Pius Kafefa
Member
- Aug 9, 2011
- 88
- 20
Nasikitishwa sana na utaratibu wa wabunge wetu kukutana na kuwekana sawa ili kuwa na msimamo mmoja wa kulinda maslahi ya CHAMA. Binafsi sifuarahii utaratibu huu kwani umekuwa ukitumika kulinda maslahi ya kundi fulani. Japo "Lobbying" ni mkakati unaotumika kupitisha hoja kwenye mabunge yetu, nadhani umefika wakati wa kujadili hili hasa kipindi kama hiki ambapo kuna hoja/miswada inayoweza kukwama kwa sababu tu haijazingatia maslahi ya umma.
"Ni wakati muafaka sasa kupima demokrasia yetu kwa misimamo ya wabunge isiyotokana na nia yao mbaya ya kulinda maslahi ya CHAMA".
"Ni wakati muafaka sasa kupima demokrasia yetu kwa misimamo ya wabunge isiyotokana na nia yao mbaya ya kulinda maslahi ya CHAMA".