Wabunge wa CCM, ninani aliwapa "mandate" ya kuisemea serikali bungeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM, ninani aliwapa "mandate" ya kuisemea serikali bungeni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gwalihenzi, Jun 20, 2012.

 1. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mimi binafsi nasikitishwa sana na tabia ya wabunge wa CCM wanaposimama bungeni kujibu hoja za serikali badala ya kuijadili bajeti. Kila mmoja wao anapopewa nafasi ya kujadili bajeti anatumia robo tatu ya muda aliopewa kujibu hoja za wabunge wa upinzani zilizoelekezwa serikalini. Mwishoni anatumia robo ya muda kuorodhesha matatizo ya jimboni kwake!
  Ninani aliwapa madaraka ya kujibu hoja zilizoelekezwa serikalini? Mwigulu anafikia hata kuwatukana wabunge na kufoka (jana 19/6/2012, bunge la jioni, alisimama na kumshambulia Mghwai, ati yeye Mwigulu alimwelimisha kaka yake Mghwai na ataendelea kumwelimisha Mghwai mpaka lini kuhusu ubora wa bajeti inayojadiliwa!). Leo Mwigulu amepambana na Zito kabwe TBC1 akashindwa kabisa kutetea hoja ya ubora wa bajeti akaishia kutoa mapovu tu!
  Nawashauri wabunge wa CCM, waache kutoa majibu ya serikali, sio kazi yao, kwani wapo mawaziri. Wajadili na kuichambua bajeti ya serikali.
   
Loading...