Wabunge wa CCM kutoka kusini (Ruvuma, Mtwara, Lindi) mnalala.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kutoka kusini (Ruvuma, Mtwara, Lindi) mnalala....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bushman, Aug 2, 2011.

 1. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,302
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli silizishwi na utendaji wa baadhi ya wabunge kutoka kusini,nasema hivyo kwa kusini mh.baruan (cuf) alfani kutoka lindi mjini ndio akisimama unaona ajenga hoja wengne duuuuuu,kama keptain komba ulitumwa ukasinzie?hali ya kusini ni mbaya nyie mnagonga meza tu kushabikia chama kimbunga kinakuja hamponi hamtarudi kwa sababu wenzenu chadema wanajenga hoja za msingi na data za kutosha nyie mnalala tu barabara mbaya,umeme wa majenerata,inasikitisha lakini kitu kimoja kila mmoja atahukumiwa kwa matendo yake nyie shabikieni tu chama chenu hicho cha ccm mh. Ole sendeka jana kasema serikali inaelekea kufa tuone mtaenda wapi ninyi?,hamoni mfano kwa wabunge wa kigoma na kaskazini wanavyokomaa na serikali?mnatia aibu basi msimamame mchangie hata wazo la tupande miti,lakini hata hilo,mnafurahishwa na umaskini huu? Mabadiliko yanakuja miaka 50 ya uhuru umeme wa genereta hakuna viwanda rasilimali ziko nyingi nyie mnalala usingizi tu mnatia aibu mnooooooooooooo!
   
 2. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa Namna Bunge lilivyo na namna ya hulka za viongozi wetu wa sasa NALAZIMIKA kukubaliana na hoja hii ( Ingawaje kwa uhalisia wake kuna punjepunje za ukanda).
  Hata hivyo baada ya kutoa huo msimamo wangu wa kimantiki, naona ni kweli hawa jamaa hawajaweza kuwa formally unified na kutetea kile wananchi kinachowakumba. Mfano mzuri ni wabunge wa kanda ya Ziwa - kule Pamba inakolimwa.... time around the clock kuna kitu kinakujaa very serious kutoka kwa wabunge hawa. Wengine ni hawa wa Kigoma, hawa jamaa they are divided in the lines of their political inclination but are strongly linked and connected kwa umasikni wa watu wao ( minus P. Serukamba)
  Lakini si unajua huko kuna Mawaziri kibao!!! Hawawezi kupiga kelele.
  Kwa hawa wa Kusini, tatizo lao ni their historical inferiority, na ni kwa namna walivyopata Ubunge wenyewe...wengi wameshikwa mkono na kupelekwa yaani ebu kaa hapa....
  Pole
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,567
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kama Barwany ndiye anaonekana kuwasemea watu wa kusini basi mjitahidi uchaguzi ujao muwachague wabunge wa vyama vingine, hawa magamba hawajali maslahi ya wananchi kabisa na hususani watu wa kusini, mtaendelea kukaa gizani, miundombinu mibovu hadi muamke.
   
 4. A

  AridityIndex Senior Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtu wa kusini pamoja naungana na mtoa mada kuhusu kitendo cha wabunge wetu kuto kuwa machachari kama wabunge wa siku za nyuma akina mheshimiwe Stephen Nandonde. Hata hivyo hayo mengine yaliyoandikwa na yalichangiwa yameniacha hoi maana hata sijuwi mtoa mada na wenzako mnaongelea kusini ipi?. Maana nijuwavyo mimi lindi na Mtwara wana barabara safi wao hufika mapema kuliko aendae Dodoma, Iringa, Moshi na Arusha. Wana uhakika wa umeme kuliko sehemu zingine za nchi tena umeme wao hauathiriwi na climate variability kama ule wa mtera. Kuhusu viwanda hatukuwahi kuwa navyo tu tangu enzi hizo ila sasa vimeanza kujengwa viwanda vya korosho, na siku chache zijazo kutakuwa na kiwanda cha cement, mbolea nk.


  Anyway kama ulitaka wabunge wetu wasimame na kumkaba koo ngereja kwa hoja ya Giza basi kuanzia sasa ujuwe hiyo si hoja Kusini na wana haki ya kusinzia mijadala ya hivyo inapoendelea. Anyway mlishaaminishwa kuwa huku ni kwa mwisho, nanyi mkaamini endeleeni kuamini hivyo hivyo. Kuhusu soko na bei ya korosho suluhisho lishapatikana na mapungufu yaliyopo sasa wala si ya kitaifa ni usimamizi wa vyombo vya ndani ya eneo hakuna haja ya kujadili huko bungeni. Nadhani kitendo cha kutupwa enzi za nyuma za akina JKN na Mwinyi imetusaidia wakati nyie mkiona vikwazo kila eneo sisi tunaona fursa na ahueni. Ingawa CCM hatuitaki kabisaaaaaaa.
   
 5. K

  Kimbondo Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ebwana hiyo ni kweli kama huku NEW WELL Bw.Mkuu wa chika yaani Tunashida ya maji lakini huyo bwana amekalia kuwatisha wafanyakazi wa halimashuri fulani tu.Na hii ni kwa sababu ubunge wenyewe aliupata KIMTINDO.
   
 6. K

  Kirungu Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda wewe utuambie unatoka kusini ipi maana unachosema akiendani na hali halisi ya mikoa iliyotajwa kwenye hoja. Hizo barabara unazozungumzia nizipi? ukiondoa barabara ya kutoka Dar iliyojengwa na mkapa? Mtoa hoja amesahau, pia wanaongoza kwa kurupuka kutoka usingizini na kugonga meza kushabikia upuuzi kutoka kwa wana ccm wanzao.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu unamaanisha daraja? kwani barabara hata sasa hivi bado inajengwa na haijakamilika karibia km 60.
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Maendeo ya mikoa ya kusini hayaonekani. Barabara ya Ruvuma mpaka Mtwara kupitia Lindi, ni muhimu sana , lakini wabunge wote wa kusini hawajaona hilo. Ukija Ruvuma, Kuna ziwa nyassa kuna samaki aitwae Mbassa. Huyu samaki anaukubwa wa kama sangara. Lakini hana soko nchini na wavuvi wa samaki huyo bado huishi ktk nyumba za rasta(nyassi). Ruvuma hakujajengwa kiwanda tangia enzi za mkoloni. Ruvuma ndio mkoa pekee unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wasio na kazi. Wao ni kulima tuu kilimo cha Ngama. Wanalima Tumbaku wangoni lakini hawana hata kiwanda cha sigara! Akienda msomi kugombea ubunge, utasikia wananchi wanasema, huyu hakubaliki kichama! Vijana watokao manda, mbamba-bay na kwisi kwi-Ilela,, wao kazi zao ni uvuvi tuu na wametawanyika, Ziwa la mungu, mtera na ifakara. Wabunge hilo hawalioni ni kero ya kukosa kazi za viwandani. Kweli wabunge wa kusini amkeni!!
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Ila hulka ya watu wa kusini si wapambanaji na haiepukiki wanapenda majungu sana na umbeya ,kigoma mwanza tarime kilimanjaro mbeya rukwa arusha bukoba, wana hulka ya kuhitaji majibu sio blah blah
   
 10. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,004
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Wengine mnajichokesha kwa kuandika mazingaombwe kama haya? Mkuu we unatokea kusini ipi iliyopambwa na kupambika na matumaini kama haya uliyoyaandika hapa? Tuachie kusini yetu tuhangaike nayo. Tafadhali Mkuu!
   
 11. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aisee wabunge wa mikoa ya kusini ndo chanzo za umasikini mikoa ya kusini yahani wote ni vilaza tu. Jamani wasomi twendeni tukainusuru mikoa ya kusini maana rasilimali zipo nyingi lakini wabunge wetu hao kazi yao kupiga mavuvuzera tu majukwani.
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,799
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Msipoamka kuchagua mtu makini wa kuwapigania mtabaki km wakimbizi kwenye nchi yenu
   
Loading...