Wabunge: Tuko tayari kuweka wazi majibu ya Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge: Tuko tayari kuweka wazi majibu ya Ukimwi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Sep 14, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesema wako tayari kuweka wazi majibu ya vipimo vya mambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi (VVU) hata kama watakuwa wameathirika.

  Walisema hayo kwa nyakati tofauti jana muda mfupi baada ya uzinduzi wa kitabu cha mwongozo kwa ajili ya kuwawezesha wabunge kupambana dhidi ya Ukimwi, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  “Changamoto iliyopo kwenye mabunge yetu ni kwa wabunge kujiweka wazi na kusema mimi hapa nimeathirika. Mimi nikipimwa nikakutwa ninao, niko tayari kujitangaza,” alisema Beatrice Shellukindo, ambaye ni Mbunge wa Kilindi (CCM).

  Pia Mbunge wa Muheza (CCM), Herbert Mtangi, alisema yuko tayari kupima afya kwani ni kawaida yake kufanya hivyo.

  Aliwataka wabunge wenzake kujiweka wazi iwapo wameathirika wasiogope kwenda kuchukua Dawa za Kuongeza Nguvu (ARVs).

  Uzinduzi wa kitabu hicho ulifanyika kwa ushirikiano wa Umoja wa Mabunge Duninai (IPU) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jina la kitabu hicho ni ‘Raising the profile of HIV and AIDS in your Parliament’.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Masula ya Ukimwi, ambaye pia ni Mjumbe IPU, Lediana Mng’ong’o, alisema kitabu hicho kinalenga kuwahamasisha wabunge kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya ukimwi ndani ya mabunge yao na majimboni mwao.

  Mbunge wa Bunge la Seneti nchini Ubelgiji, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri kuhusu Masuala ya Ukimwi katika IPU, Marleen Temmerman, aliipongeza Tanzania kwa kuwa mfano baada ya Rais pamoja na wabunge kupima afya zao.

  Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba.

  Washiriki walikuwa ni mabalozi, wabunge pamoja na wadau wengine wa kupambana na Ukimwi kutoka nchi mbalimbali duniani.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  So What?
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Wameshindwa kuweka wazi wizi na ufisadi leo waweze Ukimwi!
  Wameshindwa kuwekawazi mafao yao leo waweke wazi Ukimwi!

  Kwanini madadapoa wanahamia Dom wakati wa bunge, au ndio wanakwenda kupewa ushauri nasaha!
  Wabunge wetu wanatia shaka sana uwezo wao wa kufikiri hasa kukabiliana na mambo ya kitaifa.
  Hivi hakuna mwongozo wa mambo wanayotakiwa kufanya 'job description'
   
 4. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  ....hilo sisi hatuna haja nalo sana......wekeni wazi mali zenu na mapato mnayopata bungeni kwanza .....
   
 5. g

  gorkava Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  bora.....
   
 6. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii itakua kampeni ya kujitakia kuongeza nyumba ndogo, kama hawajaweka wazi bado mnavinjari hivi je mkitangaza? PRIVACY PLZ
   
Loading...