Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Niko viunga vya kinondoni kila napopita nasikia mtulia ,mtulia hakika huyu kijana anakubalika sana

Nimtakie heri ya ushindi
 
Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.


Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).


Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.


Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.


“Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.


Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
Mwisho.
Kauli ya ndugulile ni ya hovyo. Inatosha kubatilisha matokeo ccm wakishinda. Ilitokea miaka ya nyuma bunda warioba alipogombea na mkondya.
 
ccm lazima tushinde asubuhi namapema,yaliofanywa na magufuli hadi sasa nkiashiria tosha kupata kura za kishindoo
 
Watanzania bhana sisi ni watu wa ajabu sana inamana mtu hawezi kuletewa maendeleo akiwa upinzani ndo matokeo yake mtu anakuja na hoja dhaifu eti kwa kuwa alikuwa upinzani ndo mana hakuweza kuwatumikia kwa ufanisi wananchi huo ni ujinga mkubwa tena kwa mtu mwenye hakiri timamu kama mimi huwezi kunidanganya na hoja za kitoto kama hizo na ndo mana trump anaposema viongozi wa Africa hawawezi kujitegemea hata kimawazo mtu anachukia lakini nashindwa kuelewa unachukia nini kwa nini usijichunguze sasa kama mtu anahama kwa hoja ya kipumbavu namna hyo huyo anafaa kuwa kiingizi kweli?
 
Asante kwa taarifa.Kampeni za Chadema zimesimama?Siwasikii siku hizi
Haya mafuriko ya leo hayo
IMG-20180211-WA0006.jpg
IMG-20180211-WA0002.jpg
IMG-20180211-WA0006.jpg
IMG-20180211-WA0002.jpg
IMG-20180211-WA0010.jpg
IMG-20180211-WA0008.jpg
 
Jamani mbona kuna majimbo ya maccm tangu uhuru yako hoi kabisa kimaendeleo ,nenda misungwi barabara mbovu ajabu, nenda kwimba, sengerema,sumve na sehemu zingine nyingi tu.
Ndio nashangaa ssa hilo jimbo la kinondoni miaka zaidi ya 50 lilikuwa chini ya CCM hawakutekeleza hayo eti leo ndio wanaahidi watayafanya ndani ya miaka 2?? Cjui watatumia miujiza gani !!!
 
Nafikili hata akishandinda Mtulia ...itakuwa ndo mwisho wabunge kujiuzuru...maana Mtulia sasa hivi anapumulia machine ICU alidhani atapata ubunge kirahis ...kumbe kazi sio rahisi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom