SoC02 Wabunge nchini wafanye haya kuleta tija kwa wananchi wao nchini na kukuza vyama vyao kisiasa

Stories of Change - 2022 Competition

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Wabunge ni viongozi wenye nguvu kubwa ya mtaji wa watu nchini, nafasi yao katika maeneo yao ni viongozi wanaobeba shida za jamii, mapendekezo kwa serikali na shukrani za wananchi kwa serikali.

Mbunge ni kioo cha jamii yake na ana nafasi kubwa ya kufanya mapinduzi ya kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kiuchumi katika jiografia yake.

Tanzania, Bunge ni mhimili mkubwa wa kutunga sheria na kufanya mijadala ya sauti za umma. Waheshimiwa Wabunge wanaporudi majimboni ndio sehemu inayowapa tathmini kuona wamefanya nini kuleta tija kwa wananchi wao. Ikumbukwe wabunge ubeba bendera ya chama na chama umtegemea kukibeba kuvuka jimbo hadi Taifa.

Waheshimiwa Wabunge nchini wafanye haya kuleta tija kwa wananchi wao nchini na kukuza vyama vyao kisiasa.

Wajiwekeze katika kuanzisha fursa endelevu zitazoibua vipaji na ajira endelevu nchini katika majimbo yao. Wabunge ni viongozi wenye kujiwekeza kwa jamii, lakini kujiwekeza kwao wengine wanakosa tija ya nini cha kufanya kiweze kuibua vipaji eneo lake na kutoa ajira endelevu. Nashauri wangewekeza katika matamasha ya sanaa na ubunifu yatajumuisha watu wenye vipaji mbali mbali, ingeunganisha wasanii jimboni, wakapeana mikakati, namna ya kutengeneza fedha, kuaminiana na kupata vikundi vya kukopa, kufanya kazi pamoja na kupata wadau, tuachane na ligi za mipira.

Watambue wana jukumu la kuvuna wanachama. Wabunge ni kundi kubwa linaloweza kuongeza ama kupunguza wanachama na hata kukifanya chama cha kisiasa kikose mvuto. Wabunge wengi, baada ya uchaguzi suala la kuanzisha chochote kuvuna wanachama bado ni tatizo. Ni jukumu lao, kwa kutumia mbinu na mikakati iliyo na msukumo hai wa kugusa maslahi ya watu kuona tija ya kuchukua kadi za chama chake.

Mfuko wa jimbo wautumie kutatua matatizo ya jamii na miradi midogo yenye tija. Mfano tundu za vyoo shuleni, visima, vifaa vya ufundishaji, pembejeo za kilimo na vifaa tiba, kuzibua visima vilivyo kauka na maafa.

Wafundishe vijana kuvua samaki na sio kuwapa samaki haisaidii. Vijana ni kundi kubwa linalonufaika kupitia ziara na kampeni. Japoi vijana wachache na pesa za msimu. Ni lazima Wabunge, waone cha kufanya kusaidia vijana wapate fursa za uzalishaji mali kama kuwakopesha, kuwapa elimu ya ujasiriliamali, kuwasemea wizarani waweze kupata fursa za kitaaluma na siziso za kitaaluma. Kila Mbunge aangaike na shida za watu wake.

Waanzishe mifuko ya kusaidia watu wenye mahitaj maalum, mtoto wa kike, kuhamasisha umuhimu wa elimu na kuboresha afya kwa watu wenye mahitaji maalumu. Ni ajabu Mbunge kutokuwa hata na mfuko wake binafsi wa kusaidia kundi lolote maalumu kama taulo za kike, vifaa kwa walemavu, huduma za afya na upasuaji kwa msimu hata mmoja katika jimbo lake. Wapo wabunge wanasifa nzuri za kujali makundi maalum.

Wabunge wenye taaluma na vipaji waone fursa kukuza taaluma na tasnia zao nchini. Wapo wabunge ni wasomi, elimu zao hazijaonekana na wengine wameshindwa kuziendesha wizara na kutolewa katika wizara hizo, Wabunge wasanii na wanahabari ila hawajaweza kuleta tija kukuza sanaa na habari, wanapaswa kuangalia njia bora ya kukuza tasnia zao ndani ya mfumo wa serikali au nje ya mfumo wa serikali kwa kuthubutu wao wenye kufanya kitacholeta matokeo chanya.

Waache kuwaza kufanya makubwa waanze na madogo ya kugusa maslahi ya wengi. Wabunge uwaza makubwa kuyafanya lakini watu wengi katika majimbo ni maskini wanahitaji huduma bora za afya, maji, elimu na kuwezeshwa katika shughuli zao za uzalishaji mali. Mfano vipo visima vya wananchi wangeweza kuviongeza urefu na wapo wachimbaji wa kawaida wangewapa kazi wakaweza kusaidia wanajamii kupata ajira na wananchi wakapata visima vingi zaidi kuliko kuwaza kutumia fedha nyingi kwa kisima kimoja.

Wabadilishe ama kuingiza na watu wengine kwenye timu zao za kisiasa kuonyesha ni viongozi wa watu. Kuna minong'ono ya timu za wabunge kuwa ni watu wale wale, hii inafanya watu waone viongozi hawana imani nao na ni viongozi wa watu wachache wanaonufaika nao kisiasa. Na mfumo huu ndio unaofanya baadhi ya wabunge kuwa na washauri wabovu. Kubadilisha watu ama kuongeza itawasaidia kupata mawazo mapya na wafuasi wapya.

Wajiwekee ukomo kuleta mgawanyo sawa wa rasilimali. Wapo wabunge wanazeekea bungeni na kufia bungeni, sio suala jema, nashauri wajiwekee wenyewe ukomo na kuwapa nafasi wengine ikiwa ni namna njema ya uongozi wenye tija kwa kizazi cha leo na kesho. Ni bora wakaandaa hata watu wenye kuona watawapokea vijiti na kuwanadi kisiasa.

Wawekeze katika viongozi wa chini kujua changamoto za watu wao. Serikali ina mipango na watu wake ila wabunge ndio watu pekee wanaokuwa karibu na wananchi. Ni lazima kuwekeza chinii ili kuibua changamoto katika jimbo, kila kijiji kina uongozi wa serikali za mitaa, watumie hawa kuzibaini shida, ila lipo tatizo baadhi ya wabunge wanawadharau viongozi wa chini, mikutano yao inaanzishwa hata serikali ya kijiji haijui wala mualiko. Ni tatizo, wanapaswa kuungana na viongozi wa chini kupata taarifa rasmi.

Watambue wao ni taasisi wanajukumu la kupiga debe maendeleo ya Taifa.Kama kuvuta wawekezaji na wadau mbali mbali wa maendeleo ndani na nje ya nchi. Tuna Wabunge ni wafanya biashara wakubwa nchini, wachimbaji wa madini, maprofesa, wanawafadhili wa miradi yao na wameweza kusafiri kimataifa na wengine kupewa tuzo na vyuo vya nje. Watumie hizi fursa kuendeleza sekta za utalii, kilimo, soko la nje, elimu, afya na kuwafumbua macho watu kuziona fursa katika majimbo yao. Wanapaswa kuibeba kauli ya Raisi kuleta maendeleo nchini sio mpaka maagizo.

Wasilewe na nafasi za Uwaziri. Utajifunza wapo Waheshimiwa Mawaziri wanafanya kazi nzuri sana katika wizara ila upande wa majimbo yao bado, hata katika kipindi kilochopita wapo waliokosa kura za maoni japo utendaji wao ulitukuka katika wizara. Mbali na kupewa wizara ni lazima wajitume kwenye majimbo yao, kwani kilichomuweka ni kiti cha ubunge na sio Uwaziri na sio Bunge bali wanachama na wananchi ni lazima wacheze vizuri pande zote.

Watumie mbinu za matembezi vijiji kwa vijiji kuhamasisha maendeleo na kutangaza vyama vyao kisiasa. Watu wanashauku na wabunge wao na wanashauku ya kuona wanaambiwa chochote na kushirikiana na Mbunge wao katika shughuli yoyote, kukaa katika mikutano haitoshi ni lazima ushiriki wako wa moja kwa moja kwa wananchi uwepo, Mbunge kwa msemo wa leo ni Chawa wa wananchi.

Wito wangu kwa Wabunge nchini, nyie ni wanajeshi mliopata bunduki zitumieni kuwaokoa wengine na mkumbuke nyie ni viongozi wa wananchi sio watumishi wa serikali. Utawala unatega siko kwenu bila Bunge hakuna maisha bora.
 
Back
Top Bottom