Wabunge wa CCM mnawachezesha Watanzania "kwata" la akili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM mnawachezesha Watanzania "kwata" la akili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 18, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sipendi sana mazingaombwe:

  Chama chenu
  Serikali yenu
  Sera zenu
  Sheria mtunge nyinyi
  Vyombo vya usalama vyenu
  Watendaji mteue nyinyi
  Majaji wote mmeteua nyiyi
  Wakuu wote wa vyombo vya usalama mmewatua nyinyi
  Mwanasheria Mkuu wenu
  DPP wenu
  Ikulu yenu
  Bunge lenu
  Mawaziri wote wenu
  Manaibu wote mawaziri wenu

  LAKINI MNA UJASIRI WA KURUKA KIMANGA KANA KWAMBA SERIKALI IMEUNDWA NA CHADEMA na wapo watu katika akili timamu kabisa wanafurahia haya maonesho yenu!! Kama kweli leo mmefunguka na kukombolewa kifikra basi fungeni kamili! Fungeni na mtoke kwenye giza na kuja kwenye mwanga. Hamhitaji kusubiri 2015! Jiuzuluni leo hii ili mjipe nafasi na kuhesabiwa! Vinginevyo, watacheza kwata wale wenye kuamini mnaweza kuwapigisha kwata la akili!!


  HAYA YALIKUWA 2008 - SIKILIZENI KWA MAKINI WANAYOSEMA WABUNGE WA CCM HALAFU MSEME KAMA LEO WAMEFUNGUKA?


  [video=youtube_share;Uvpaxg1ksr4]http://youtu.be/Uvpaxg1ksr4[/video]

  [video=youtube_share;43uIv7_VSnY]http://youtu.be/43uIv7_VSnY[/video]
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,402
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  I love JF. Hakika MM umenena ya msingi. Tunahitaji muda kuwaamini hawa wabunge wa chama cha mapinduzi ili tujuwe kama kweli wameamua kukipindua chama chao. Maana tulishawahi kuwa na G55, vilevile tulishakuwa na wapambanaji wakati wanaopambana nao ni mabosi wao... KUWASHINDA NI NGUMU. Wengine walitaka kuanzisha CCJ lakini bado wapo kule kule... Siyo wa kuwaamini kirahisi hawa
   
 3. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,146
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Tukio la leo ndani ya bunge,si la kawaida hata kidogo na litabaki katika kumbukumbu,ufisadi uliotolewa hadharani hakika umewafanya hata hao wabunge wa ccm kugundua kwamba kelele za wapinzani huwa zinaashiria ukweli halisi,
  Na impact ya kule Arusha kwa Ole millya na jinsi tukio hilo lilivyopokewa na jamii, na hasa inapoashilia anguko la kigogo Ole sendeka jimboni kwake simanjiro toka kwa millya CDM.
  Huku wao wakikomaa mikono kwa kuchubua meza za bunge kupiga ndiooo!,na yule anayewaharibia pamoja na aliyemteua wote wanakula kuku ughaibuni kila mtu nchi yake.
  *wamekaa kila mmoja ametafakari na akachukuwa hatua kwamba bora UBUNGE kuliko ukerketwa!,na sasa ndio wamegundua kwamba gari walilopanda Dereva wake haoni vizuri,kondakta anawazidishia nauli na turn boy amelewa na hawezi kuziba pancha.
  KILICHOJILI, SASA,kila mmoja sasa ameamua kuchukua maamuzi magumu kwa manufaa ya familia yake maana basi walilomo linaelekea kupata ajali kama ya lile basi maarufu la kenya lililotumbukia shimoni maarufu kwa jina la KANU likiendeshwa wakati huo na Dereva maarufu Moi.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  It is like a tale,
  Told by an idiot,
  Full of sound and fury,
  Signifying nothing!

  - Shakespeare, Macbeth
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wabunge wa ccm hata wangeongea wakajaza viti vyote mate!. Ni wanafki tu!, ni hofu inaanza kuwapata... 2015, tusiwaamini kamwe.
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Siku zote walikuwa wapi?Lakini ktk baadhi ya wabunge Wa ccm walikuri udhaifu wao oohhh"tuamke sasa kuwatumikia wananchi"ooohhh wananchi watatushangaa"na mengine ya kufanana hivyo,mimi nnawauliza walikuwa wapi wanakumbuka kuvuta Shuka ilhali pamekucha?Siwaamini kabisa na ukali wao Wa leo tu(waigizaji).
   
 7. SoNotorious

  SoNotorious JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 2,426
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hawa makuwadi wa serikali, wazomeaji wa wakosoaji wa serikali na wagonga meza leo wanatuzuga watanzania wanafikiri sisi ni maiti, hatuwataki, i cant c u beyond 2015!
   
 8. n

  ngaranumbe Senior Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu hamfichi mnafiki, hata mali ya ushirikina shetani lazima ajionyeshe ni yeye kakupa; nawaambia Watanzania wenzangu wa dini zote na vyama vyote vya siasa, hakika kuna mwisho wa dhuluma. Wabunge(mavuvuzela) wa CCM na wachumba wao wa CUF na vyama vya TLP NCCR nk hawana uchungu na nchi hii hakika, utawaona bungeni wakipiga meza hwahwahwahwaa na ndiyoooooooo. Ni aibu kubwa kwa TZ. CCM ni wezi wa kura Na 1 duniani, wabunge wengi hawakushinda uchaguzi uliopita wa wabunge na rais. Mungu atatujalia CCM ije ikose hata uenyekiti wa nyumba kumi hata kama wana PhD ya kuchakachua.
   
 9. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Dereva yupo Majuu Kumsalimia Maximo!!
   
 10. b

  balosi Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika siku gari la ccm zinahesabika,abiria chukua tahadhari kuepusha maisha yako kabla ya 2015. Vijana tunasubiri lini daftari la kudumu la wapiga kura litarekebishwa?
   
 11. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alinifurahisha yule Mchangiaji wa mwisho wa viti maalum (CCM) aliyekiri kwamba Maisha bora kwa Mtanzania ni NDOTO!
   
 12. m

  maramojatu Senior Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mzigo ndani ya basi si dhamana yetu. Chunga mzigo wako
   
 13. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  MM Umenikosha,wewe mkeo wako ndani unamchungulia akiwa bafuni
   
 14. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Wamwambie JK aachie ngazi kama wanaubavu
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kama kweli wanaona serikali haiendi si wapige kura ya kutokuwa na imani na wazirimkuu ili ajiuzulu na baraza la mawaziri libadilishwe?
   
 16. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji nimekukubali sana kwa tenzi zako. Hawa jamaa wanakumbuka shuka wakati kulishapambazuka. It is too late to catch the train.
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hizi ndio siasa ngumu tunazotakiwa tuwe tunapita kwa nyakati kama hizi....
  Ila sio Tanzania ya sasa, iliyobemendwa na Chama Cha Mapinduzi.
   
 18. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  MMM.... its not a spin, ufa umeanza kuonyesha ya chumbani!!!!!

  chunguza utagundua... NI kama yale ya NEC na CC, mpasuko umevuka bendera sasa umeingia kwenye madawati
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  subiri utasikia, ndanda kosovo akipata nafasi ya kikao kimoja tu na wanawe, utasikia habari...........
   
 20. S

  Stephen Buloya Verified User

  #20
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Makelele yooote yale. Wana uwezo wa kuleta hoja binafsi kuziba mianya ya sheria na kuongezea nguvu sheria dhaifu. Au kama Mwanakijiji alivyosema, wana weza kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Hivi si katika bunge la mwaka jana tu Serukamba alimtolea macho Zitto akimkoromea eti "wapinzani wana nongwa kungangania" wabunge waondolewa kwenye bodi za wakurugenzi kwenye mashirika ya umma. Leo hii ndo anajifanya kukoremea serikali yake? Wabunge wa CCM ni wanafiki wa kutupa!
   
Loading...