Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Nimekuwa nikifuatilia majadiliano ya Bunge la Bajeti tangu kuanza kwake. Kwasasa, bajeti kuu ya Serikali ndiyo inayojadiliwa. Wabunge wanatumia nafasi, maarifa, uwezo, na muda wao kujadili Bajeti iliyopo mbele yao.
Lakini, kila anaposimama Mbunge wa CCM, hujadili mambo mawili: Bajeti na Tundu Lissu. Hata wale Wabunge wazoefu na 'maarufu' kama Kangi Lugola, Martha Mlata na kadhalika wamejikuta katika mkumbo huo.
Imekuwa fasheni sasa Bungeni kwa kila Mbunge wa CCM kuonyesha umahiri wake wa kumjibu Lissu kwa kumtaja waziwazi au kumzungumzia kwa mafumbo. Najiuliza, kwanini nguvu kubwa itumike kumjadili Lissu hata wakati wa kujadili Bajeti kuu ya Serikali?
Kama Lissu amechafuka kiasi kinachosemwa na Wabunge wa CCM, CCM imejipangaje au inajipangaje kumng'oa Lissu kule Singida Mashariki mwaka 2020? Au ndiyo ameandaliwa Martha Mlata kumpoteza Lissu kule Singida Mashariki?
Kwa msemo maarufu wa Mnyika : tukubaliane kutokukubaliana kwa baadhi ya mambo. Kadiri Lissu 'anavyojibiwa', ndivyo atakavyoendelea 'kujibu' na kuufanya mjadala usio na msingi kumhusu kuendelea. Hakuna sababu yoyote kuendelea kuzodoana.
Huyu hapa Mbunge Kangi Lugola (Mwibara):
Huyu hapa ni Mbunge Martha Mlata (Viti Maalum) akijadili naye: