Wabunge vijana msikubali kujazwa uoga na Dr.Salim na Jaji Warioba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge vijana msikubali kujazwa uoga na Dr.Salim na Jaji Warioba.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Aug 5, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..nimesoma kwamba wazee hawa wamemtuma Zitto Kabwe awakutanishe na wabunge vijana.

  ..lengo ni kuwafunda jinsi ya ku-behave wakiwa ndani ya bunge.

  ..nakumbuka ktk semina moja Dr.Salim na Jaji Warioba walijaribu kila mbinu kuwasihi Mateo Quares na Joseph Butiku wasikemee utendaji mbovu wa serikali ya CCM.

  ..wazee hawa ni WAOGA na sidhani kama wana lolote lile lenye tija la kuwapa wabunge wetu vijana.
   
 2. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hawa Wazee hawana Jipya ktk Kipindi hiki kwa yanayojiri ndani ya Mjengoni,

  Wakiwa kama wazee waastafu wanajua tatizo ktk nchi yetu hasa kipindi hiki wapi tulipo!
  Wangeanzisha CLUB YAO YA MAWAZIRI WAKUU WASTAAFU...!
  Kupitia Club yao wangekuwa na chance nzuri tu ya kutoa ushauri na kutoa ufafanuzi nk....,

  NB. E Lowassa kwa kweli cjui kama anastahili kupewa heshima ya Ustaafu, hilo nawachia wana JFs!

  Bongo yetu ufisadi, ubinafsi na kushindwa ktk uwajibikaji wa Govt kw wananchi...,
  hata watoto wa chekechea wanajua tatizo lipo ndani ya CCM na Govt...

  Just wishing wangempa ushauri JK na kwenda kuifunda CC ya CCM khs nidhamu, uwajibikaji na masuala yote ya ufisadi!
  maana walikuwepo enzi za Julius Nyerere ktk enzi zake!

  Hapa wangelamba Bingo la Ujasiri...!
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wanalinda maslahi ya serikali ndo mana wanataka kuwabana wabunge vijana.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  EL hakustaafu uwaziri mkuu aliwajibika kutokana na utendaji wake mbaya hastahili sifa ya ustaafu.

  Wanaweza kutoa mwelekeo kwa wabunge vijana tusikatae wito tukatae ujumbe, wabunge vijana wanauwezo mkubwa wa kufahamu kama wanatishwa au la. Wawasikilize halafu wachanganye na za kwao!!!!!!
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Aaaah wapi! Wameshindwa kukemea bila kuyumba upuuzi mwingi tu leo wawafundishe nini? Hao vijana ni matunda ya matendo yao! Kwani hao vijana wametokea mbinguni? Kama busara zianzie huko ccm kwa kina nape!
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  wanaacha moshi unafuka wanaibuka moto tayari! Wabunge wa ccm ndo wanaitaji semina kuelewa maana ya kuisimamia serikali.
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naam kidogo sana ama kwa mbali sana nimemsikia Mr Superman au Mwanadiplomasia wa Afrika Dk Salim Mohamed Salim,pamoja na Judge Sinde Warioba wakijaribu kufikisha ujumbe wao kwa waheshimiwa wabunge haswa vijana.

  Ndio ni sawa ujumbe huo muhimu uwafikie vijana hao kupitia Mbunge Zitto Kabwe,ambae ufikaji kwao kwake ni lahisi sana kuliko wabunge vijana wengine.Imekuwa ikifahamika kuwa kimahusiano Zitto yuko karibu sana na Mwanadipomasia huyo wa Afrika sijui kwa upande wa Mzee Sinde Warioba.

  Namkubali na kumheshimu Judge Sinde Warioba katika siasa zetu za ndani,lakini namheshimu pia Mr Superman Mwanadiploamsia Salim Mohamed Salim nikiwa sifurahishwi nae na mwenendo wake wa ukaaji kimya usio na mchango wa kupaza sauti kwa umma pale inapobidi yani anafumbia macho yote yanayoendelea ndani ya Nchi nyuma ya kivuli [Mask] ya uwana diplomasia.Mimi kwake huyu ni mtoto mdogo lakini tunajifunza na kuiga kwa mujibu wa jinsi tunavyowaona.

  Kama ningekuwa kiongozi ningetamani kuwa kama Judge Sinde Warioba kwa haiba ya kuwa na uthubutu na kidogo nivae udiplomasia yaani uzoefu wa kidplomasia wa mheshimiwa huyu Mwanadiplomasia Salim Mohamamed Salim.

  Tulikuwa watoto leo watu wazima tukisikia Salim Mohamed Salim ni chaguo la Mwalimu,hakika mtu unapokuwa chagua la Mwalimu ni matarajio kuwa unakubalika kwa jamii.Lakini Mheshimiwa huyu AMTENDEI HAKI HAYATI BABA WA TAIFA KWA IMANI YAKE DHIDI MHESHIMIWA HUYU ALIVYOITHIBITISHA KWAKE KWA MIONGO NA MIONGO AKIWA TANGU KIJANA MDOGO.Amekuwa mkimya kwa ukimya usio na tija [samahani kwa hili si maanishi kutokuwajibika kwa Taifa] ila nikimaanisha kuwaonyesha umma ni jinsi gani kama kiongozi mwenye uzoefu wa siasa za Taifa na Kimataifa toka ujana wa miaka 22 mpaka sasa anavyoshiriki siasa za ndani za Taifa lake katika uwazi usio tia shaka hasa katika kipindi ambacho jamii iko kwenye mpito wa tikisiko la kiuchumi na kisiasa haswa kupitia chama kilichomlea na kumpa nafasi ya kutumikia kada ya kimataifa.

  Tunajua katumikia Mataifa lakini akija kwetu Tanzania ambako ndio kwao bado anabaki kuwa Mtanzania.Mohammed ElBaradei Mwanadiplomasia mwenzie toka Misrii [Is a well-known figure because of his long-career abroad with the International Atomic Energy Agency in Vienna. The Nobel Peace laureate and former Egyptian diplomat has gained international attention as a vocal critic of Mr. Mubarak and his government.]

  Mohamed ElBaradaei pamoja na uwana diploamsia wake lakini bado alisimama na kusema hapana kwa mtawala Hussein Mubarak.Hivi mtu akivishwa moyo wa Mohamed akimuangalia Mtu mzima mwenzie Mubarak ndani ya Sero za Mahakama hoi kwenye kitandani unafiklia nini kinaendelea kichwani mwake.Anatamani kama angemchomoa ndani ya kasheshe hilo la Wananchi lakini kwa kuwa ni amri ya umma hana jinsi ya kufanya pamoja ya kuwa Mubarak alimtendea unyama na kumnyima nafasi ya kulitumika Taifa lake kwa visingizo vichafu kupitia waandishi wa habari,kama kutokuwepo Nchini humo kwa muda mlefu na kuwa anamiliki pass ya kusafilia kutoka Nje [Foreign Passport].

  Hivyo ugomvi wangu na Mwanadiplomasia huyo makini ni Ukimya na kutokuongea na kuweka msimamo wake na mwenendo mzima wa Taifa hili na siasa na uchumi wake kwenye kipindi hiki cha mtikisiko.Kwa kupitia kuongea kwake kunajenga na kuimalisha kuamini na kuona mwanga na njia ya kujinasua na misukosuko tunayopita.Kwani anajua kabisa mambo mengi yanaendelea juu ya siasa zetu kama chokochoko za Muungano, Mwanadiplomasia huyu kakaa kimya kama sio Mtanzania linae muhusu.

  Anaogopa au ni tabia yake ya ukimya?Je anawaogopa Viongozi watawala?.amewezaje kuwa Kiongozi kwa kuwa ili uwe kiongozi pia ni kuwa na nguvu ya ushawishi kwa Wananchi na wafuasi wako.Kama ni kwa kuchafuliwa kwake yeye kuwa ni kizazi cha Izibu hayo kwetu ni hadithi na hakuna ushahidi wakutoshereza na jamii nzima inajua kilichotokea, Watanzania na Wazanzibar wanajua nani ni nani,kwani siku hizi taarifa nyingi sio siri tena.Kwani Nape, Sita na kina Mwakembe awajaambiwa juzi kuwa wao ni CCJ mbona wako CCM na wanaendeleza mapambano.Jeneral Ulimwengu aliambiwa si Mtanzania lakini hakuweka Kalamu yake chini kufundisha vijana na umma juu ya umuhimu wa viongozi waadilifu [Intergrity Leaders] leo hii wenye akili zao wanajua na kumheshimu Jeneral Ulimwengu kuliko waliomtuhumu ambao kila siku kuishi kwao siku hadi siku kunazidi kuwa ni kwa magutu.

  Wengi walituhumiwa na kashifa kibao lakini kwa kuwa ni viongozi na kwa kuwa sifa ya kiongozi ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuongea na kufikisha ujumbe hata katika mazingira magumu.Fredrik Sumaye kaongea,David Cleopa Msuya kaongea,Mzee Ali Hassan Mwinyi kaongea na hata Marehemu Mzee Kawawa aliongea na kuasa,hata wadhamini wa CCM bado pia waliongea,Mzee Walioba yeye kwake mpaka amekuwa ni sehemu ya mjadala kwa kipimo cha maoni yake na misukosuko ya jamii inayopitia.Mzee Regina Mengi na kumilki biashara zake lakini amekuwa msemaji na Wananchi wamekuwa na support juu yake.

  Hata Edward Lowasa ambae jamii bado inamtuhumu bado yuko barabarani anaongea na kupata support pamoja na vulugu mechi zote zilizoleta mtafaruku kwa Taifa.

  Ujumbe kwa Zitto Kabwe amwambie Mzee huyo kuwa mimi binafsi kama kijana ninamuheshimu Mwanadiploamsia huyo makini lakini naomba ATOKE HUKO KWENYE KUJIFUNGIA CHINI YA KIVULI [MASK] CHA UWANADIPLOMASIA.Awajibike kwa Taifa chini ya kivuli sio cha ubora wake kimataifa bali kama Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Na hayo aliyotaka vijana wabunge wayasikie yeye Salim Mohamed Salim pamoja na Judge Sinde Warioba,David Cleopa Msuya ,Fredrik Tulaye Sumaye na hata mtuhumiwa wa ufisadi Edward Lowasa kama ataweza kuhudhuria manake kwa taswira yake kwa jamii kuhudhuria kwake kwaweza kuwa moto kwa upande wake, WATAYALISHE KIPINDI MAALUMU JUMAMOSI WAONGEE NA WABUNGE HAO VIJANA WA VYAMA VYOTE KUPITIA KIPINDI MAALUM CHA TELEVISION KAMA KONGAMANO LA KUJADILI MWELEKEO WA TAIFA NA KUWAPA DILA[VISION] VIJANA.

  WAJADILI HAYO WANAYOTAKA KUWAAMBIA LAKINI PIA KUNA UJIO WA KATIBA MPYA,SWALA LA MUUNGANO,MAADILI YA UONGOZI [INTEGRITY] NA WIZI WA MALI YA UMMA CHINI YA MIKATABA MIBOVU. TUPATE NAFASI HIYO ADIMU TUSIKIE KAURI ZA WATU HAO MUHIMU HASWA HUYU AMBAE ANASIKIKA KWA ADIMU SANA.


  Nasilisha.

   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jaji Warioba na Barozi Salim pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi wachache sana waliobakia, wanao heshimika siyo tu kwa nyadhifa walizowai kushika lakini hasa kwa uadirifu wao na utumishi wao kwa umma uliotukuka, hata hivyo na wao ni wafaidika wakubwa wa mfumo uliopo husiyo na uwiano hata kidogo katika ugawaji wa keki ya taifa. Kwa wengi wetu tunaiona serikali iliyoko madarakani imejipambanua kuwa kinga kubwa ya udhalimu wa kila aina. hivyo yeyote anayejitokeza kutetea serikali ya aina hiyo, hawe Salim au Warioba ni wakuogopa kama ukoma.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli imenishangaza sana kuwasikia Salim na Warioba wakijaribu kutetea Ufisadi unaofanyika..Naanz akutia shaka sana na uwezo wa Salim kama mshauri wa Zitto yawezekana Uzee ameanza kuvuruga kichwani..
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Niseme nini! Kudos mkuu!
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Binafsi nawaheshimu sana hawa wazee lakini sioni kama watakuwa na kipya cha kuwaambia wabunge vijana. Ningependa kusikia wamewaita mawaziri au waziri mkuu Pinda wampe ushauri wa jinsi ya kuendesha serikali na sio wabunge vijana ambao wanafanya wajibu wao vizuri zaidi ya mawaziri wengi wa serikali.

  Kama alivyosema DSN at least Warioba amekuwa akiishauri serikali angalau kwa woga kuliko huyu mwanadiplomasia Salimu, kuwa kiongozi mzuri ni pamoja na kuwa na uwezo wa kujibu na kujenga hoja kwa mambo unayorushiwa yawe mazuri au mabaya. Toka azushiwe kuwa yeye ni Hizbu yuko kimya, tuseme ni upole au amezira siasa za nyumbani hata kama ni mwanadiplomasia lakini uanadiplomasia wa aina hiyo ni wa kinafiki.

  Tumeona Lowassa, Msuya, Sumaye na wengine ingawa wana matatizo yao lakini wamekuwa na uwezo wa kujitokeza hadharani kujibu tuhuma hata wakati fulani kuikosoa serikali na viongozi waliopo, lakini sijasikia huyu mwanadiplomasia akiikosoa serikali au viongozi waliomadarakani tuseme hajaona udhaifu wowote alichoona ni udhaifu kwa wabunge vijana.

  Nawashauri wabunge vijana wasikatae wito waende ila wakati wakimsikiliza wamwangalie usoni watauona unafiki wake.
   
 12. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umakini wabunge wa upinzani mshishiriki na lolote kutoka kwa hao viongozi wastaafu. Wana jipya gani.

  Waweke kila kitu wazi katika vyombo vya habari ili nasi tuweze kuelewa, wabunge kwa ridhaa zetu wapiga kura ndio tumewachagueni mtuwakilishie kero zetu na kutuletea maendeleo. Bungeni hapo akujakuwa na upotovu wa nidhamu kwa wabunge wa upinzani bali ni upotovu wa wabunge wa chama tawala wanaopinga kila hoja ya maendeleo na kutetea ufisadi na malumbano ya kujaribu kuwaweka chini na kuwanyamazisha wabunge wa upinzani.

  Wabunge wa CCM wamesahau kama wao ni waajiriwa wa wananchi. Wabunge wa CCM mnatakiwa mtoe sauti za wale mnaowakilisha na kutetea maslahi ya taifa ili tuweze kujitoa katika hali ngumu ya maisha na umaskini uliokithiri, wabunge wa CCM sasa hivi mnafaa muige mfano wa mbunge mwenzenu Filikunjombe CCM. na sio kutetea chama na serikali bungeni hilo ni baraza la kutunga sheria au mnakuwa amuelewi nini maana ya uwakailishi wenu bungeni.
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 610
  Trophy Points: 280
  Usikatae wito, lakini pia iwepo nafasi ya kuwa-shoot maswali kujua msimamo wao katika maswala yanayoimaliza nchi kwa sasa.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Zitto Kabwe, mawasiliano yoyote ya aina hii ipitie RASMI kwenye uongozi wa vyama husika na wala kusiwe ni swala la mtu mmoja jinsi ulivyokua approached katika hili.
   
Loading...