Robinhomtoto
JF-Expert Member
- May 17, 2017
- 238
- 244
Wadau nachukua nafasi has a Kwa Wabunge wa CCM kuacha Mara moja tabia yao ya kuipongeza Serikali badala ya kuibana Na kuisimamia kutekeleza majukumu au miradi ya maendeleo Kwa wananchi.Wabunge wa CCM wamekuwa Na tabia ya kuanza kuipongeza Serikali hata kama haijatekeleza miradi iliyotakiwa kutekelezwa.Tumejionea Bajeti ya 2016/2017 Serikali ilivyoshindwa kuitekeleza lakini ni wabunge wa Upinzani waliosimama Na kupaza sauti Kwa serikali kushindwa kuitekeleza.Tabia ya wabunge wa CCM inakera sana kwani inashusha hadhi ya Bunge kuibana Na kuisimamia serikali.Wananchi ndio wanatakiwa kuipongeza Na kuipigia makofi serikali kama itakuwa imetekeleza miradi yake lakini badala take utasikia Mbunge wa CCM anakiri kabisa Serikali haijatekeleza miradi eti anaunga Hoja Mkono Kwa asilimia 100% ni aibu sana.