Wabunge wa CCM msituumize wananchi

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,598
2,000
Wabunge wengi wa CCM wamekuwa na mawazo ya kuwaumiza wananchi. Kama mbunge anasema hadi kuku alipiwe kodi kwakweli hii sasa imezidi. Msipende kupigiwa makofi bali angalieni nini kitamrahisishia mwananchi hali ya Maisha. Mmekuwa wakwanza kutukandamiza sijui mtatuambia nn wakati wa uchaguzi. Mnapitisha vitu vya hovyo sana.
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,299
2,000
Wabunge wa CCM wengi ni vilaza na bendera fuata upepo

Budget nyingi hupitishwa hata kama zinaangamiza nchi

Taifa lolote lenye GDP ndogo watu wake wengi ni masikini and hence low purchasing power.

VAT Ni kodi inayolipwa na consumer ambayo ndio hawa masikini

Sasa, ili nchi iendelee, inatakiwa kukuza Sekta za uzalishaji zinazogusa watu wengi (Agriculture and Tourism).

Bila Shaka Tanzania ni nchi masikini Kusini mwa Janga la Sahara, hata Kenya wana GDP kubwa kuliko Tanzania. Hivyo basi, tuwe wawazi kabisa, Tanzania bado inahitaji misaada.

Nini kimesababisha Tukose Msaada?

Ni Nani anawatesa Watanzania?

Hii kelele ya makinia tumeibiwa ni usanii mtupu! Madini hayana mchango kwenye uchumi mpana wa Watanzania.

Kwanza wao ndio walisaini hii mikataba...

Pili Makampuni ya madini wananunua vyakula na Nyama nje ya nchi...

---Sioni Juhudi za Serikali katika kuinua uchumi? Juhudi zipi sasa? Kilimo kimeachwa kife na wakulima wateseke

hakuna miundo mbinu ya Umwagiliaji

Viwanda vitakufa bila Kilimo imara

Nimekosoa kwa hoja....
 
Uwingi wetu umeleta Shida kwa nchi hatufikirii tena
 
Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,889
2,000
Mkuu Yeye akikaa pale mpaka kikao kinaisha anaondoka na pesa ndefu ambayo ukipewa wewe mwenzangu na Mimi unaweza kuifanya bajeti ya familia yako ya Mwaka mzima... Kwahiyo yeye haoni kama kweli maisha Ni Magumu...

CCM Oyeeeeeeee

ACTwazalendo Oyeeeeeee.

CUF-LIPUMBA Oyeeeeee
 
kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,598
2,000
Hali ya Maisha kuwa ngumu ni kutokana na michango hasi ya wabunge wetu CCM juu ya wananchi
 
BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,059
2,000
Wabunge wa ccm tunataka kodi ya Kichwa ili tupate akili vizuri
 
kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,598
2,000
Leo makinikia imelenga kabisa jinsi gani wabunge wa CCM wamehusika wote kutuibia
 
kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
4,064
2,000
[HASHTAG]#RipotiYaKwanza[/HASHTAG]

Lissu: Tusihangaike na udongo, tuhangaike na mikataba na sheria mbovu za madini zilizotufikisha hapa. Tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia.

CCM: Lissu analinda wezi. Mikataba na sheria za madini hazina shida. Shida ipo kwenye udongo wenye makinikia. Tumeibiwa sana kwenye udongo. Hatukubali.

[HASHTAG]#RipotiYaPili[/HASHTAG]

JPM: Tumelogwa na nani? Watanzania tumeibiwa sana. Naagiza mikataba yote na sheria zote za madini zipitiwe upya.

CCM: Rais wetu mzalendo. Amefanya kazi kubwa sana. Tumuombee.!!

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Lugha ileile aliyoongea Lissu akaambiwa amehongwa, ndiyo aliyoongea JPM leo akaitwa mzalendo. Akili za CCM kama kifurushi cha jaza ujazwe .!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom