Sipendi sana mazingaombwe:
Chama chenu
Serikali yenu
Sera zenu
Sheria mtunge nyinyi
Vyombo vya usalama vyenu
Watendaji mteue nyinyi
Majaji wote mmeteua nyiyi
Wakuu wote wa vyombo vya usalama mmewatua nyinyi
Mwanasheria Mkuu wenu
DPP wenu
Ikulu yenu
Bunge lenu
Mawaziri wote wenu
Manaibu wote mawaziri wenu
LAKINI MNA UJASIRI WA KURUKA KIMANGA KANA KWAMBA SERIKALI IMEUNDWA NA CHADEMA na wapo watu katika akili timamu kabisa wanafurahia haya maonesho yenu!! Kama kweli leo mmefunguka na kukombolewa kifikra basi fungeni kamili! Fungeni na mtoke kwenye giza na kuja kwenye mwanga. Hamhitaji kusubiri 2015! Jiuzuluni leo hii ili mjipe nafasi na kuhesabiwa! Vinginevyo, watacheza kwata wale wenye kuamini mnaweza kuwapigisha kwata la akili!!
HAYA YALIKUWA 2008 - SIKILIZENI KWA MAKINI WANAYOSEMA WABUNGE WA CCM HALAFU MSEME KAMA LEO WAMEFUNGUKA?
Well said MM. CDM tusirudie tena makosa ya 2010 kuwaingiza watu kama Shibuda. Yeyote anayetaka kuingia kwenye historia ya mabadiliko ni lazima atoke hadharani sasa ili ahesabiwe.