Wabunge wa CCM,someni alama za nyakati na muache kujiaibisha.

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,115
2,000
Inashangaza pale mnapoanza kwa kuisifia serikali ya ccm,mnasema iko imara na inatekeleza vizuri ilani ya ccm.mnawazodoa wabunge wa upinzani kwanza alafu mnaanza kuchangia kwa kulalamika yale yale ambayo mnaambiwa na wabunge wa upinzani.jee hii ni halali?
Nimemuona mh kamani sasa hivi kupitia TBC kwamba anatetea mkurugenzi wa halmashauri mbeya kwenda kumpokea katibu mkuu wa ccm kwa kutumia gari la TAMISEMI.

Anatolea mfano wa nchi kama uingereza kwamba chama cha siasa kinapochukua madaraka huwabadilisha watendaji wa kidiplomasia kutoka nchi mbalimbali akiwa na maana ya kuwaunganisha na uhusiano wao na chama.

Anashindwa kuelewa kwamba wawakilishi wa kidiplomasia kama mabalozi,huwa ni watendaji wa serikali moja kwa moja na hakuna namna unaweza kuwaacha waendelee kuwakilisha nchi wakati chama kinachotawala kinakuwa kimebadilika hivyo kuwalamizisha wao kurudishwa nyumbani na chama kinachounda serikali kutuma wawakilishi wao wapya wenye ilani na sera ya chama na serikali yao.

Sasa hapa TAMISEMI ni mtendaji wa halmashauri ambayo ina jukumu la kumsaidia mwananchi kupata huduma bora za kijamii kwa kusimamia miradi mbalimbali katika halmashauri za wilaya nchini. Sasa mbunge msomi kama Dokta mlengeya hastahili kumtetea mkurugenzi wa halmashauri ambaye anatumia mali za walipakodi ya serikali na kwenda kufanya mambo ya kisiasa kinyume na sheria ya katiba ya nchi.

Hawa ni wasomi ambao walitakiwa kuisaidia ccm kuikwamua kwenye tope la lawama lukuki zinazotolewa na wananchi kila kona ya nchi.badala ya kuendelea kuisadikisha ccm kwamba iko sahihi (kwa maslahi yao binafsi).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom