Uchaguzi 2020 Wabunge wa CCM mpya ni mkakati maalum wa kubadili katiba, Paul Makonda na Alexander Mnyeti ni kishindo kikuu

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
164
1,000
Tetesi

Members, wasibezwe hili kundi la CCM mpya na waongeaji watapita kwa kishindo kikuu kwa lengo maalum bungeni kubadili katiba na Kuongeza muda wa Rais kutawala

Kauli ya Rais mstaafu Mwinyi sio mara moja au kwa bahati mbaya anapenyeza kauli ya kubadili Katiba kuhusu ukomo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Watu wafuatao ndio watakaoendesha bunge na kuwa waongeaji wakuu bungeni. Hakuna atakaye nyanyua mdomo wake kuwapinga watu wafuatao bungeni:

Paul Makonda
Cyprian Musiba
Alexander Mnyeti
Mchungaji Gwajima
Tulia Ackson

Waliotajwa wataingia bungeni kimkakati na siyo kwa bahati mbaya. Hoja zao ndio zitakuwa za mwisho kwa maamuzi ya Taifa.

Paul Makonda, Alexander Mnyeti, Mchungaji Gwajima na Cyprian Musiba msiwachukulie kirahisi na kuwadharau, Hao watu ni wajenga hoja wazuri tena za kulazimisha utake usitake lazima uwaunge mkono ili ubaki salama kwenye CCM mpya.

Hakuna cha mpasuko wala ufa CCM. Sauti ni moja tu yenye nguvu na kuheshimiwa. Hakuna mwenye uwezo wa kumpinga Mwenyekiti wa chama wala kunyanyua mdomo kuhoji maamuzi ya Mwenyekiti.

Mwenyekiti amepitishwa kwa asilimia 100%. Hii inampa nguvu ya kuaminiwa na yeyote atakaye ongea kuhusu kura za maoni kwa upande hasi hasa za ubunge basi atafute Maisha mengine nje ya bunge na CCM mpya.

CCM ni moja na yenye nguvu zaidi, Wapinzani tafuteni mbinu mpya, CCM imempa mamlaka ya asilimia 100% Mwenyekiti kwa kupiga kura za ndio Dodoma, Sauti yake ni sauti kuu. Hakuna mwanachama atakaye tenda nje ya Maamuzi ya Chama

Wapinzani msisubiri eti CCM kutakuwa na mpasuko ili mpate hoja za ubunge, Bunge linakwenda kuwa la kimkakati kupitisha hoja maalum ya ukomo wa Rais madarakani.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,471
2,000
Dalili zinaonekana, mtu kama Musiba anataka kwenda bungeni kufanya nini?!

Amesifia kwenye gazeti lake ameona hiyo haitoshi sasa anataka kupeleka mapambio yake bungeni, hilo bunge lijalo linaweza kuwa la hovyo zaidi ya lile lililopita la Ndugai.
 

Kwekitui

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
837
1,000
Ni point nzuri hizo
Ila kwani hata wakisema aongeze muda wa ukomo wa urais unadhani kuna mtu ataandama kulipinga hilo? Thubutu tulivyo waoga hivyo.. wale mlio karibu na kituo cha polisi Oysterbay mnaona yale yanayoendelea hivi karibuni milio ya risasi kila mara kama una pressure huwezi kuendelea kukaa maeneo yale ...walivyohoji kwanini wakaambiwa watu wapo mafunzoni...daah sasa kama ile milio inasikika vile eti ni mafunzo si wangetoka nje ya mji kidogo ili kuepusha hofu kwa wananchi walio karibu na maeneo ya Oysterbay Morocco na Msasani
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,396
2,000
Kwani CCM itashinda uchaguzi?
Kuna kitu inaitwa "SHIKWAMBI"
Maana yake "Shinda kwa Mbinu "

Iwe Jua au Mvua, Iwe kelele au vicheko ccm itashinda kwa mbinu

Serikali za mitaa ilitumika mbinu inaitwa "KATA" maana yake katisha tamaa

Sasa uchaguzi mkuu ni mwendo wa "SHIKWAMBI"

Ahaaa Mshana huyajui Haya, Hujapata kuyasikia Haya

Na mwenye masikio na asikie, Hata hii mbinu ilipata tapakaa majimbo yote kuanzia kusini hata kaskazini kwa wenye roho ngumu nako ilipata kutumika

Ni nani mwenye kuhoji kazi nzuri zilizofanyika kwa miaka mitano, Ni wewe Mshana

Hujasikia habari kuu za SGR, Uchumi wa kati, Flyovers

Yote hayo ni sehemu ya Shikwambi
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,804
2,000
Thats logical bunge likiwa limejaza amateurs ambao hawana uzoefu wa kubishana juu mwelekeo wa chama ata kama wote wasomi Magufuli can do pretty as he pleases akiamua kubadili katiba wala sio issue.

Hila kubadili katiba ya nchi ni jambo moja na kubadili katiba ya CCM ni jambo jingine na huku ndio kuna amua upate ridhaa ya kuendelea ata yeye Magufuli atakuwa anajua hii ni mission impossible ndani ya CCM.
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,853
2,000
Dalili zinaonekana, mtu kama Musiba anataka kwenda bungeni kufanya nini?!

Amesifia kwenye gazeti lake ameona hiyo haitoshi sasa anataka kupeleka mapambio yake bungeni, hilo bunge lijalo linaweza kuwa la hovyo zaidi ya lile lililopita la Ndugai.
Inamaana Ndugai hatakuwepo Mjengoni kutetea Kiti chake??

Sasa ndipo napata picha halisi kwanini Membe amekataa kusubiri hadi 2025. Ni wazi Jiwe hataachia madaraka.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,953
2,000
Nilitegemea bavicha kuchafua bada ya kusikia Makonda si RC tena,lakini wamekua bardiii,kumbe wamenywea wanaona akiingia bungeni atakua hatadi sana kuliko kuwa RC
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom