Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,722
- 21,778
Wabunge Tanzania Wasema Nchi inafilisiwa
Jengo la Bunge Wednesday, April 22, 2009 7:31 AM
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamechachamaa na kuelezea kukerwa kwao na kukithiri kwa utendaji kazi katika makaratasi badala ya utekelezaji wa vitendo.
Baadhi ya wabunge hao walidai kuwa, hali hiyo inaweza kuifilisi nchi bila kuwepo kwa sababu za msingi.
Hali hiyo ilijitokeza wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia mlundikano wa mizigo.
Baadhi ya wabunge hao walielezea kutoridhishwa kwao na utendaji wa mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Mamlaka ya ukusanyaji wa mapato (TRA), kwa kutoonyesha juhudi za wazi za kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam.
Walidai kuwa, wakati Tanzania ina bandari nyingi kama Mtwara na Tanga lakini mkazo umewekwa katika bandari ya Dar es Salaam pekee jambo ambalo linasababisha msongamano wa mizigo.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Lulindi Suleiman Kumchaya alisema hakuna sababu ya kuendelea kungangania kutumia bandari ya Dar es Salaam wakati kuna bandari nyingine.
Alielekeza lawama zake kwa TPA na TRA kwa kutotumia bandari ya Mtwara ili kupunguza mlundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Kumchaya bila kufafanua alisema kuwa, vitendo hivyo vinaweza kuifilisi nchi bila sababu na kushauri kufunguliwa kwa bandari ya Mtwara.
Sisi wote ni watanzania nawaambieni tutakuja kuifilisi nchi hii bila sababu zozote, hizi ofisi ni dhamana tu nendeni bandari ya Mtwara , ifungueni tuachane na kazi za kwenye makaratasi zisizo na ufanisi", alisema Kumchaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mohamedi Misanga alisema kamati yake imepata malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Alisema kamati yake iliwahi kupata malalamiko kutoka Mamlaka ya bandari (TPA) kwamba TRA ndiyo imekuwa chanzo cha msongamano huo.
Wabunge wa kamati hiyo waliiagiza TRA kuanza kutumia bandari ya Mtwara ili kupunguza msongamano wa mizigo, usumbufu na kuliongezea tija taifa.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha kimataifa cha uondoaji wa makasha bandarini (TICTS) Fred Tranchart alisema mlundikano wa mizigo katika Bandari ya Dar es salaam unatokana na wateja wengi kutopenda kufuata utaratibu wa utoaji mizigo na kutafuta njia za panya kutoa mizigo yao.
Akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Tranchart alisema mizigo mingi yakiwemo makontena na magari imekuwa ikikaa bandarini kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutafuta njia za mkato ili kukwepa kulipa ushuru.
Alisema kwa sasa wana utaratibu mzuri wa kuondoa mizigo bandarini hapo ambao unampunguzia mteja kuzunguka na mafaili mkononi kwa kuwa wanatumia njia ya mtandao ambapo mteja anaweza kutoa mzigo kwa muda wa saa 24 toka ulipoingia nchini.
Meneja huyo alisema pamoja na kuboresha huduma hiyo lakini wateja bado wamekuwa wakiacha mizigo yao bandarini hapo kutokana na ukwepaji huo wa kodi kwa kutumia muda mwingi kutafuta njia za panya.
Tatizo la mlundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam limekuwa sugu licha ya juhudi zinazochukuliwa na vyombo mbalimbali.
Katika ziara yake katika Bandari ya Dar es Salaam mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete aliagiza mamlaka husika kuongeza kasi ya kutoa mizigo ili kuuepsha usumbufu.
Bandari ya Dar es Salaam imekuwa tegemeo kubwa la wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi hasa kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia, Malawi na Burundi.