisongo sasa mhhhh shwari heko mbunge ar mjini

Hata Dodoma kuna taa za barabarani!!!.
 
Back
Top Bottom