Wabunge wa CCM kuwaadabisha wale wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kuwaadabisha wale wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, Nov 20, 2010.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baada ya kutoka ukumbini wakati Mh. Rais wa JMT - DR. JAKAYA , M. KIKWETE akianza kuhutubia. Wabunge wa CCM sasa wanajipanga kutoa AZIMIO LA BUNGE kwa wale wabunge wote hawamtambui Rais watoke Bungeni hadi pale watakapo mtambua, kwani wameenda kinyume na kiapo chao cha Ubunge cha kutii na kuilinda Katiba ya JMT.
  Na kwa vile wabunge wa CCM ni wengi , hili linaweza kufanyika na Azimio likapata uungwaji mkono wa 2/3 ya wabunge, ambapo CHADEMA hawatapata fursa tena ya kutoa michango yao bungeni.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Natamani itokee haraka hiii!!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani wabunge wa CHADEMA wamevunja kifungu gani cha katiba
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanasema ndani ya katiba Rais ametajwa na mamlaka yake. Kama wakati unaapa 'utailinda na kuitii' ina maana yale yote yaliyomo umekubaliana nayo. Sasa inakuwaje , tena humtambui Rais wakati kiapo chako cha kukuweka ubunge ulisema utaitii na kuilinda katiba?. Hapo sasa ndio jamaa wanataka kuja na azimio la bunge, na kwa kweli itawa affect sana CHADEMA.
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbona mleta mada
  haelezei na kuweka wazi kipengele au sheria ilyovunjwa na CDM?
  Propaganda nyingine bana..agrrrrrrrr!!
  Ila ukweli chama cha mafisadi na serikali yake dhalimu wameshikwa pabaya, na uwezekano wa kujinasua haupo.
  Kuanzia sasa na kuendelea ndiyo mchakato wa kuandika katiba mpya unashika kasi yake hivyo.
   
 6. M

  Mikomangwa Senior Member

  #6
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa CCM wakifanya hivyo watakuwa wamejiandalia kaburi lao 2015. Kura nyingi za "huruma" watapewa wagombea wa CHADEMA. Nawashauri viongozi wa CHADEMA kuanza operation mpya (name it) ya kuhamasisha vijana wajiandikishe kwa wingi kwa ajili ya kupiga kura 2015. Ukombozi wa nchi upo mikononi mwa kizazi kipya na ccm wanalijua hilo.
   
 7. minda

  minda JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  hii ni vita ya kisiasa kwa upande wa ccm hivyo kwa uwingi wao wanaweza kulazimisha hoja na kulazimisha kiti utii wao; m bona kuna mifano mingi.
   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  mypopic vision
   
 9. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  chondechonde ccm. Chondechonde jk. Tafadhali vitendo vyovyote vya ubabe vitahatarisha usalama, amani na utulivu ambao ulijengwa na mwalimu kwa ufundi sana. Ccm isigeuzwe kuwa sawa na mkoloni wa 1954 -1961 ambapo chadema ikawa kama tanu ya kipindi hicho. Nchi yetu haikumwaga damu kuupata uhuru. Vivyo hivyo tunatarajia ccm na ukomavu wake ianze mchakato kwa amani na bila masharti wa kurekebisha kasoro za taratibu za uchaguzi na ikibidi katiba. Itakuwa inafanya hivi kwa faida ya kizazi kijacho. Kwa kufanya hivyo ccm iajijengea heshima kubwa kwa kizazi kijacho. Vinginevyo ikitumia ubabe leo itakuwa imepandikiza bomu ambalo litakimaliza kizazi kijacho.
  Hadi sasa tuna statesmen 2: Mwalimu kwa kuwezesha kuleta uhuru bila kumwaga damu 2. Mzee wetu rahim mzee mwinyi kwa kuleta mageuzi makubwa ya siasa na kiuchumi bila damu kumwagika. Chonde chonde jk uwe statesman wa tatu katika kuleta mageuzi ya katiba ambayo itaendelea kuitunza amani hii na kuleta maendeleo makubwa zaidi ili kizazi kijacho kikukumbuke. Acha ubabe na usiwasikilize wanaokuchochea ufanye ubabe. Dira yako iwe ni kizazi kijacho. Ili jk afanikiwe kuwapuuza wapinzani ni kufanya hayo mageuzi - ataona kama watakuwa na kuu jipya.
   
 10. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama swala ni kuilinda na kuitetea katiba,ina maana haibadilishwi daima? imekuwa msaafu/biblia? think twice before posting rabish matter to us..
  Sasa bungeni unaona wameenda kutembea/picnic? WaTz tumewatuma wakafanye kazi kwa kura zetu, MSITAFUTE MAKUBWA ZAIDI. You have matter on your table,you have to learn to deal with it, as consequences of your whole system of UCHAKACHUAJI
   
 11. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Je, Katiba ikizingatiwa kikamilifu Rais huyu amechaguliwa na umma au na NEC?
   
 12. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #12
  Nov 20, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Naomba mungu wafanye hii move ili mwisho wa CCM uje mapema kwani tumechoka kusubiri, haitakuwa tofauti na kile kitendo cha kumtoa Zitto kabwe bungeni kwa kuanika madhambi ya Karamagi na mikataba ya ajabu.
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Nov 20, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nadhani CCM wanajua yaliyowakuta baada ya kutumia wingi wao kumwadhibu Zitto; sidhani kama watakuwa wajinga kurudia makosa ya nam,na hiyo. Ila kama inavyojulikana, madaraka bila hekima ni kiwanda cha ujinga; sitashangaa wakirudia kosa hilo.
   
 14. P

  Preacher JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wasilete "uswahili" kama jk - wachukue hatua za haraka kulinusuru taifa letu la Tanzania - shida ziko kila upande halafu wanafikiria mambo ya kupambana na Chadema - hivi wanajua kuwa kodi zetu ndio zinawalipa posho????? wasilete maudhi zaidi ya yaliyoletwa na kiongozi wao wa ccm kwa kuiba kura - enough is enough

  kiongozi wao bado anacheka cheka tu na kutoa hopeless hotuba - "tutafanya hivi ........tutafanya hivi - na wabunge wa ccm wanampigia meza wakati wanajua kabisa He is lying ...................... God Help Tanzania
   
Loading...