Wabunge na wawania ubunge wazuiwe kutoa misaada/zawadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na wawania ubunge wazuiwe kutoa misaada/zawadi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by akajasembamba, Jan 1, 2011.

 1. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunaelewa na ipo katika katiba ya nchi kwamba kazi za Wabunge na Bunge ni KUTUNGA SHERIA na KUISIMAMIA SERIKALI, kifupi ni kuwakilisha wapiga kura wake bungeni, pale ambapo serikali inagawa NATIONAL CAKE/BUDGET kila mwaka basi Mbunge naye atoe hoja ya kutetea hiyo National Cake iende kwa kiasi gani jimboni kwake, na pia kazi za Mbunge ni kupitisha SHERIA, zile sheria ambazo anaziona zitaathiri wapiga kura wake basi anatakiwa atoe hoja za kupinga kupitishwa sheria hiyo, cha ajabu tunaona wabunge wanachaguliwa kwa kutozingatia mantiki na maana ya Mbunge, kigezo kikuu na cha kwanza cha Mbunge ni UWAKILISHI na UWEZO KUJENGA HOJA, kwa niaba ya Wapiga kura wake. Inasikitisha kuona Wadanganyika wamepumbazwa na kunajisi tafsiri ya Ubunge na kugeuza kwamba Mbunge ni MFADHILI WA JIMBO badala ya MWAKILISHI wa jimbo, mbunge hatazamwi tena kwa uwezo wake wa kujenga hoja na kuwakilisha wananchi wake bungeni, badala yake ni kwa kiasi gani ametoa na ana uwezo wa kutoa misaada kwa wananchi wake, hata akienda kushona mdomo wake bungeni na kusinzia bungeni miaka 20 hatujali tena! matokeo yake bungeni zinapitishwa sheria kandamizi bajeti za kifisadi etc etc. Matokeo yake mikoa fulani imeng'ang'ania kuchagua wafanyabiashara, ambao wengi wao ni wenye asili ya kiarabu na kihindi! Na la kustaajabisha kabisa watu utawasikia wakimsifu Mbunge kwa kujenga shule, visima,kutoa vyarahani nk nk wakati mbunge huyo huyo ameachia mabilioni ya fedha yanapitishwa bungeni kama bajeti ya vitafunwa na mambo mengine ya ajabu, HATUCHAGUI MBUNGE ATOE HELA MFUKONI MWAKE, ila tunataka aibane serikali irudishe majimboni kwetu hela yetu tunayokatwa kodi kila kukicha. Mbunge akichimba kisima au kujenga shule DED,DC,Waziri nao wafanye nini na wapo kwa madhumuni gani? Au la mfumo ubadilishwe tuwe tunachagua MAGAVANA ambao watakuwa na mamlaka ya kiutawala, siyo upotoshaji ulio sasa ambao utaendeleza ufisadi. Ni muhimu sana pia Wabunge wazuiwe kuwa Mawaziri, utawakilisha vipi jimbo nawe ukiwa waziri, pia unakuwa na unfair advantage katika uwanja wa kugombea ubunge, huenda ukachaguliwa kwa uwaziri wako, hatushangai wengi waliopita bila kupingwa ni Mawaziri watarajiwa.Suluhisho wabunge na wawania ubunge wazuiwe kutoa misaada misaada ya aina yeyote ile, kwa kuwa wapiga kura wanapumbazwa na tunapata wawakilishi wabovu. Kwa kuzuiwa kutoa misaada na zawadi ndiyo wadanganyika wataelewa maana halisi ya Mbunge.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watakuambia ni kawaida ya waafrika kukirimu wapiga kura ambao hawajiwezi! Wananchi nao wanajifanya kama vile ni haki yao kufadhiliwa na ndo hapo wabunge wananyakua points haramu za kutumia umaskini huo kuwatumia kama ngazi!
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Lakini jamani si wanasaidia wapiga kura wao kimapato ambapo at least umaskini unapungua?
   
 4. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo utoaji wao misaada unapotosha kazi yao ya UWAKILISHI na unatumika kuwa KIGEZO cha kuteua Mtunga sheria na Msimamizi wa Serikali! Tatizo ni hilo tu, tutakosa wawakilishi bora kwa kuchagua wafadhili bora!
   
 5. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  misaada wanayotoa badala ya kuleta maendeleo, inapunguza na inazidi kusababisha fedha za umma zizidi kuliwa kwa kupitishwa bajeti za kifisadi bungeni, hawawajibiki kwa kuisimamia serikali,wanawajibika kwa kutoa vijizawadi majimboni! na hawataweza kamwe kuleta maendeleo kwa misaada yao finyu hata wawe matajiri vipi, hela za wananchi zinavuja bungeni
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu umejenga hoja vizuri sana lakini nashangaa unavyomumunya maneno unaposita kutaja mikoa inayoshabikia wahindi,waarabu,na wasomari,bado tu wachina.Mikoa hiyo ni MOROGORO,TABORA,SINGIDA NA MTWARA.Sijui wakazi wa mikoa hii huwa wanajisikiaje kuchagua hawa wageni?ni kama hakuna vijana wao wenye uwezo wa kufanya kazi hizo!!!
   
 7. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mheshmiwa Tukutuku nilidhani Mikoa hiyo ipo wazi na inajulikana, ila kwa faida ya wale walio mbali na matukio ya TZ, ni Morogoro na Tabora zaidi, kwa Wanyamwezi, Waluguru, Wapogoro, Wandamba, Wakaguru na Wavindunda! wao wameona kuchagua wafanyabiashara matajiri wahindi na waarabu ndiyo kupata wawakilishi bora bungeni, bila kujali huo utajiri wao wameupata wapi kwa njia halali au haramu!tunajua kila raia ana haki ya kugombea nafasi ya uwakilishi ila cha ajabu ndugu zetu hawa wao wameng'ang'ania wanyabiashara matajiri weupe, matokeo yake tuliona Wabunge wao wanaongoza kwa kuwa MABUBU, Bungeni Dewji na Rostam Aziz wakiwa wamechangia michango michache kabisa au kutochangia chochote bungeni, na wanajua kuwa wao bungeni wanaenda as a mere formality tu hawana haja ya kuhoji chochote serikali, wao wakimaliza ni kwenda kugawa vijisenti tu majimboni na siyo kusimamia Bajeti! Its a shame and a total misconception of the term Member of Parliament as a Representative of his/her constituency.
   
 8. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuna kazi kubwa kuelimisha kuhusu uzalendo ili tufike mahali pa kuona vijana wetu wana uwezo wa kutuongoza badala ya kuendelea kuchagya warabu na wahindi. Kuna waafrika wangapi katika bunge la india?
  :clap2:
   
Loading...