Bunge lililopita lilikuwa lenye Wabunge wa CCM na wa vyama mbadala. Hoja zinapotolewa na Wabunge wa CCM hata kama hazina uzito wowote zinashangiliwa lakini zikitolewa hoja zenye maslahi ya Wananchi kwa kiasi gani, kama mleta hoja hiyo siyo CCM basi atazomewa, ataombewa miongozo au tàarifa ya Spika hadi hoja inakosa uungwaji mkono aidha kutekelezwa.
Mfano G. Lema aliwahi kuonya juu ya kuwafilisi wafanyabiashara, kuwakimbiza au kuwabambikia kesi za ukwepaji kodi ili wasote jela. Hakuungwa mkono hata kidogo, akaitwa majina.
Juzi Rais Samia Suluhu karejea kauli kama hiyo ya Mh. Lema na Wabunge wetu waliopinga hiyo hoja Bungeni wanashangilia na kuunga mkono kwa 100%.
Je, huwa Wabunge wana mwakilisha nani pale Bungeni? Nahisi kama hawajielewi wapo Bungeni kufanya kazi gani.
Leo unapinga jambo na kesho unashangilia?