Wabunge wa CCM inabidi tu mkubali kuwa mnazidiwa ujanja na wabunge wa upinzani

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Hakuna mtanzania asiyejua kuwa wabunge wa CCM wapo mle mjengoni kwa kuitetea serikali hii hata kama maamuzi yao hayana maslah mapanai kwa wananchi walio wengi.

Nikitoa mfano ulio wazi kabisa ni namna wabunge hao walivyoondoa matangazo ya moja kwa moja ya Luninga (Live Broadcast) ambayo sisi wananchi tulikuwa tunapata fursa ya kuwasikia wawakilishi wetu namna wanavyotusemea huko Bungeni Dodoma

Ingawa hatua hiyo ilipingwa vikali sana na wabunge wa upinzani, lakini kwa kutumia uwingi wao wabunge wa CCM, wakaipitisha sheria hiyo ya wawakilishi wetu kuongea "gizani" Bungeni.

Ikabidi wabunge wa upinzani wabuni mbinu ya kujirekodi wanapoongea humo Bungeni na kurusha "clips" hizo kwenye mitandao ya kijamii, ili wananchi waliowachagia waone namna wanavyowasemea.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alipoona kuwa wabunge wa upinzani wanajizolea umaarufu mkubwa kwa hizo "clips" wanazozirusha mitandaoni, akaamua kuwasihi wabunge wa CCM nao wajibu mapigo kwa kurusha "clips" zao nao mitandaoni.

Lakini nimeshangaa majuzi, Naibu Spika wa Bunge hilo, Tulia Ackson, akipiga marufuku mtindo huo wa kujirekodi na kurusha "clips" hizo mitandaoni na akapiga marufuku kwa mbunge yeyote awe wa CCM au upinzani kujirekodi na baadaye kusambaza kwenye mitandao ya kijamii "clips" hizo.

Ndipo hapo nikajiuliza, ni nini kilichomsababisha Naibu Spika, Tulia Ackson, achukue uamuzi huo?

Hivi yeye hajui kuwa "Bosi" wake Spika Ndugai, alishatoa ruksa kwa wabunge kujirekodi na kurusha kwenye mitandao, lakini akasisitiza kuwa wabunge wa CCM wasiishie tu kulalamikia "clips" hizo Bali na wenyewe wajibu mapigo?

Sasa ni kitu gani kinachowapa kiwewe na kuweweseka hadi waamue hata kupiga marufuku kujirekodi na baadaye kuzirusha "clips" hizo mitandaoni?

Ninachokiona Mimi ni kuwa wabunge wa CCM wameona tayari wamepigwa bao na wabunge wa upinzani, kwa hiyo wanachofanya wao kama kawaida yao ni kutembeza ubabe na kupiga marufuku kujirekodi huko.

Imenenwa na wahenga kuwa ukijifanya unajua huku na wenzio watakuwa wanajua Kule.

Inabidi tu wabunge wa CCM wawe wapole, kwa kuwa ni wao ambao walitetea msimamo wao wa "kipuuzi" kwa lengo la kuzuia matangazo hayo na kutoa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu kuwa kwa kuangalia Bunge Live wakati wa kazi, watakuwa wanapoteza muda wa kufanya kazi!

Hivi niwaulize swali dogo tu nyinyi maccm, hivi TBC wanavyozunguuka naye, Mheshimiwa Rais Magufuli nchi nzima na kutangaza Live mikutano yake yote, tena muda huo huo wa kazi, je yeye ndiye hajui kuwa anawapotezea muda wananchi wake kwa kumwangalia Live muda huo ambao nyinyi mnadai kuwa ni wa kufanya kazi?
 
Back
Top Bottom