Wabunge ni walevi - Chiligati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge ni walevi - Chiligati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 21, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  1 )"Kwa hiyo tumesema inatosha, hapo tulipofikia tusiendelee mbele. Wanaoropoka hovyo ni walevi ....! - Chiligati

  Chiligati ni kimbelembele na anajiona yeye ni mwenye kupendeza ndani ya serikali hii kumbe hajui kama amekalia kuti kavu,Cheo alichonacho kinamfanya ajione yeye ndio mwenye kauli ya mwisho ,mambo ya kuwaita watu walevi yalitokea kwa kuitwa viongozi kuwa ni walevi wa gongo sasa yeye anendeleza kuwaita wabunge watetezi wanaoihoji na kuijadili pamoja na kufikisha ujumbe kwa wananchi kuwa ni walevi ,hili wabunge wapo na watamueleza vilivyo ili ijulikane nani mlevi

  2)
  Njia sahihi, alisema, ni malalamiko kushughulikiwa kulingana na taratibu za chama na siyo kuyasema majukwaani ili kuufurahisha umma - Dk Mahanga, ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi.

  Naibu huyu hajui analolisema maana mafisadi hawazungumziwi katika ngazi ya Chama bali wanazungumzwa katika ngazi ya Taifa hivyo anashindwa kutofautisha Chama na Bunge,anasema zitumike taratibu za chama katika mambo ya kiTaifa, pia amezidi kujidharaulisha pale aliposema wanafurahishwa umma ,yaani wananchi kufahamu na kuelezwa mambo ya ufisadi haihusu na wananchi hao hawana uwezo wa kufanya lolote lile,amesahau kuwa wananchi ndio wanaowachagua wabunge ,ila hapa ifahamike tu wabunge wengi wa CCM hupitishwa kwa njia za panya kama alivyopitishwa yeye Mahanga.

  Mahanga anashindwa kufahamu kuwa mambo ya ufisadi sio ya kuzungumzwa katika vikao na kamati za siri bali ni mambo ambayo yanahitaji kila mwananchi ayajue na inapotokea mtu kufukuzwa wananchi wasione ameonewa, mficha uchi hazai ndivyo wahenga wanavyosema kwa maana hiyo kama tukiendelea kuficha na kuzungumza ndani ya vikao ya siri hakuna maendeleo yatakayopatikana..

  3) Kuna haja ya wabunge kudhibitiwa kwa sababu wengine wamefikia hatua hata ya kuwakejeli viongozi wa serikali badala ya kutumia hoja katika kujenga hoja.- Shelukindo
  Mwengine huyu anasema kuwajadili viongozi kwenye bunge ni kuwakejeli sasa atueleze ni wapi viongozi wajadiliwe ikiwa mienendo yao inaenda kinyume na utaratibu wa uongozi kwa maana Mkapa alienda kinyume na taratibu za kiutawala na sheria za nchi,wapi akajadiliwe ?

  Majibu waliyoyapata CCM baada ya kikao chao cha siri au NEC.
  Spika Samuel Sitta ambaye alikuwa kwenye wakati mgumu wakati wajumbe wapatao 22, walipopendekeza atimuliwe kwenye chama, bado ana msimamo wa kuendeleza vita ya ufisadi.

  Wabunge ambao majina yao kapuni.
  "Kama kuna watu serikalini au wabunge wanaofurahia msimamo huo wa Nec, wajue wanajidanganya kwa sababu hauna nguvu yoyote ya kudhibiti uhuru wa bunge,"Bunge lina nguvu ya kujadili mambo ambayo si spika wala Nec wanaoweza kuizuia."  "Kama suala ni uhuru ambao umefanya wabunge kuvuka mipaka na kila mmoja kuamua kufanya lolote bungeni, basi Nec isingesema na kuacha tu hewani. Ingeorodhesha kanuni zilizovunjwa na wananchi wakaelewa,"


  Tunawataka wananchi kuondoa shaka kuhusu uamuzi huo wa Nec akisema kuwa wao kama wabunge wako imara na wataendelea kutetea maslahi ya wananchi bila kuogopa. - Christopher Ole Sendeka mbunge CCM.  "Sidhani kama kuna mtu amefungwa mdomo na Nec.

  Mdomo upo palepale na watu wataendelea kuongea. Nec haiwezi kumfunga mdomo spika wala wabunge
  "Tumeisikia Nec, lakini wavumilie tu kwani lazima mabadiliko yatokee. Wananchi ndio wenye chama na ndio wanaotaka wabunge wao wapambane na uovu na ufisadi,"Ni lazima watuhumiwa wa rushwa wafikishwe mahakaman.-Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro


  Kazi kwenu CCM mnavuna mlichopanda watu hawarudi nyuma tena kuogopa makeke na vishindo vyenu.


   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nadhani haya ndiyo matokeo ya kuwa na viongozi .. (Wanajeshi) + (Waliofoji vyeti) + (waalimu)?
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Solution ni moja tu.. Kuchukua Bunge toka CCM basi! haya ya Spika ni matokeo ya kuchagua wabunge wa CCM ambao ndio wasemaji wakubwa ktk viukao kama hivi. Kama bunge lingekuwa limetawaliwa na Upinzani haya yote yasingezungumzwa.
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  kwenye hiyo listi ya walevi na chiligani nae yupo kwa kuwa nae ni mbunge, au hajui hilo
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Aneropoka ovyo ni mlevi ,kwa maana yale madai yanayotolewa bungeni yote huwa wanaoyatoa wameshapuliza au kunywa ulevi wa tende ,ndio maana yake yeye si katika wanaosikitishwa na mafisadi wala wafanya biashara ikulu.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MIMI kama geoff,kwa mbaali naiona taswira ya uongozi bora some x-years ahead!
  bravo sitta
  bravo slaa
  bravo mwakyembe
   
 7. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2009
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mishahara Milioni 8+, kwa ajili ya WALEVI????
   
 8. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naomba tukumbuke tu kwamba haya ni matokeo ya kura zetu (kwa wale tuliochagua CCM). Na hali hii itaendelea hivyo mpaka siku tuseme basi sasa imetosha. Ni hali ya kusikitisha sana kwa kweli.

  Kwa mimi mwananchi wa kawaida sioni kama spika alivunja kanuni yoyote ya kuendesha bunge, na sioni kama amekiuka maadili yoyote ya kiuongozi. Kitendo cha wajumbe wa NEC kusema alikuwa anaruhusu mafisadi kujadiliwa ni kitendo cha aibu sana. Ni kitendo kinachodhihirisha kwamba CCM imejaa mafisadi ndio maana hataki kujadiliwa bungeni.

  Wananchi hatulioni hili? Shime jamani watanzania tuamke usingizini na kusema basi. Adui wetu mkubwa ni CCM. CCM ndio inatupelekea kuwa hivi tulivyo, yaani masikini wa kutupwa. Sasa, tuseme basi.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Inauma sana kuona hali hii watawala kutugeuza sisi wananchi mazuzu wkt sisi ndo tumewaweka madarakani leo hii tunaoneka hatufai mbele ya macho yao imradi tu wanapata masrahi yao binafsi huku wakituacha ss raia tukitanga tanga.
   
 10. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Itakuwaje jamaa wakiamua kuomba muongozo wa Spika juu ya kauli ya Chiligati kuwa wabunge wanaoropoka ovyo ni walevi na kuwa bunge imekuwa kama The Comedy...! Hili akiuliza kiongozi wa upinzani bungeni ndio itakuwa funga kazi....
  1. Ataje ni kina nani wanaropoka ovyo
  2. Kitu gani hicho ambacho yeye anaita kuropoka ovyo
  3. Kufananisha bunge la Jamhuri sawa na The Comedy si kuwadhalilisha watanzania na katiba ya nchi

  Patakuwa patamu......!
   
 11. B

  Burton New Member

  #11
  Aug 22, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mgeni kabisa katika uchangiaji lakini ni msomaji mzuri sana wa JF. Naomba niulize. Kuna mtu ameniambia kuwa mwenyekiti wa CCM katika hatua zake za awali wakati anaanza kampeni za kugombea urahisi alitamuka kuwa "atatengeneza matajiri 100 katika kipindi chake ambao wataweza kuwakwamua wengine katika dimbwi la umasikini". Matamshi haya hakuendeleza katika kipindi chote cha kampeni na badala yake akawa na "maisha bora kwa Watanzania wote". Inawezekana hao watu aliyotaka kuwatengeneza matajiri walimshauri kuwa itakuwa noma kuanza kuzungumza katika wakati huo wa kamapeni watu wasije kustukia hiyo dili na pengine utajiri ule ulikuwa ni kukomba mali za nchi. Kama kweli alitamka hayo maneno, ina maana hii ilikuwa sera ya chama ambacho sasa kinajulikana Chama Cha Mafisadi (CCM). Na ni kwamba, sasa sera hii inatekelezwa kichini chini. Wana CCM ambao wanapiga kelele za mafisadi hawajashirikishwa katika kutekeleza hii sera wakati akina chiligati, kusila, mahaga wanaijua hii sera. Je ni kweli alisema hayo maneno?. Naomba kutoa hoja ndugu zanguni.
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,675
  Likes Received: 21,908
  Trophy Points: 280
  Nadhani alikuwa anamaanisha yule Naibu waziri aliyetoa majibu ya HOVYO HOVYO Bungeni kuwa ndio Mlevi (joke)
   
 13. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee amejisahau kewa sisi kama wapiga kura ndo tunaye muweka mjini? Ajaribu kuchuja kauli zake kama anataka kuwepo sama mjini.
  Lakini ni kawaida ya watu ambao hawana sera kuwa waropokaji!
   
Loading...