Wabunge sasa kimbilio la utatuzi wa ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge sasa kimbilio la utatuzi wa ardhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Oct 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160  Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla (wenye suti) akiangalia uziouliowekwa na mwekezaji katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji chaKipera, Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro na kuziba njia inayokwendakatika mtaa wa Mwanga na katika mashamba. Pia mwekezaji huyo raia wakigeni amechukua sehemu ya mashamba ya wananchi hao bila ya taarifayeyote kwa Halamashauri ya Kijiji na wananchi.


  Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoa mpya wa Njombe (Iringa)Mhe.Deo Filikunjombe amewataka madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kusaidia kutoa elimu ya umiliki wa ardhi kwa wananchi kama njia ya kuwakwamua katika dimbwi la umasikini.

  Mbunge Filikunjombe ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakati wa kuwashukuru wataalam kutoka mpango wa MKURABITA ambao walikuwa wakitoa elimu ya umiliki wa ardhi katika wilaya hiyo.

  Amesema kuwa wahisani wa kuwekeza katika wilaya ya Ludewa ni wengi ila wanasubiri utayari wa wananchi wa wilaya hiyo na mipango ya viongozi katika kuvutia uwekezaji wa ndani katika wilaya hiyo ambayo ipo mbioni kuanza kunufaika na madini ya liganga na mchuchuma.

  Mbunge Filikunjombe amesema kuwa uwezo wa kuendelea kuifanya Ludewa kuwa wilaya ya kipekee kiuchumi anao ila peke yake hataweza pasipo kuungwa mkono na viongozi na wananchi wa wilaya hiyo.  MBUNGE WA JIMBO LA SONGWE PHILIPO MALUGO
  AWAASA VIONGOZI WA VIJIJI KUWA WAWAZI

  [​IMG]
  VIONGOZI wa vijiji na kata ya Kanga Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuwasomea wananchi misaada na vifaa ambavyo vinatolewa na Mbunge wa jimbo Songwe Bw. Philipo Mulugo kwa ajiri ya kusaidia uhjenzi wa shule za swekondari na msingi ili kuondoa maneno kwa wananchi.

  Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mkoani Mbeya Esther Macha anaripoti kuwa hatua hiyo inatokana na Kauli ya Mbunge huyo baada ya kuwauliza wananchi kuhusu kupata msaada wa mifuko 50 ya saruji ili ziweze kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Kanga.

  Akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Tete juzi , Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Bw. Philipo Mulugo alisema kuwa kitendo chja kutotoa taarifa kwa wananchi kuhusu misaada inayotolewa na Mbunge huyo ni kutengeneza maneno ambayo matokeo yake si mazuri.

  “Unafikiri mimi kama Mbunge wenu wanananchi watajisikiaje kama nimehaidi jambo msaada harafu viongozi mkae kimnya inajenga picha gani hapa hebu badilikeni ndugu zangu hiki kitendo si kizuri kabisa kwani sijakipenda mkifanya mikutano yenu waelezeni wananchi nini nimefanya siyo kukaa kimnya jamani”alisema Bw. Mulugo.

  Hata hivyo alimtaka Mwenyekiti wa Kijiji hicho kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara kuwasomea wananchi misaada au vifaa vinavyotolewa na mbunge si kuona misaada hiyo ni kitu cha kawaida na kuacha kutoa taarifa kwa wananchi.

  “Ndungu yangu Mh. Diwani mimi na wewe sote ni wa kuchaguliwa hivyo ni vema ukawa unatoa taarifa kwa wananchi siku ikifika tutakuja kuambiwa hatujatekeleza ahadi tulizotoa sawa ndugu yangu Mh. Diwani”alisema

  Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijijiji cha Kanga Bw. Vicent mpanzo alisema taarifa ya msaada huo alitoa katika mahafali ya darasa la saba shule ya msingi kanga.

   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Wote ni wasanii/wanafiki. Kwani Makala, na ufisadi wake, hamjui huyo mwizi (muwekezaji) aliyevamia ardhi ya kijiji? Hiyo ni sera ya Magamba na Makala ni gamba la mamba.
   
Loading...