Wabunge wa CCM kuna wakati wanachekesha sana, Hamis Taletale atoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,113
2,000
Kuna wakati huwa najiuliza kama hawa wabunge waliopita bila kupingwa wana tija yoyote kwa Chama na jamii kwa ujumla.

Mbunge wa Morogoro kusini mashariki mh Hamis Taletale aka Babu Tale ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule moja ya msingi jimboni kwake.

Babu Tale amesema msaada huo utakuwa endelevu kila watakapozihitaji na kumpa taarifa kwa miezi 6.

Babu Tale amepiga picha ya Ukumbusho na wanafunzi hao wasichana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,981
2,000
Kuna mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema pale Geita mjini, hii ndio ilikuwa ilani yake. Kuomba kuchaguliwa ali akapiganie watoto wa kike kupatiwa hivyo vihifadhio. Kama hamjui umuhimu wake mkamuulize Penny. Kusoma na kuandika kunahitaji utulivu.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,330
2,000
Kuna wakati huwa najiuliza kama hawa wabunge waliopita bila kupingwa wana tija yoyote kwa Chama na jamii kwa ujumla.
Mbunge wa Morogoro kusini mashariki mh Hamis Taletale aka babu Tale ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule moja ya msingi jimboni kwake.

Babu Tale amesema msaada huo utakuwa endelevu kila watakapozihitaji na kumpa taarifa kwa miezi 6.

Babu Tale amepiga picha ya Ukumbusho na wanafunzi hao wasichana.

Maendeleo hayana vyama!
Duh! Una PhD ya unafiki. Acha wapige kazi.
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,517
2,000
Taulo kitu gan had za 1500 zipo
hv unayajua maisha ya kijijini ndugu yangu? hiyo 1500 kila mwezi mzazi anaitoa wapi ya kumpa mtoto akanunue pedi? wasichana wa vijijini wanatumia vipande vya vitambaa tu, so kwa mtazamo wangu Tale amefanya jambo jema sana kwa hao mabinti hasa kwa kuwa ameahidi kitakuwa kitu endelevu kila baada ya miezi 6
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
3,462
2,000
hv unayajua maisha ya kijijini ndugu yangu? hiyo 1500 kila mwezi mzazi anaitoa wapi ya kumpa mtoto akanunue pedi? wasichana wa vijijini wanatumia vipande vya vitambaa tu, so kwa mtazamo wangu Tale amefanya jambo jema sana kwa hao mabinti hasa kwa kuwa ameahidi kitakuwa kitu endelevu kila baada ya miezi 6
Maisha ya kijijini zipo familia nyingi sana bajeti ya pedi haipo kabisa. Utasikia wazazi wanawaambia mabinti zao kuwa mbona wao walikua kwa kujifunga matambala na hadi sasa wapo na wamewazaa.

Pedi ni kwa class flani ya familia, wengine unakuta familia yenye watoto watatu wa kike wananunuliwa kadhaa kwa pamoja kuwa zikiisha watajua wao. Sasa unakuta hapo kuna mmoja anaenda siku 7 mwingine anaenda siku 3 wanazigombania.

Hapa nimeongea experience 99.8%
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom