Wabunge wa CCM mmechimba kaburi la kukizika Chama

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Kwamba ili Serikali ya Awamu ya Sita ikamilishe miradu ya kimkakati, ilianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano na kuboresha Huduma za Jamii (Afya, Elimu, Maji nk) ni kuweka tozo kwenye miamala ya simu, ati ni TOZO SHIRIKISHI.

Hakuna ubishi kuwa mmewagusa watu wa kipato cha chini ambao hutegemea miamala ya simu kwa shughuli zao za maendeleo na kijamii. Hao ndio wapiga kura ambao Serikali ya Awamu ya Tano iliwajali na kuadabisha mafisadi.

Mmemhujumu Rais Samia Suluhu Hasan kupitisha sheria hiyo. Kuanza kutekelezwa kwa hiyo sheria haraka haraka bila Kanuni na Taratibu kuwekwa wazi, ni ushahidi wa hoja yangu.

Wakati mnapata malipo na marupurupu mengi yasiyo na kodi, mtambue mmewakosea wapiga kura na mtaadhibiwa kama Wabunge kwenye sanduku la kura. Mmekichimbia kaburi chama chenu.
 
..sio sahihi kupandisha kodi, na kuongeza tozo mbalimbali, kipindi hiki ambacho vyuma vimekaza, uchumi umeyumba, na wawekezaji wamekimbia.

..kwanini suala hili halikusubiri mpaka pale Rais atakapoweka uchumi sawa, na wawekezaji watakapoanza kurudi nchini?
 
Acha upotoshaji usio na tija yoyote, ccm hawategemei kura za wananchi kukaa madarakani. Rais aliye madarakani kwa kutumia katiba hii mbovu anaagiza tu Tune ya uchaguzi imtangaze mgombea wa CCM.
 
Kwamba ili Serikali ya Awamu ya Sita ikamilishe miradu ya kimkakati, ilianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano na kuboresha Huduma za Jamii (Afya, Elimu, Maji nk) ni kuweka tozo kwenye miamala ya simu, ati ni TOZO SHIRIKISHI.

Hakuna ubishi kuwa mmewagusa watu wa kipato cha chini ambao hutegemea miamala ya simu kwa shughuli zao za maendeleo na kijamii. Hao ndio wapiga kura ambao Serikali ya Awamu ya Tano iliwajali na kuadabisha mafisadi.

Mmemhujumu Rais Samia Suluhu Hasan kupitisha sheria hiyo. Kuanza kutekelezwa kwa hiyo sheria haraka haraka bila Kanuni na Taratibu kuwekwa wazi, ni ushahidi wa hoja yangu.

Wakati mnapata malipo na marupurupu mengi yasiyo na kodi, mtambue mmewakosea wapiga kura na mtaadhibiwa kama Wabunge kwenye sanduku la kura. Mmekichimbia kaburi chama chenu.
Sijajua serikali ina mikakati gani ambayo haiwezi kutumia kodi za kawaida mpaka wafikiria huku kwenye tozo. Anyway ulichoandika kina points zake.
 
Back
Top Bottom