Wabunge wa CCM kwa nini mmekuwa wabinafsi hivi ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kwa nini mmekuwa wabinafsi hivi ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Jul 13, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  KILA SIKU UKIFUNGULIA REDIO Unachosikia kutoka kwa wabunge hasa wa ccm akiwemo kiongozi
  wao Job ndugai ni namna ya kujinufaisha wao kupitia posho na bima za afya kwa wao wabunge sasa unajiuliza
  wabunge hawa wako bungeni kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi au wako bungeni kwa ajili ya kutatua
  matatizo yao binafsi. ungetegemea bunge linajidili namna ya kusisaidia hospitali zetu zinazowaudumia watanzania
  walio wengi mbunge anajadili namna serikali itakavyomsaidia yeye na familia yake kupata BIMA YA AFYA ni aibu kubwa.
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Job Mbaruka Yusto Ndugai,

  Hebu jiangalie utendaji wako wa kazi siku hizi, Kiukweli kabisa hutendi haki hata kidogo. Hebu fikiria maneno aliyoyatoa 6 kwa wapinzani, hivi kweli yangekuwa yametolewa na Mb wa upinzani na hasa CDM si ungempa siku3 alete uthibitisho, ushahidi vielelezo nk, lakini kwa 6 achilia mbali kutompa yeye nafasi ya kufafanua alichomaanisha na pengine angefuta kauli, wewe ukakomelea msumari kwenye matusi yake ukisema kweli wapinzani ni Wanafiki.

  Kweli unaona ni kauli ya kutolewa na spika hiyo, kabisa yaani wewe unaunga mkono neno lenye utata. Uliombwa muongozo, kwa nini hukuutoa??

  Jamani, ccm mmekuwaje?? Halafu mje mtafute mchawi 2015?? Hasa wewe ambaye watu walikuwa bado na imani na wewe, halafu umeanza kujichafua mwenyewe, hujipendi au??
   
 3. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hali halisi inaonyesha wabunge wa magamba wameshapiga picha huko tuendako na wanaona giza nene limetanda. Hasa kwa vile serikali ya ccm imeshindwa kazi na hii siyo siri. Kinachobakia kwao ni ku-plan namna ya kuchukua kila kitakachopatikana na ndiyo maana wanataka marupurupu yaongezwe zaidi na maslahi mengine katika miaka yao iliyobaki kabla ya uchaguzi. Utaona pia kuna kasi kubwa ya kuuzauza nchi katika nyanja mbalimbali kwa mgongo wa kinachoitwa kilimo kwanza. Watahakikisha madini yote yameisha, ardhi ya nchi nzima wamepewa wageni kwa maslahi yao na kuuza kila kinachowezekana. Haitakuwa ajabu kesho ukasikia hata watu wenyewe tunauzwa. Kaeni chonjo
   
 4. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa fikira zangu ndogo, mimi sidhani kama mapinduzi ya kweli na maendeleo endelevu yataletwa na wanasiasa uchwara wetu..Ifike wakati tusema TOSHA kwa wabunge na tufanye Social revolution kama Misri..Misri, wamemwondoa Mobarak lakini bado hawajaridhishwa na mabadiliko yanayofanywa na Serikali ya Mpito ya Kijeshi kuhusu mambo mengi ikiwepo na lakuwafikisha mahakamani polisi waliowauwa Raia, wamerudi tena barabarani hadi kieleweke. Nafikiri hii ndio njia pekee iliyo salia hapa kwetu kwa sababu wabunge wetu hawatusaidii kitu na wale wachache wenye dhamira ya Ukweli wanazidiwa na wasio na uchungu na wananchi wa Tanzania. Nilisha sema Nchi hii si ya CCM nchi hii ni kubwa kuliko CCM. sasa, ni kwa nini CCM inataka kuwa kubwa kuliko Tanzania?
   
Loading...