Hakuna aliyetumwa.... so that's nonsense na hao wote hasa waliozaliwa 1982 watachinjiliwa mbali !!Tetesi
Members, wasibezwe hili kundi la CCM mpya na waongeaji watapita kwa kishindo kikuu kwa lengo maalum bungeni kubadili katiba na Kuongeza muda wa Rais kutawala
Kauli ya Rais mstaafu Mwinyi sio mara moja au kwa bahati mbaya anapenyeza kauli ya kubadili Katiba kuhusu ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Watu wafuatao ndio watakaoendesha bunge na kuwa waongeaji wakuu bungeni. Hakuna atakaye nyanyua mdomo wake kuwapinga watu wafuatao bungeni:
Paul Makonda
Cyprian Musiba
Alexander Mnyeti
Mchungaji Gwajima
Tulia Ackson
Waliotajwa wataingia bungeni kimkakati na siyo kwa bahati mbaya. Hoja zao ndio zitakuwa za mwisho kwa maamuzi ya Taifa.
Paul Makonda, Alexander Mnyeti, Mchungaji Gwajima na Cyprian Musiba msiwachukulie kirahisi na kuwadharau, Hao watu ni wajenga hoja wazuri tena za kulazimisha utake usitake lazima uwaunge mkono ili ubaki salama kwenye CCM mpya.
Hakuna cha mpasuko wala ufa CCM. Sauti ni moja tu yenye nguvu na kuheshimiwa. Hakuna mwenye uwezo wa kumpinga Mwenyekiti wa chama wala kunyanyua mdomo kuhoji maamuzi ya Mwenyekiti.
Mwenyekiti amepitishwa kwa asilimia 100%. Hii inampa nguvu ya kuaminiwa na yeyote atakaye ongea kuhusu kura za maoni kwa upande hasi hasa za ubunge basi atafute Maisha mengine nje ya bunge na CCM mpya.
CCM ni moja na yenye nguvu zaidi, Wapinzani tafuteni mbinu mpya, CCM imempa mamlaka ya asilimia 100% Mwenyekiti kwa kupiga kura za ndio Dodoma, Sauti yake ni sauti kuu. Hakuna mwanachama atakaye tenda nje ya Maamuzi ya Chama
Wapinzani msisubiri eti CCM kutakuwa na mpasuko ili mpate hoja za ubunge, Bunge linakwenda kuwa la kimkakati kupitisha hoja maalum ya ukomo wa Rais madarakani.