Wabunge wa CCM kila mara wanaambiwa lakini hawatekelezi Kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM kila mara wanaambiwa lakini hawatekelezi Kuna nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Nov 9, 2011.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka Mh. Rais wa JMT Dr. J M Kikwete wakati wa semina elekezi aliwaambia mawaziri na viongozi wengine wa CCM kuwajibu wabinzani kwa hoja pale wanapoonenakana kubeza mafanikio ya maendeleo ya nchi hii tangu uhuru. Hali imekuwa kimya hatusikii wakijibu kwa kujiamini

  Jana Mh. Waziri mkuu Pinda naye amerudia kuwataka wabunge wawajibu wapinzani wanaobeza maendeleo. Kwa nini hawajibu hali majibu hapo tena mengi tu Hawaonekani wakifanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwajibu wapinzani zaidi zaidi hawapo majimboni. Kwa nini hawabadiliki kutetea chama Nape tu anazunguka nchi nzima hadi USA wengine wako wapi jamani.
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono kauli hiyo, wasiwaache wapinzani watambe kiasi hicho wakati majibu yapo. Amkeni jamani.
   
 3. L

  Losemo Senior Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani atawasikiliza wabunge wa CCM walivyo na ahadi za uongo miaka nenda rudi. Kwanza uongozi wenyewe wanautafuta kwa kununua na baada ya hapo wanatafuta hela za kulipa madeni na kununua uongozi ujao. Wamefilisika sera
   
 4. M

  Mwansiti Omari Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo sio kuwajibu au kulumbana na wapinzani hapo kinachotakiwa ni kujibu utekelezaji wa majukumu yako, umemsaidia nini mwananchi hasa yule wa jimbo lako, umesaidiaje kuleta na uboresha huduma za jamii na mwananchi atafaidikaje na uongozi wako.
   
Loading...