Wabunge ndio Adui mkubwa wa Maendeleo.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,799
48,939
Tujiulize walikuwa na maslahi gani kupitisha miswada ya mikataba ya Madini, Gesi na Mafuta isiyo na maslahi kwa Taifa?

Kwanini tusianze nao, tuunde tume ya kuwachunguza na kuwabaini wabunge wote walioshabikia kuandaa na kupitisha miswada ya kinyonyaji, wakiwemo waliokuwa wajumbe wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini wakati huo, tukiwabaini tuwa label 'Maadui Wa Taifa'.

Haiwezekani leo wabunge wengi wao kutoka CCM eti waongee kwa uchungu kana kwamba hawajui wao ndio walihusika kupitisha miswada, mikataba na sheria mbovu kwa maslahi yao, wengine tunawajua walishuhudia ikisainiwa hotelini nje ya nchi.

Wabunge ndio wabaya wetu, rekodi za Hansard zipo, video clips zipo na wabunge waliohusika wapo, kwanini tutafute mchawi wakati mchawi anajulikana?

Kwa mawazo yangu wabunge ndio chanzo cha haya yote rais anayohangaika nayo.

Naomba kuwasilisha.
 
Hii VAT ya utalii mwaka jana, Wabunge wa CCM wakapitisha budget ya Maghembe kwa 100%

Madhara ya VAT ni makubwa, hawajafanya thathmini...bado mwaka huu wamelete Concession fee

Wabunge wa CCM ndio wanaopitisha kwa wingi wao Bungeni...

Serikali inawaza kuvuna kodi nyingi kwenye utalii badala ya kuwaza jinsi ya kuboresha utalii
 
Back
Top Bottom