Uchaguzi 2020 Wabunge wa CCM mpya ni mkakati maalum wa kubadili katiba, Paul Makonda na Alexander Mnyeti ni kishindo kikuu

Sipendi wala situkani. Kuna wakati niliandika na sasa narudia. Wale wenye kithembe si kizembe kilaza wanathema kilatha! Yawezekana babu alikuwa na kithembe. Wewe ni kilaza kwelikweli.
Corona haitosababisha kuahirisha uchaguzi. Nani anataka kuendelea kukaa katika nafasi hizi. Kazi ya urais ni ngumu sana. Mungu, why me?
Fomu ya kuongoza vyombo vya dola ni moja. Aliyetaka ya pili kafukuzwa chamani. Kuna mambo ya kukamilisha yeye tu. Hakuna mwingine anayeweza. Muhula wa pili mambo ya kukamilisha yatakuwa mengi na magumu zaidi!
We unadhani swala la maamuzi ya fomu yangekuwa yake peke yake ungeona uongozi wote wa zamani na leo kwenye jukwaa moja wakicheka mpaka kukenua meno yote yaliyobaki.

Hayo maneno mengine na Magu as Magu without a script expect anything lakini aindoi dhamira yake.
 
Tetesi

Members, wasibezwe hili kundi la CCM mpya na waongeaji watapita kwa kishindo kikuu kwa lengo maalum bungeni kubadili katiba na Kuongeza muda wa Rais kutawala

Kauli ya Rais mstaafu Mwinyi sio mara moja au kwa bahati mbaya anapenyeza kauli ya kubadili Katiba kuhusu ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Watu wafuatao ndio watakaoendesha bunge na kuwa waongeaji wakuu bungeni. Hakuna atakaye nyanyua mdomo wake kuwapinga watu wafuatao bungeni:

Paul Makonda
Cyprian Musiba
Alexander Mnyeti
Mchungaji Gwajima
Tulia Ackson

Waliotajwa wataingia bungeni kimkakati na siyo kwa bahati mbaya. Hoja zao ndio zitakuwa za mwisho kwa maamuzi ya Taifa.

Paul Makonda, Alexander Mnyeti, Mchungaji Gwajima na Cyprian Musiba msiwachukulie kirahisi na kuwadharau, Hao watu ni wajenga hoja wazuri tena za kulazimisha utake usitake lazima uwaunge mkono ili ubaki salama kwenye CCM mpya.

Hakuna cha mpasuko wala ufa CCM. Sauti ni moja tu yenye nguvu na kuheshimiwa. Hakuna mwenye uwezo wa kumpinga Mwenyekiti wa chama wala kunyanyua mdomo kuhoji maamuzi ya Mwenyekiti.

Mwenyekiti amepitishwa kwa asilimia 100%. Hii inampa nguvu ya kuaminiwa na yeyote atakaye ongea kuhusu kura za maoni kwa upande hasi hasa za ubunge basi atafute Maisha mengine nje ya bunge na CCM mpya.

CCM ni moja na yenye nguvu zaidi, Wapinzani tafuteni mbinu mpya, CCM imempa mamlaka ya asilimia 100% Mwenyekiti kwa kupiga kura za ndio Dodoma, Sauti yake ni sauti kuu. Hakuna mwanachama atakaye tenda nje ya Maamuzi ya Chama

Wapinzani msisubiri eti CCM kutakuwa na mpasuko ili mpate hoja za ubunge, Bunge linakwenda kuwa la kimkakati kupitisha hoja maalum ya ukomo wa Rais madarakani.
yaa, it might be
 
Inaweza kuwa hivyo au isiwe. Inawezekana kina Makonda na Gwajima wanataka uwaziri, mpaka uwaziri Mkuu

Paul Makonda huwa anaamini siku moja atakuwa Rais wa nchi hii.
Na hapo ndipo akili za kitanganyika zitajulikana zilivyo
 
Cha msingi mi naona wananchi tuamke tupeleke wabunge wa upinzani wakutosha bungeni, vinginevyo tutakuja kujuta huko mbele. Mungu epusha haya yasitokee
[/QUOTE Wapinzani wapi, hao 2015 tuliowapa kura wakaunga juhudi, bora kuchagua ccm tu.
 
Hatuwezi kuruhusu watu wachache wachezee katiba yetu!! Haiwezekani.
 
Maskin nchi yangu GININGI....
giphy.gif
 
Magufuli hataongeza hata dakika moja. Akithubutu lazima watanzania tukatae.
Ata akifanya hivyo hamna cha kufanya maana anayo kinga kubwa na sasa wameongezeka spika,Jaji mkuu na Waziri Mkuu. Pole yenu.
 
Ndipo pale watakaposhangazwa na nguvu ya umma mithili ya ile Arab Spring. Wacha wajiaminishe hivyo halafu watashangaa yajayo, hakuna jela au risasi zitatosha kuuzima moto utakaowaka.
 
Back
Top Bottom