Wabunge wa CCM kuweni wazalendo japo kidogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kuweni wazalendo japo kidogo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rich Dad, Feb 9, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jana wakati wabunge wa Chadema wakisusia kikao kilichokuwa na nia ya kutoa tafsiri ya kambi rasmi ya upinzania bungeni, sikutaka kuamini kile nilichokuwa nakisikia kutoka kwa wabunge waliobaki ( kwa uwingi wao CCM). Kutoa lugha chafu za kejeli kwa wenzao waliokuwa wanatoka sikuona hata chembe ya busara waliyonayo.
  Yaani kumbe nimegundua ni watu waliozoea mipasho, upashkuna, na maneno ya vijembe vya kwenye taarabu na Kanga.

  Kweli hawa ni watu watanzania tunaowategemea watajadili mijadala yenye maslahi kwa taifa?? MMh inatia mashaka mno.

  Ushauri wangu;
  Binadamu ameumbwa na mdomo mmoja, na masikio mawili. Mungu alikuwa na makusudi yake kuweka masikio mawili, sikia zaidi kabla ya kurusha maneno. Nashauri bunge liweke kozi maalumu zitakazowaandaa wabunge wote kuwafanya watambue kwamba bunge sio sehemu ya vita ya kutumia nguvu, hoja zenye maana na ushawishi ndio nguvu pekee itakayokuwezesha kumu-win mpinzani wako.

  Kozi za soft skills pia zinahitajika kwa wabunge i.e. presentation skills, persuasive skills, interpersonal skills n.k
   
 2. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hakuna cha kushaangaa hapo mzeee, mipasho kwa ccm ni kawaida mnoo. kwanza nikukumbushe kuwa ccm ni chama pekee kinachomiliki kundi la taarabu TOT, Pia mwenyekiti wao ndo kawaambukiza mipasho ulitegemea kamata au mrema angesema nini wakati wanaume wanatoka bungeni?
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duh kuna mama mmoja nilisikia anamung'una maneno ya kiingereza cha kuungaunga kuwatupia wanaume. Alikuwa anajaribu kuongea kiingereza kwa lafudhi ya kikwere.
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa mbona wanapotosha?
  Ni wabunge wa UPINZANI ndio walilalamika au ni WANANCHI pamoja na WANAHARAKATI?
  sasa kwa nini CCM wanapotosha tena Bungeni?
  wana mdanganya nani hawa wenye MAGAMBA?
   
 5. M

  Msharika JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndiyo CCM zaidi ya uijuivyo
   
 6. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Achana na hao watu wameshamaliza wamenunua mafenicha ya mamilioni huku hata wazazi wao wanakaa kwenye nyumba zisizoeleweka, saa hizi wanasubiri posho tu za maanna makinda!
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Halafu wanapewa MIKOPO mingine, kuna mmoja kalalamika kuwa MAKATO yamezidi, BUnge liwafikirie jinsi ya kuamishia MAKATO sehemu nyingine!
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wapo wabunge walilalamika, magazetu yapo, katafute, mie nawajua, halafu wakazikimbilia fasta kuzichukua.
   
 9. k

  kakini Senior Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wapo akam wamelogwa na wao wenyewe wanalogana
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WABUNGE wamewalaumu watu wanaohoji kwa nini wamekopeshwa Sh milioni 90 kununua vyombo vya usafiri na wanaowashutumu kwa kununua magari ya kifahari.

  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, amesema bungeni mjini Dodoma kuwa, kuna watu wamekuwa wakipotosha kuhusu malengo ya mikopo hiyo na akawashangaa wabunge wa kambi ya upinzani kwa kujiweka kando kama vile mikopo hiyo haiwahusu.

  Malecela amesema, usafiri ni jambo la msingi kwa Mbunge ili aweze kuwahudumia wapiga kura wake hivyo wana haki ya kukopeshwa. Ametoa mfano wa jimbo lake kuwa lina kata 15, 10 kati ya hizo ni eneo lenye milima mirefu, na tano ni eneo tambarare.

  “Naomba wananchi wote mliotuchagua muelewe kuwa hii ni mikopo, tunakatwa kwenye mishahara mwisho wa mwezi” amesema Mbunge huyo wakati anachangia Azimio la Bunge la kurekebisha Mfuko wa Kutoa Mikopo kwa Wabunge na kuunda Mfuko wa Mikopo kwa Watumishi wa Serikali Kuu.

  Mbunge wa Nzega (CCM) Dk. Hamisi Kigwangala, anashangaa kwa nini watu wanalalamika kwamba wabunge wamekopeshwa na kwamba, kwa sababu za kisiasa, jambo hilo limekuwa likipotoshwa.

  Mbunge amewataka wapinzani waache kuwapotosha Watanzania na akadai kuwa hali ikiendelea hivi, taifa halitafikia malengo yake ya kukuza uchumi.

  Mbunge wa Ukonga (CCM), Eugen Mwaiposa, amesema bungeni kuwa kauli za kupotosha kuhusu mkopo huo zimewafedhehesha. “Ile ni mikopo ambayo tunakatwa katika mishahara yetu” amesema Mbunge huyo wakati anachangia azimio hilo.

  Mwaiposa amesema, Serikali pia inapaswa kuangalia utaratibu mwingine ili wabunge wasikatwe bima katika mikopo ya magari.

  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Stella Manyanya, amesema, wananchi wamekuwa wanahoji kwa nini wabunge wamenunua magari ya kifahari ikiwa ni pamoja na Toyota Land Cruiser badala ya gari kama Suzuki.

  Source: Habari Leo

  Surprising Careers With High Earning Potential

  These occupations have the potential to pay more than you might think.

  Pop quiz: who makes a fatter annual income?

  Nuclear techs or elevator repairmen? How about power plant operators or funeral directors? Urban planners or high school art teachers?

  The correct answers may surprise you.

  •Elevator repairmen ($67,950) edge out nuclear technicians ($66,700) in annual income.
  •Funeral directors ($60,390) beat power plant operators ($60,270).
  •High school art teachers ($68,230) make more than urban planners ($64,680).

  USA wage by yahoo.com
   
 11. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,279
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  wabunge wa chadema wamekaa kimya, kwako unaitafsiri vipi?
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Niliweka post moja hapa juzi kwamba CCM ni sawa na gari chakavu au kuukuu linalotoa moshi mwingi barabarani, na mafundi kila wanapofanya tune up ndo moshi unazidi kuongezeka hadi kufeli emission test. Hivyo ni bora kupelekwa recycling dep.

  Mishahara na malupulupu ya viongozi na wawakilishi wa wananchi haviwiani na hali ya maisha ya watanzania wanaowatumikia. Ni aibu kwa wawakilishi wa CCM kuendelea kutetea hali hiyo inayowanyonya walipa kodi.

  Nchi zilizoendelea walimu, na wataalamu mbalimbali wanalipwa zaidi kuliko wanasiasa na ndio wengi wa wanasiana wanafanya zaidi kwa kujitolea. Tanzania walimu na wataalamu wanakimbilia siasa kwa vile mishahara hawalipwi kadiri ya taaluma yao.

  Katu hatutaondokana na hili hadi mapinduzi ya kweli ya kijamii yataweza letwa na chama kingine chenye itikadi tofauti na chama kikuukuu cha ccm.
   
 13. e

  englibert Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wasiwafanye watanzania wajinga ,kwani katika hali ya kawaida mshahara unao weza kulipa mkopo wa milioni tisini kwa miaka mitano ni mshahara mkubwa sana ambao mafisadi tu wanalipwa.
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...Ndio wamejivua gamba hao....haya ngoja tuone..
   
 15. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,139
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wanajipenda kweli..milion 90 zote ni za nini?..
   
 16. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unafiki wa Chadema na Wabunge wao! Hivi Wabunge wa Chadema hawakuchukua 90 milioni? Kama wanaweza kutoka nje ya ukumbi kwa nini wamelamba 90 m nakutulia!!! Sauti ya Wabunge wa Chadema mbona haitoki hapa kwenye 90 milion?
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh, kuna kukuza uchumi wa taifa hapa?
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh, kuna kukuza uchumi wa taifa hapa?
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Ingekuwa ni bora ukaonyesha upande wa pili, wale wa CHADEMA wanaopinga mashangingi!
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Hawalipi zote hizo bali kuna msamaha karibu nusu ya hizo!
   
Loading...